Naona shule zimeanza ukorofi, wanatoza ada ya muhula ambao wanafunzi wamekuwa nyumbani

Naona shule zimeanza ukorofi, wanatoza ada ya muhula ambao wanafunzi wamekuwa nyumbani

Rudisheni pesa za wazazi,we are up to your necks.Miezi mitatu bila kazi imewafanya muwe desperate mpaka mnapanga ujambazi.Pumbafu kabisa.
Kiongozi mimi narudishaje pesa?

Binafsi namuandalia mwanangu ada tarehe 28 awasili shuleni. Uongozi wa shule ulitutumia ujumbe wenye mchanganuo mzuri. Kama mzazi nikajiridhisha.

Kuna haja ya wewe kujiridhisha pia.

Usitukane shule usitukane walimu.

Nafahamu pesa si chochote katika kile mwalimu anampatia mwanangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yote Haya yasingetokea kama Serikali ingezifanya shule zake kuwa Bora kama zamani.
Sasa Serikali yenyewe haiziamini shule zake wala walimu wake unafikiri wamiliki wa hizi shule wataogopa mtu?
Kuna dawa ndogo ya kukomesha hii biashara haramu....boresheni shule za umma mtaona kama kuna raia atahangaika na hizi shule.
Jambo lingine baya wapo watendaji wa Serikali wanatumika kuhujumu Elimu yetu kwa kuzipa sifa hivi private Schools na kuzididimiza shule za umma ili biashara zao za kuhuni ziendelee.
Boresheni mazingira, lipeni walimu wenu vizuri, weka top 10 kutoka public schools tuone kama hawajatia adabu.
 
Ukitaka kujua uchumi halisi was maisha ya mtanzania pitia huu Uzi.

Watu wanashindwa kulipa laki 1 au milion 1 kwa nchi inayojivunia kuwa tajiri na donor country. Haya ndio maisha halisi sisi watanzania sio hayo ya wanasiasa eti tuko vizuri.


Vizuri ya nyoko [emoji1]
Wewe ni mhuni flani asee!! Hapo juu tu umelalamika eti mtu kulipa 2.5m kwa chekechea,hapa tena umegeuka.
 
Waalimu wanalipwa mshahara, majengo yanalipiwa kodi au yana gharama za matengenezo, walinzi na gharama nyingine zinakuwepo hata kama watoto wanajifunzia nyumbani. Fedha hizo zinalipwa kwa njia ya ada. Ni sawa ada ilipwe semesta zote.

If you think education is expensive consider ignorance
hapo tunajua elimu ni gharama shida inakuja walikataa kulipa mishahara ya watumish wao kwa kipindi cha corona
 
Ndugu Mzazi/Mlezi;

*Kuelekea kufungua Shule(Toka likizo ya Janga la corona), ADA YETU ITAKUWA KAMA IFUATAVYO:-

1. Ili kuwapa wepesi wazazi katika kufanya Malipo ya Ada kutokana na Janga hili la korona, Uongozi umeamua kupunguza ada kwa kiasi cha Sh. 100,000/= (Shilingi laki moja). Hivyo bas:-

● Kiwango cha Ada ya awamu ya Pili(Mwezi March) ni Sh.500,000/= badala ya Sh.600,000/= hapo mwanzo.
●Awamu ya Tatu(Mwezi June) ni Sh.500,000/=
●Awamu ya Nne(Mwezi septemba) ni Sh. 500,000/=
● *Baada ya punguzo hilo, Jumla ya Ada kwa Mwaka huu itakuwa 2,500,000/= Badala ya 2,600,000/= hapo kabla.*

2. Mara tu Mwanafunzi atakaporipoti atatakiwa kulipa kiasi cha Tsh. 1,000,000/= (ambayo ni mjumuisho wa awamu ya Pili na ya Tatu kama ilivyoainishwa hapo juu)👆

●Ili uendeshaji wa Shule uende ipasavyo, mwanafunzi anatakiwa alipe kiasi chote cha Sh. 1,000,000/= (milioni moja) kabla ya siku ya kuripoti shuleni.

3. Kwa wanafunzi wanaodaiwa ada ya awamu ya kwanza wanatakiwa kukamilisha kiasi chote cha deni hilo pamoja na Malipo ya Awamu ya Pili na ya Tatu Sh.1,000,000/=

6. Wanafunzi wote wasiolipia BIMA YA AFYA TSH. 50,400/= wanakumbushwa kulipia katika akaunti za Shule na kukabidhi risiti hiyo kwa Muhasibu ili asajiliwe na kuweza kupata huduma ipasavyo.

