Msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Mh Nape Mosses Nnauye kasema ukweli usiopingika halafu huyu mama anakuja kumfuta kazi kinafiki wakati ukweli hata yeye mwenyewe Bi Tozo anaujua.
Na kibaya zaidi, Bi Tozo anamuondoa Nape na Makamba halafu anawajaza wazanzibar kwenye teuzi. Kama urais umemshinda bora aachie ngazi arudi kwao Zanzibar badala ya kuwaondoa watanganyika kwenye nafasi nyeti na kuwajaza wazanzibar.
Uliona wapi, kwa mfano, mzanzibar anateuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi au Waziri wa Mambo ya nje? Mambo ndani ya Tanganyika mzanzibar anayajulia wapi? Au mzanzibar anaiwakilishaje Tanganyika nje ya nchi? Mambo ya Tanganyika anayajua? Jamani acheni masikhara!
Haya mambo ya kinafiki anayofanya Rais Samia imefika wakati sasa Gen Z wa Tanganyika wachukue hatua kudai nchi yao kutoka mkoloni huyu wa kizanzibar. Mwanzoni alikuwa anateua waislamu wenzake kushika nyadhifa nyeti serikalini. Sasa ameona hilo halitoshi, ameanza kutujazia wazanzibar wenzake kwenye teuzi na nafasi nyeti za kuiwakilisha Tanganyika wakati Tanganyika hawaifahamu vizuri. Huu ujinga utakoma lini?
MaCCM na serikali yao ni majitu manafiki sana. Nape kusema ukweli inakuwa nongwa wakati hata mama Samia mwenyewe kuna siku alisema mambo hayo hayo aliyoyasema Nape. Alichokosea Nape ni kutamka hadharani. Hawakutaka aseme hadharani kuanika mbinu wanayotumia kushinda uchaguzi.
Mimi namuona Nape kama shujaa kwa sababu amethubutu kusema ukweli ambao sio kila mwanaCCM anayependa ujulikane. Nape daima atabakia kuwa shujaa kwa namna alivyowawezesha watanganyika kuufahamu uweli ambao CCM wamekuwa wakiutumia kushinda miaka nenda miaka rudi.
Rais Samia anajifanya haelewei magoli yamkono wakati mwaka 2020 alishirikiana na Magufuli hadharani kuiba uchaguzi uliomuweka madarakani hadi leo hii anakula bata ikulu kwa sababu ya uchaguzi wa wizi. Unafiq ni kitu kibaya sana.
Hongera Nape kwa kusema ukweli. Ushujaa wako umekugharimu kama ambavyo mashujaa wengi wa Afrika akina Lumumba, Steve Biko, Tom Mboya, Robert Ouko, Nelson Mandela na wengine wengi walivyopata gaharama kwa kuetetea maslahi ya waafrika. Nawe umeng'olewa madarakani kwa kutetea demokrasia ya nchi yetu.
Mungu mbarike Nape, Mungu ibariki Tanganyika.