Naona shule zimeanza ukorofi, wanatoza ada ya muhula ambao wanafunzi wamekuwa nyumbani

UNALIPA MTOTO USAFIRI 200"000
EMBU TUSAIDIANE WAMEBRBWA NA NANI HII LIKIZO MPAKA HIZO HELA TUENDELEE KULIPA AISEE LOH
 
Nilishawahi kuleta hii mada. Sema kipindi hicho wengi hawakuielewa sababu hayakua yamewakuta tayari. Janga la Corona na mustakabali wa ada kwa wanafunzi
 
Na chakula?na usafiri? Mali bila daftari hupotea bila habari,ngoja nikuulize,kunatofauti gani kulipia pesa ya chakula na usafiri na tofauti ya kwenda kutupa hela shimoni?utalipiaje msosi wakati Mtoto yuko home?au usafiri?
 
Wanadai hata pesa ya chakula wakati hakukuwa na wanafunzi mashuleni,wanadai ada wakati hawakufundisha,wansema ni kwa ajili ya mishahara , ninavyojua mshahara unalipwa baada ya kufanya kazi,na ni jukumu la shule kuwalipa mishahara wafanyakazi wake na si kutegemea ada ya wanafunzi ambao hawajafundishwa.Ni funzo kwa shule kubuni miradi au kuweka vitega uchumi kwa ajili kupata mishahara ya wafanyakazi wao, kama hali ni ngumu kwa shule na hata sisi wazazi nasi tuna hali ngumu.Huu ni wizi ,serikali iingilie kati
 

Una tatizo wewe kulazimisha mtu aone sijui nini!!!
Umeandika kama vile watawakalisha macho hadi midnight au watakaa nao madarasani hadi jioni
 
Likizo ndefu huwa June na watoto wametumia June nyumbani. July shule huwa zinafunguliwa. So huna hoja kaa pembeni
 
====
(1) Shule za binafsi hazijalipa mishahara kipindi cha Corona na hawatalipa walimu. Hiyo jazal imewapa walimu wake likizo bila malipo.
(2) Hatakama watasomesha content yote lakini gharama ya chakula na huduma zingine mwanafunzi hawajibiki kulipia kwani hakutumia.
(3) Wanafunzi wa darasa la saba wanamaliza mitihani October 8. Hakuna logic ya 125 kwa kundi hili.
(4) Kama unachosema ni kweli kwamba semester ni siku 96 na hao wanakaa 125. maanna yake 125-96 (june december)=29 Unamaanisha chakula cha ziada ni siku 29. So wazazi kwanini walipie miezi 3? Tumia akili...
 
====
Kufundisha na kutoa maswali sio kitu kimoja. hata wazazi tulikuwa tunawapa maswali. Pili, shule ya jazar wanafunzi waliosoma online walilipishwa pesa ya kugharamia huduma huzika.
 
Mtoto bado Yuko chekechea unamlipia kwa mwaka milion 2.5 bado hajafika shule ya msingi , secondary na chuo halafu anakuja kulipwa mshahara wa laki 9 ...


Wazazi fikirini nje ya box
Hizo ni biashara kama biashara nyingine tu mkuu wazazi wanatakiwa kuchagua kama vile wanachagua bidhaa nyingine sokoni, La huwezi lipia 2.5m mpeleke mwanao Kayumba kwa manufaa ya kipato chako .
 
Tutaelewana tuuu. Wacha tuonyeshane makali.... in dokta SHIKA voice...
Mama kalibutua kombolera watu kimyaaaaaàa. Nawaonaaaa mlivyokuwa mna hanyaaaa
 
Mie nawadai hela ya mwezi mmoja ya ada,usafiri na chakula maana ilikuwa inaisha April ila march 17 wakakatisha!!

Wote ni hivyo hivyo lakini haya mashule yapo kibiashara zaidi, hayataki kukubali hilo
 
Muongozo wa Wizara huu hapa mkuu,kwa hiyo wewe tulia tu.


*Wazari wa Elimu atoa maelekezo kwa shule binafsi.Asema watakao toza ada baada ya Corona kufutiwa usajili.

Waziri wa Elimu Prof.Joyce Ndalichako amesema serikali haitasita kuzichukulia hatua shule zote ambazo zitatoza tena ada kwa wanafunzi wanaotarajiankurejea mashuleni baada ya mlipuko wa ugonjwa wa corona.

Akizungumza leo mjini Dodoma Prof. Ndalichako amesema taifa lilipata tatizo na wanafunzi walishalipa ada hakuna haja ya shule kuanza kuchangisha tena ada nyingine kwa wananfunzi hao

“Watu waache kutumia corona kama kitega uchumi yaani watu wanaanza kuagiza hela za ziada za kazi gani Wanafunzi walishalipa ada kabla ya kufunga shule walienda nyumbani sababu ya changamoto za kitaifa sasa kwa nini uwalipishe tena ada” amesema


“Tusianze kuumizana kwa sababu ambazo hazina msingi wizara itafuatilia shule ambazo zinataka kutumia corona kama kitega uchumi tutazichukulia hatua hata kuzifutia usajili” ameongeza

Ikumbukwe kuwa mapema mwenzi Machi shule zote nchini zilifungwa kutokana na mlipuko wa homa ya mapafu (Corona) lakini kutokana na mwenendo wa kupungua kwa wagonjwa nchi Rais John Magufuli aliagiza kufunguliwa kwa shule kwa wanafunzi wa kidato cha sita pamoja na vyuo ifikapo Juni Mosi*


 
Muongozo huu hapa,ni marufuku kutoza ada baada ya Corona,watoto wapokelewe bila usumbufu wowote, walishalipa ada ya mhula mzima.




bWaziri wa Elimu Prof.Joyce Ndalichako amesema serikali haitasita kuzichukulia hatua shule zote ambazo zitatoza tena ada kwa wanafunzi wanaotarajiankurejea mashuleni baada ya mlipuko wa ugonjwa wa corona.

Akizungumza leo mjini Dodoma Prof. Ndalichako amesema taifa lilipata tatizo na wanafunzi walishalipa ada hakuna haja ya shule kuanza kuchangisha tena ada nyingine kwa wananfunzi hao

“Watu waache kutumia corona kama kitega uchumi yaani watu wanaanza kuagiza hela za ziada za kazi gani Wanafunzi walishalipa ada kabla ya kufunga shule walienda nyumbani sababu ya changamoto za kitaifa sasa kwa nini uwalipishe tena ada” amesema


“Tusianze kuumizana kwa sababu ambazo hazina msingi wizara itafuatilia shule ambazo zinataka kutumia corona kama kitega uchumi tutazichukulia hatua hata kuzifutia usajili” ameongeza

Ikumbukwe kuwa mapema mwenzi Machi shule zote nchini zilifungwa kutokana na mlipuko wa homa ya mapafu (Corona) lakini kutokana na mwenendo wa kupungua kwa wagonjwa nchi Rais John Magufuli aliagiza kufunguliwa kwa shule kwa wanafunzi wa kidato cha sita pamoja na vyuo ifikapo Juni Mosi


 
Ni nursery&Primary iyo.

Apo chukua miaka 3 nursery jumlisha miaka 7 primary.

Jumla miaka 10,mara 2.5million. italeta 25 million.

Sawa Kabisa na Deni la HESLB chuo kikuu.
Ni bora ukaweka benki akikua unampa afanye maisha....elimu yenyew haina uhakika mkuu
 
We endelea na miongozo yako tu katafute hela au mpeleke mwanao shule za kata ni bure acha vilio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…