Napata mshahara ila unaisha ndani ya wiki mbili au tatu, naishia kukopa

Usagara nayo ni Marekani ..tunaiitaga USA... LABDA anaishi usagara ya kwanza au Tanga.
Huyu Ashura wa mpanda namjua vizuri na juzi nimepita kwao bibi yake anaumwa siku ya tatu sasa mdogo wake Rajabu ndio kabaki na jukumu la malezi.

Just imagine,juzi kapita na mzigo wa kuni hapa anasema anenda kumchemshia bibi yake maji na dada yake Ashura kaenda Daslamu.Leo hii Ashura anatueleza habari za maisha ya Kimarikani sijui mlimani city bure kabisa
 
Sijui kama Moderator watakuacha kwa kukiuka sheria za JF

Name calling.
 
Tatizo lako ni kama langu... Huna nidhamu ya pesa. Usipokuwa na nidhamu ya pesa hata upewe Bilioni moja bado itaisha punde ndani ya muda mfupi bila kufanya nayo kitu cha maana.. Suluhu ya hili ni kujifunza kuwa na nidhamu ya pesa.
 
Ukiona mshahara wako unatoboa wiki 3 ujue upo kwenye right track.
Wenzio huwa wanakaa nao wiki baada ya hapo anabaki na hela ya nauli na soda sio bia tena.
 
Mikopo yako bado stahimilivu πŸ˜‚ unakopesheka ,keep moving
 
Mambo Maiii...
Kwanza hongera kwa kusoma Marikani natumai elimu yako ni nzuri na una akili. Karibu Tanzania na mtaani huku kuna shule nyingine.

Pili unapoandika mada epuka kuchanganya mada mbili au kuweka vionjo vitakavyoondoa muktadha au maana ya uzi mkuu. Hapo kuweka Makonda mara PM mara Samia mara JPM utaacha uzi wako kujadiliwa kwa undani na utaingia siasa.

Tatu, turudi kwenye mada kuu.
Kuwa na kipato kikubwa hakuwezi kufanya uwe na saving kubwa.
Saving inaendana na nidhamu ya matumizi ya fedha. Usipokua na nidhamu hata upate milioni 300 kwa mwezi fahamu hela hiyo itaisha tu na utakopa tena.

Nini cha kufanya.
1. Kaa chini uangalie hela zako huwa zinaenda wapi? Matumizi yako makubwa ni nini?
2. Je matumizi yote ni muhimu kufanya?
3. Je umepanga? Kodi ya nyumba inaendana na kipato chako? Au bado unaishi home?
4. Starehe yako ni nini?
5. Angalia marafiki wanaokuzunguka, je wana msaada kwako?
6. Fungua account nyingine hakikisha unaweka kila mwezi milioni pembeni ndio uanze matumizi....
7. N.k n.k

By the way you are just 23 huo ndio umri wa kufanya mistakes zote kabla jua halijazama. So kula life.

Mwisho wewe ni ME au KE?
 
Una uhakika umekomaa kiakili kama unavotudanganya?
 
Chai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…