Naona wazazi wangu wamenichoka, ni muda sasa nami nianze kujitegemea

Acha tu hapa naishi na wazazi wangu tena wakunizaa ila naona manyanyaso yamekuwa mengi hapa nyumbani ngoja nichomoke mwisho wa mwezi huu
Mkuu naona kama haupo Sawa. Ngoja ukue kiakili ndipo utajua kama wazazi walikua sahihi au lah.

Angekua wakike ningesema ngoja aoelewe ataoata majibu ya usahihi wa wazazi
 
Mkuu nakushauri usitoke hapo home. Ni heri ukavumilia hayo unayoita manyanyaso, kuliko kukutana na mateso ya kuingia kitaa kurupu kurupu bila mipango.

Bado uko chuo, matumizi na mahitaji yako ni mengi sana. Nakushauri endelea kujipanga mdogo mdogo, make sure siku unayo graduate chuoni, tayari uwe na ramani kamili ya kuingia mtaani.

Yani kwa ufupi, uwe na double graduations. Yani unagraduate chuo, at the same time una graduate nyumbani.

Ila ukisema utumie hasira na kuondoka home sasa hivi bila plan, trust me, chance ya kupoteana ni kubwa mno, na hivi double kick na smart gin ni 2000? Sijui.
 
Ushauri murua sana kutoka kwa apostle asante mkuu maana na mm nimo humo aseee 😁😁😁
 
Pole sana kaka mimi nilishawahi kuambiwa namaliza chakula sababu mara nyingi mimi nakuwa wa mwisho kula kwahiyo Huwa najisevia wenyewe[emoji1787][emoji1787]
[emoji38][emoji38] acha tu ndugu Imagine unaambiwa unaacha mavi chooni tena kwa sauti kubwa utajifeel vipi hapo majirani washasikia yaani ni aibu tu maza ananitia mtaanj
 
Mkuu naona kama haupo Sawa. Ngoja ukue kiakili ndipo utajua kama wazazi walikua sahihi au lah.

Angekua wakike ningesema ngoja aoelewe ataoata majibu ya usahihi wa wazazi
Kivipi mkuu? unajua wazazi sametimes kuna maneno flani hivi akiyaongea hata mtu wapembeni atajua huyu anamnyanyasa mwanae
 
Mkuu hata mimi nilijaribu kuwa bize kidogo na sikutaka kushinda home nikaamua kukaa chuo mpaka saa 4 usiku ila kila nikirudi maneno hayaishi nasemwa sana
Shida ninayo Iona kwako unawategemea kwa Kila kitu hivyo huna budi kwenda na matakwa yao, ila kwangu mim ilikua ni kulala tu kula na mahitaj mengine yote sikuwahi omba kwao.
 
Ushauri murua sana kutoka kwa apostle asante mkuu maana na mm nimo humo aseee 😁😁😁
Mdogo wangu, fanya vyote ila usije ondoka home kwa jazba, maana kuna siku utahitaji kurudi hapo 😅
 
Mkuu me nimeshamvumilia sana bimkubwa na nimehmshajitahidi kumweka sawa (yaani asinichukie) ila kila nikijaribu kufanya kazi za hapa home maza bado anafoka nimeshajitahidi kuvumilia maisha ya hapa nyumbani ila sina amani wala furaha.

Hali hii inanifanya mimi nisishinde hapa nyumbani nakaa zangu chuoni mpaka saa 4 usiku na weekend naamua kusepa home nikawacheki wana ilimradi niyakwepe maneno ya bimkubwa mimi kumvumilia nimeshindwa mkuu mwisho wa mwezi huu nimeshapanga nasepa home potelea mbali changamoto za mtaani
 
Kivipi mkuu? unajua wazazi sametimes kuna maneno flani hivi akiyaongea hata mtu wapembeni atajua huyu anamnyanyasa mwanae
Haya kapange ili wapangaji wenzako wakakufurahie uvivu wako uliokukimbiza Kwa wazazi wako. Na siku ukirudi tena Kwa wazazi tunakupeleka Polisi.

Nakumbuka hili ni jaribio lako la pili maana la kwanza ulibandika kule Twitter nikakufukuza
 
Shida ninayo Iona kwako unawategemea kwa Kila kitu hivyo huna budi kwenda na matakwa yao, ila kwangu mim ilikua ni kulala tu kula na mahitaj mengine yote sikuwahi omba kwao.
Sasa mkuu kama kula home nakula usiku tu nikirudi na kama kuwategemea wazazi basi ni sehemu ya kulala tu ila mengi najitahidi kujihudumia mwenyewe ila manyanyaso bado hayaishi.
 
Haya kapange ili wapangaji wenzako wakakufurahie uvivu wako uliokukimbiza Kwa wazazi wako. Na siku ukirudi tena Kwa wazazi tunakupeleka Polisi.

Nakumbuka hili ni jaribio lako la pili maana la kwanza ulibandika kule Twitter nikakufukuza
Kwani mleta mada unamjua mkuuu
 
Akili za kimasikini za wazazz Akili za kimasikini za wazazi wa Kitanzania
 
Pole sana...mimi nimekataa utumwa wa nyumbani nikiwa na miaka 20 ingawa Mama yangu hana isipokuwa mzee alikuwa na nongwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…