Naona wazazi wangu wamenichoka, ni muda sasa nami nianze kujitegemea

Naona wazazi wangu wamenichoka, ni muda sasa nami nianze kujitegemea

Hapo uamuzi wa busara ni kutafuta chumba cha nafuu ukalianzishe kigetogeto uanze kujichanganya na harakati za mtaa. Uzingatie masomo usije haribu maana uhuru huwa anakuja na uzembe.

Pambana sana.
 
Haya kapange ili wapangaji wenzako wakakufurahie uvivu wako uliokukimbiza Kwa wazazi wako. Na siku ukirudi tena Kwa wazazi tunakupeleka Polisi.

Nakumbuka hili ni jaribio lako la pili maana la kwanza ulibandika kule Twitter nikakufukuza
Hatujuani mkuu hunijui sikujui so usinitishie maisha
 
Hapo uamuzi wa busara ni kutafuta chumba cha nafuu ukalianzishe kigetogeto uanze kujichanganya na harakati za mtaa. Uzingatie masomo usije haribu maana uhuru huwa anakuja na uzembe.

Pambana sana.
Hamna shida ushauri wako nishau note kikubwa dua namuomba mola aniongoze
 
Mtoto Kwa wazazi hakui... Tena Kwa huo umri wako Bado unaonekana mtoto angalau ungekuwa na 25 wangekuchukulia mtu mzima.

So vitu ambavyo mzazi wako anaona ni kawaida kabisa kukwambia, wewe unachukulia manyanyaso Kwa kuwa Kwa umri huo wewe unajiona tayari ni mtu mzima na yawezekana pia baadhi ya kazi unaona ni za kike hupaswi kufanya.

Chagua njia utayochagua ila hakikisha ukihama hapo usiwaongezee majukumu, maana wazazi wengi wanatarajia ikifika umri Fulani basi majukumu Kwa watoto wao hasa wa kiume yanapungua.

Sio ukapange huko uanze kuomba pesa za chakula na mahitaji mengine home, unawaongezea Budget zinazoepukika.
Nadhani kijana anakua kiumri amekuwa sasa wazazi hawaendani na umri wake na kumtambua kuwa amekuwa na yeye anataka heshima yake.[emoji23]
 
Hapana mkuu unajua kuna maneno mzazi akiyaongea unajua kabisa hapa mzazi anakunyanyasa hivi kweli mimi na umri wangu huu niachae mavi chooni hebu mkuu think twice, sikuwahi kuambiwa hivi hapo nyuma. Na suala la kuanza kupanga chumba tayari nimeshaweka mipango yangu fresh nina akiba yangu ya boom kama 200k nahisi itanitosha kabisa kuanzia maisha
Kumbe una boom kabisa. Aaaah we basi hapo ushatoboa.
 
Usiombee uzaliwe kwenye familia ambazo historia ya wazazi wako nao walinyanyaswa na wazazi wao (bibi na babu) huwa wana revenges
Ha ha ha ha ha [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] huwa wanakuwa na ghubu sana aisee wanaamini kuteseka ndio maisha na kumsapoti mtoto ni kumlemaza.
 
Acha tu hapa naishi na wazazi wangu tena wakunizaa ila naona manyanyaso yamekuwa mengi hapa nyumbani ngoja nichomoke mwisho wa mwezi huu
Wakisema waendelee kukupenda hutakua utaendelea bora wa kukazie upate akili za kujitegemea
 
Pole sana...mimi nimekataa utumwa wa nyumbani nikiwa na miaka 20 ingawa Mama yangu hana isipokuwa mzee alikuwa na nongwa sana
Hongera mkuu! Ndio wazazi wetu sasa utafanye muhimu kukubaliana na hali halisi, ila kuepuka shari za wazazi ni kuanza kujitegemea tu hakuna namna
 
Hapana mkuu unajua kuna maneno mzazi akiyaongea unajua kabisa hapa mzazi anakunyanyasa hivi kweli mimi na umri wangu huu niachae mavi chooni hebu mkuu think twice, sikuwahi kuambiwa hivi hapo nyuma. Na suala la kuanza kupanga chumba tayari nimeshaweka mipango yangu fresh nina akiba yangu ya boom kama 200k nahisi itanitosha kabisa kuanzia maisha
Kwa Nini unahisi mama yako kaanza kukuchukia na kukunyanyasa sasa Kabla ya hapo nyuma?

Je unahisi mama yako anakuonea WIVU unavyosoma chuo au?
 
Mgongano wa kifikra,WAZAZI wanakuona wewe bado mdogo,hujakua na WEWE unajiona umekua. Hata hivyo sikushauri utoke hapo kwenu,umri wako bado mdogo na pia HUNA SABABU KUBWA ya kuhama home. Hao ni wazazi wako,ishi nao kitaalamu.
 
Nadhani kijana anakua kiumri amekuwa sasa wazazi hawaendani na umri wake na kumtambua kuwa amekuwa na yeye anataka heshima yake.[emoji23]
Yeah heshima muhimu mkuu atakama ni mzazi kuna muda utahitaji heshima kutoka kwake ila kwakua ni mzazi basi unaamua tu kukausha
 
Wakisema waendelee kukupenda hutakua utaendelea bora wa kukazie upate akili za kujitegemea
Lakini si wangeniambia tu niondoke sio kuniambia nimeanza kuacha mavi chooni hayo sio maneno ya kuongea mtoto
 
Boom lipo mkuu nasubiria awamu hii ya pili mwezi huu nijumlishe na akiba I think itanitosha kabisa kuanza kujitegemea
Hapo lazima utoboe. Geto la 50K unalipa kuanzia miezi 4 au 6 kabisa. Unanunua godoro lako la tano kwa sita inches 6 linatosha unalitandika chini, pazia nunua zile za bei nafuu kabisa najua chumba kitakuwa na dirisha moja.

Then tafuta mama ntilie aliyekaribu na wewe kaweke bili ya chakula cha mchana na usiku kwa mwezi m'moja haitakuwa pesa nyingi inaweza kuwa hata 60,000. Halafu unaweza nunua hata mtungi wa gesi au jagi la umeme unakuwa unachemshia chai asubuhi kama unapenda kunywa chai asubuhi.

Life litaenda utazoea then utaendelea kujiimarisha as life inasonga mbele.
 
Kwa Nini unahisi mama yako kaanza kukuchukia na kukunyanyasa sasa Kabla ya hapo nyuma?

Je unahisi mama yako anakuonea WIVU unavyosoma chuo au?
Hamna maza sikuhizi kabadika mpaka mimi namshangaa sijui anataka nini kwangu kama anataka nijitegemee kwanini asinifukuze nijue moja sio kunifokea tena kwa sauti kubwa.
 
Back
Top Bottom