Nape alichoongea ni ukweli mchungu; atabaki kuwa shujaa daima

makamba alipewa wizara yenye tanesco akaua, imechukuwa muda na kazi ya ziada mpaka waziri mpya Doto ilibidi afute likizo ili kurudisha umeme na kuiweka tanesco sawa (tena) sasa angalau umeme unawaka, kama hilo halitoshi kahamishiwa mambo ya nje kaharibu pia, ulitaka raisi ambebe kwa mbeleko ipi ? baada ya hizo chances zote kupewa tena wizara nyeti na kuharibu bado unamlaumu raisi kweli ? ulitaka raisi afanye nini? huyo jamaa ni incompetent aliondolewa na Magufuli pia sawa mlisema Magufuli hivi na vile sasa kaondolewa pia na Samia mama yenu tena baada ya kupewa kila kitu ili a shine lkn bado ameshindwa, sasa ulitakeje?
 
Nashauri uteuzi ufuate utalaam, weledi, ufahamu wa eneo la uteuzi na uwe mwananchi ambaye amekubali kutumikia nchi yake pasipo shaka na uteuzi usifuate DINI, eneo, ukabila, urafiki, uchawa, jinsia n.k.
 
Vipi tena, Mwizi anayesaidia Mwizi mwenzie kwako ni Shujaa? Hapana wote ni Wezi. Na wote siyo mashujaa.
Yes Mama lazima ajitenganishe na wezi, alivyofanya ni vizuri, na akitaka apendwe aondoe wezi wote hasa wale Chawas
 
Nape na Makamba utoto bado wanao mwingi vichwani mwao wanasahau kuwa kwa sasa sio vijana tena.

Kupigania CCM na kulala maporini miaka ya nyuma sio kigezo cha wewe kuongea pumba halafu mheshimiwa SSH aendelee tu kukuachia uwepo kwenye serikali yake.
 
Hili ni andiko la nape mwenyewe,sauti ya intonation onasikika katika hili andiko, naona umetumika kumtetea na kupima upepo!
 
Nape amekunya juu ya meza ndani ya nepi. Walimzoea Mama vibaya, walijifanya untouchables
 
Shujaa wa nini? ..Bora unge define ushujaa wa nnape ni nini maana tunaona ujinga tu kwake.
 
Kwenye siasa hakuna uadui wala urafiki wa kudumu. Makonda kuna video ana dance anashuka kwenye landrover new model alifurahia mahasimu wake kutumbuliwa.

Kilichofanyika ni mbinu ya kutafuta kuhalalisha uchaguzi wa 2025. January ni mtu ana ji brand sana ili aje awe raisi na nahisi ndio aliosababisha mkataba wa DP world kuonekana kwa umma. Ni mtu wa kung'ata na kupuliza kama babake JK.
 
Mzee wa bao la mkono.
Nape ali asisi bao la mkono, aka asisi kuzima bunge live sasa aka asisi kuwa back bencher. Mpanda ngazi hushuka kwa speed karibu Nape
 
Nape ni Shujaaa........sio uongo ndugu zangu.

Sema Mama amesanuliwa kwenye mipango yake ya 2025. Sijui atatokaje
 
Huwezi kuwa hujalewa. Kwamba Nape ni shujaa!!!?? Naungana nawe kwenye kila ulichoandika isipokuwa hapo kwa Nape kuwa shujaa.

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Kwa mujibu wa Nape, ule ulikuwa utani na siyo ukweli.
Kuna ukweli na KWELI inayowaweka watu huru kweli kweli.
KWELI hubaki kuwa KWELI, isemwe isisemwe, Ila kuna ukweli unaosemwa hadharani na usiosemwa.
 
Mzee wa bao la mkono.
Nape ali asisi bao la mkono, aka asisi kuzima bunge live sasa aka asisi kuwa back bencher. Mpanda ngazi hushuka kwa speed karibu Nape
Huu ni uonevu wa Bi Tozo kwa Nape kama alivyofanya mwendazake. Nape amekuwa mtu wa kuonewa tu bila sababu. Hii haikubaliki.
 
Wote hao kilicho waponza ni kumshabikia mzee Magoma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…