Naona wazazi wangu wamenichoka, ni muda sasa nami nianze kujitegemea

Kuhusu pesa kulipia kodi na mambo mengi we niachie mimi nitajuwa namna ya kuyashughulikia ila kikubwa mwisho wa mwezi huu niwe nimeshasepa home
 
At 21 unahama unaenda wapi, nina bro ana 26 na yupo bado home

Fanya hivi wewe jali mishe zako, msalimie tu then pita kule usiwaongeleshe ongeleshe

Usitoke home mpaka pale utakopojiweza
Mimi nimeshajitahidi sana kujali mishemishe zangu nakuishi na wazazi wangu ila tabia ya bimkubwa kunifokea kwa sauti kubwa kwakweli nimeshamvumilia vyakutosha sasa ni muda wangu wa kuwa huru na kelele za bimkubwa. Kuhusu umri wangu 21, najua utashangaa kwanini naondoka home ila ndio hivo mkuu kelele za bimkubwa ndio zinanifanya niondoke nyumbani
 
Mwaya mdogo wangu,
Nenda kapambane huko duniani, wengine tulianza kujitegemea hata huo umri wako ni mkubwa,

Ila aga nyumbani kwa amani, maana hujui siku utakayorudisha mpira kwa kipa, wewe ni wa kiume hivyo usiuogope mtaa, jitafutie kakitu kako kadogo ka kuingiza shilingi mbili tatu unakuwa unaenda home mara chache kuwasalimia, unawapelekea japo mafuta na mchele,

Mama atakuheshimu tu, asikudanganye mtu, wamama wetu wengi wanawaheshimu zaidi wale watoto wanaowa support..!!
 
Jiweke kama mtu anayestahili kuheshimiwa, mwenye Akili,
Fanya wanaokuzunguka wakuogope, yaani MTU akitaka kukutuma kazi anajifikiria mara tatutatu!

Wengine tulizaliwa hivyo,
Ndio naanza sasa kujitafutia heshima hasa kwa wazazi wangu naona nikiendelea kukaa hapa nyumbani zarau zitakuwa nyingi na nataka niwaonyeshe kwamba naweza kuishi bila wao ili heshima iwepo
 
Polesana
 
Umejaribu kuongea na mzaziwako wa kiume umsikie anasemaje huenda Kuna changamoto wazazi wanapitia hivo wanadhindwwa kuzuia hasira zao Kwa watu wengine kujitegemea na kusoma naona haviend pamoja waulize hata ambao walifnya hivo wengi waliishi Kwa shida sana
 
heshimu wazazi
ni hayo tu. acha kiburi, mzazi hawezi kumnyanyasa mwanae
tena ukome kabisa kwa maneno uliyotumia
Mkuu tatizo wewe hayajakukuta, hao wazazi unaowatetea sametimes tabia zao huwezi kuzivumilia. Ni wazazi najua ila sio kwamba wanahaki ya kuwa sahihi muda wote kuna wazazi wanakosea hasa jinsi ya kuongea na mtoto huwezi kumfokea mtoto tena kwa sauti kubwa kwangu mimi hili hapana kama heshima wazazi nawapa ila wao mbona mimi hawanipi heshima yangu
 
Huko kufoka kaanza lini au wewe humjui maza ako??
Maana huyo sio mke kusema eti mmekutana ukubwani, umekua unamuona, au hujaishi nae muda mrefu??
 
Yaani Dogo angejua mtaani Sio poa,angetulia.,labda Kwa vile wanasemaga wenzetu ni wanaume
 
Kabisa mkuu nami nataka nifanye hivo hivo nijitafutia hata kibiashara kidogo au vibarua ili niweze kukidhi mahitaji yangu then kingine nitakachokipata nipeleke home ili nipate heshima yangu
 
Nimecheka sana unaposema eti umemvumilia sana. πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…

Mpaka umri huo, nani kamvumilia mwenzie sana?. Narudia kukwambia mdogo wangu, nyumbani hutakiwi kuondoka kwa hasira. Na siku utakayoamua kuondoka, make sure umejipanga, wahenga waliposema "Ukitaka kuruka, Agana na nyonga" walikuwa na maana yao kubwa sana.

At 21, bado sana mdogo wangu. Tena kibongo bongo ndio kabisaaa. Tumia hizo hasira ulizo nazo kujipanga namna ya kuondoka hapo home. Kama Unaona huwezi kuendelea kukaa hapo mpaka utakapo graduate, basi atleast jiwekee deadline, then anza mipango ili kumeet hiyo deadline.

Unga kilo 2200, nyumba za kupanga hata huwe na taa moja tu ndani malipo ni 10000/=. Usije ukasoma story za watu waliosurvive kitaa zikakupa mori, mwaka mmoja una siku 365, na siku moja ina masaa 24. Haya masaa 24 ni mengi sana, hasa ukiyapitisha bila kupata proper meals.

Humu JF Ushawahi kusoma story ya yule jamaa aliyeondoka kwao kwa jeuri ya boom? Matokeo yake mambo yalikuwa tight ikafikia hatua giza likiingia anapanda juu ya mparachichi anakula Yale majani, then anaenda kushushia na maji bombani?

Fikiria upya mkuu. Then jipange
 
Pole Sana kak haya maisha nimewai ishi unagombezwa bila sababu yoyote ile

Kuna chumba kipo pale kibo nilikuwa nakaaga wakt nasoma hapo chuo

Hvyo ukifika kibo uliziaa bar ya daga daga kisha nitexr pm nikupe maelekezo

Ujingwa sna kunyanyaswa bila sababu za msingi sijapenda hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…