Tunawaomba wazazi/walezi kukamilisha Malipo kama yalivyoelekezwa na Uongozi wa Shule ili kufikia Malengo yetu kwa pamoja.

N:B. Malipo yote yafanyike kupitia Akaunti za shule:-
AMANA BANK
Acc Name: IBN JAZAR ENGLISH MEDIUM SCHOOL
Acc No: 001120310750001

KCB BANK
Acc Name: IBUN JAZAR ISLAMIC ENGLISH MEDIUM NURSERY AND PRIMARY SCHOOL
Acc No: 3300618819

NBC BANK
Acc Name: IBUN JAZAR ISLAMIC ENGLISH MEDIUM NURSERY AND PRIMARY SCHOOL
Acc No: 048132000088

Kwa maelekezo zaidi:
0658514451 Mkuu wa Shule
0659907513 Muhasibu.

Shukran
Naomba kukuuliza he unajua mtoto wako anatakiwa kusoma siku ngapi kwa muhula? Anatakiwa kusoma siku 96 ila akirudi anasoma siku 125. Pili anatakiwa aongezewe masaa mawili ya kusoma kila siku. Mikataba mingi ina saa 40 mpaka 45 kwa wiki kati ya mwajiri na mfanyakazi. Kwa nyongeza hiyo no lazima wafanyakazi wafanye kazi masaa mawili ya ziada kila siku. Jumla ni masaa kumi.
Pia inahitajika kulipa mishahara ya April mpaka June kwa wafanyakazi wore. Hii maana yake tayari mmiliki anadaiwa. Kwa namna nyingine una mkataba Wa mwaka na mmiliki.Kwenye mkataba hakuna sehemu amesema atasamehe ada ikiwa mwanao atapata kile kilichokusudiwa kwa mwaka. Ninaona wamiliki wanayo haki ya kudai ada ya April-June maana watoto watafundishwa vyote walivyostahili
 
Wazazi tupunguze jazba.

Nilipata nafasi ya kuutazama waraka unaoelekeza kufunguliwa kwa shule zote.

Unawataka walimu/shule kufidia muda ambao wanafunzi hawakuwapo.

Shule zimetakiwa kuongeza muda wa masomo kila siku kwa saa mbili.

Muhula wa kwanza uliokuwa uishe mwezi June mwanzoni, kwa sasa utakamilika mwezi August mwanzoni.


Muhula wa pili hautakuwa na Likizo na wanafunzi watasoma mpka 18 December.

Sasa hapo ni jitahada za kumtendea haki mwanafunzi. Shule pia zitendewe haki.

Ada yako itasaidia kuinua hali za walimu ambao kila siku wamekuwa wakisemwa wanafanya kazi katika mazingira duni. Wazazi kwa pamoja tutimize wajibu wetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
je shule binafsi ambao hawakulipa mishahara watawalipa walimu wao
 
mzazi sio shareholder wa smile hizo gharama hazimuhusu yeye analipia mwanawe akiwa shule. Hayo magharama ya mumiliki shareholder sio mzazi. Usitafute kesi ukaburuzwa mahakamani
There lots of public school around. Why don't you take your son or daughter. No one has forced you to take him or her to those school sir.
 
je shule binafsi ambao hawakulipa mishahara watawalipa walimu wao
Kiongozi hilo jambo mimi kama mzazi kulijibia ni ngumu.

Tusubiri nyuzi za walimu baada ya wazazi kutimiza wajibu wao. Kama kuna waajiri wataleta ubabaishaji naamini wazazi lazima tutajua. Na hapo tutakuwa na uwanja mpana wa kuwagusa waajiri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Just let him vent at the last end he has two option..one to transfer his did k to government school or to pay the amount. Don't give him a platform.
Yani umeona hali za walimu tu,

Haujaona namna mtoto wako atakavyotendewa haki?

Wewe unapima muda wa mtoto kukaa shuleni au unapima kile alichotakiwa kukipata ndani ya mwaka mzima wa masomo???


Korona haijaletwa na shule.

Fikiri kwa pande mbili punguza ubinafsi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Just let him vent at the last end he has two option..one to transfer his did k to government school or to pay the amount. Don't give him a platform.
Ndio madhara ya kusoma shule za serikali, badili lugha kwani hii uliyotumia huielewi🙁
 
There lots of public school around. Why don't you take your son or daughter. No one has forced you to take him or her to those school sir.
My money forced me! it is not about which school!!!! but you can`t take my money easily!!! you have to abide to the contract sir
 
Back
Top Bottom