#COVID19 Napata shida kuelewa kwanini Rais Samia kamuajiri Tonny Blair kuhusu COVID-19 na kurejesha jina zuri Tanzania

Ni hela nyingi sana. Nchi yetu haijawahi kukodi huduma za aina hiyo. Nchi zenye viongozi madikteta wa kweli au tawala corrupt kama congo brazaville, drc, togo gabon, equatorial guenea ndio hua wanahitaji huduma hizo. Mara nyingi ni ili habari mbaya za kweli zigeuzwe nzuri. Sisi tumekua tunajitangaza wenyewe kwa uzuri wa nchi yetu. Kama mama ameanza kutumia huduma kama hizo sio sahihi. Kwanza hua wanatoza ghali kupindukia maana itahitajika kuhonga watu na wala hakuna uhakika wa matokeo mazuri maana wateja ni kweli wana sifa mbaya. Sisi hatujafika huko.
 
Kagame used Blairโ€ฆ tukashangilia

Today hatutaki

Anyways
 

Umekoroga ulipomwingiza mwana Chato kwenye mada yako. Huyo ana maswali yetu mengi ambayo tunahitaji majibu hata yeye akiwa mfu:



Tony Blair umemdadavua vyema.

Tunamhitaji nani wa kutusemea nini wapi kwa pesa? Mbona hata kwa bure hatumhitaji hata Steve Nyerere, wala Wema kutufanyia hilo eti kuwa ni kazi?

Kweli cha mjinga huliwa na mwerevu.
 
Leta ushahid mkuu..usilete porojo..

Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app
 
Manake zile trilioni 1.3 ndo zimeanza kazi hivyo!! Yaani Mia ndo imeenda kwa mtu moja tu?
 

Thread closed
 
Tony Blair atafanya lobbying kwa niaba ya serikali ya CCM siyo kwa niaba ya wananchi. Viongozi wa serikali ndiyo wanahofu kwamba watawekewa pingamizi, akaunti zao za benki huko Uswisi na kwingine walikoficha hela zitafungwa, wao na familia zao watanyimwa visa za kwenda Ulaya na Marekani. Mwananchi wa kawaida ni vigumu kuona faida ya kazi atakayofanya Tony Blair lakini viongozi wa serikali wataiona.
 
Kama uwezo wako wa kufikiri ni mdogo na exposure ni ndogo UTAPATA SHIDA sana kuelewa mambo haya.

Wewe ubongo wako peleka chit chat na siyo huku JUKWAA la siasa
 
Kila utawala na aina yake ya utawala! Kama ambavyo mtu wako aliachana na yote ya watangulizi wake, akawaita mafisadi, hawajafanya kitu miaka yote 30 ya utawala wao na wengine akawaambia wanawashwawashwa, basi mwacheni Samia naye aongoze kwa maono yake! Hata akiwaleta Taliban as long as ni kwa maslahi ya nchi then ni sawa tu
 
Hako kazee ni kajanja kajanja, katakuwa kanatumika na tawala za mabeberu kushawishi maslahi yao kwa nchi za ulimwengu wa tatu na pia kanatafuta maslahi binafsi. Kwa sababu ngozi nyeusi tuna kawaida ya kuwaona ngozi nyeupe kama ni watu ambao ni genuine basi huwa tunaishia kuwademkia kama mazwazwa, watu vichwa kama Nyerere ilikuwa ngumu sana wazungu kuwaingiza kingi kwa namna yoyote ile maana falsafa zimelala pale.....
 
Wewe unafikiri hao IMF na WB kumwaga mahela hapa ni bibi yako ndio kawashawishi?
Watu kama kina tonny wametoka ushawishi mkubwa Sana huko in short ni kama wadhani vile kwenye hiyo mikopo huko...
 
Watanzania kila mtu na maisha yake, wanaofuatilia issues za a siasa mtandaoni tumebaki kuwa keyboard warriors wenyewe kwa wenyewe, kikubwa tunaparulana sisi wenyewe wanaokula kwa mlija wanabaki kucheka hata cheche hawajui zinadondokea wapi!.
 
Weka ushahidi wa unachokisema ili tuweze kuchangia kwa usahihi
 
Watanzania wengi ama hawasomi au kumbukumbu yao ndogo, huyu mtu aliyetuuzia Rada kwa Bei kubwa kisa kulinda ajira za raia wake 200 Leo tunamwona ni shujaa wakati kwao wamemwumbua juzi juzi kwa tuhuma za ufisadi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