Nape Amlilia Roma Mkatoliki, ‘Ooooooh No!’

Nape Amlilia Roma Mkatoliki, ‘Ooooooh No!’

Ni mapema sana kufahamu nani yuko juu ya upoteaji wa wanamuziki.
Isije ikawa ni njama ya kundi fulani kutafuta
msaada wa kupaza sauti kupitia sanaa au kundi lingine kutumia mwanya huo kufutilia mbali kile kinachoitwa muziki wa uhanarakati.
Lakini pia wasanii/msanii mwenyewe anaweza kujiteka/kujificha ili tu aurejeshe umaarufu wake
uliopotea ili atakapotoa wimbo apate atension/kiki.
Ni vyema tukavuta subra na kuchunga mdimi zetu
kwani lolote lawezekana.
Ben Saanane mlisema hivi na wengine kufikia kudai amejiteka mwenyewe!! Mwezi wa 5 sasa hakuna taarifa zozote!!
 
Watanzania wengi hawana akili kama yako, wengi wanaangalia upande mmoja na ndio wanaitwaga nyumbu!!


mtu yeyote anaweza kufanya uhalifu na akataka ukitokea muwaze aliyefanya ni mwingine
Yapo mengi ya kuangalia. Mara nyingi polisi na sare zao wanapokwenda kukama watu hujazana kushuhudia tukio na huwa hawwafukuzwi na wakamatwaji huhoji uhalali wa kukamatwa kwao. Hapa nashangaa watu wasio na sare wanawateka na watekwaji awahoji wapi wanapelekwa na wamekamatwa kwa kosa gani.
Kujua kama kuna watu walikuja kuwachukuwa watu sita akiwamo Roma ni wazi kuna waliona tukio hilo. Basi watuambie waliwaamini vipi kuwa wale ni askari au watu salama? Kama walitumia nguvu kubwa, kwanini wasijulishe vvombo vya ualama wakati huo huo? Nina mambo mengi nayashakia huenda kuna njama za kutaka kujipa uhalali wa kufanya vurugu kwa visingizio vya utekaji.
 
Kumbe unajua ni kazi yao? sasa si uwaache wampate?? au kuna timelines/deadlines?

ujinga ni pale unapolaumu askari, na wao ndio suspects?? na umekaa tu mwaka mzima Ben kapotea mnakaa tu na kunyoosha yule anahusika

mkiambiwa wengi wenu si riziki mnaona mnatukanwa

wewe na kuandika kwenye keyboard huna uwezo wa kuandamana peke yako!! achilia mbali kuwakaumbusha akina mbowe na msigwa na Lissu!!

hata wewe ukipotea leo usitegemee Lissu, na mbowe watafanya lolote lile

mnaongea sana
Mkuu mbona povu linakutoka hivyo matundu yote? Au mnashea Bwana na Bashite nini?
 
Yeye ni mbunge, akiishia kuandika kwenye mitandao , kusikitika na kulia lia Tu atakuwa hajafanya kitu.
Ashirikiane na wenzake hatimaye Bunge kwa haraka lijadili hilli suala la watu kutoweka na kupotea kama ndege ya Malaysia... ( walau hii vipande vya ndege vilionekana) then wake na maazimio yatakayafanya ukweli kujilikana.Vyombo vya usalama hii ndio kazi tunayowalipa kuifanya... Zinazoitwa kamati za ulinzi na usalama za mikoa wilaya hiki tatizo mnalichukulia pouwa... Mkija shutka limeshakuwa sugu.
Nape wewe ni mbunge, Bashe ni mbunge. Jiongezeni zaidi ya kuandika kwenye mitandao. You can do it
 
Analilia nini badala ya kuwaasa wasanii namna ya kulinda maudhui ya kazi zao?
 
sasa mkuu, si unawajua kuwa hao ndio suspects

then unafanya nini?? unasema tu yanaisha huku umejifungia na mke wako na watoto wako , au unafanya nini?

maana kwa akili za kawaida, ningetamani hao unaoita suspects ndio wafanye kazi, tena mkuu bila aibu unamwita bashite na Bwanaake?? seriously?? unajua mvute madawa lakini msifikie to this extent

haya ukiwa na kende zako mbili, mwaka sasa unakatika hatumuoni wala kumsikia Ben saa nane, na Roma atapotea hivi hivi na wewe kama umepaka lipstic kwenye midomo yako unasema suspect na yule na yule

get up! stand up!! lets do something acha ujinga

Hukumu yao ni 2020, na kama wameshaweza teka toka jana uwezi lia sasa. Hii vita haitaki hasira ni timing na hawawezi fanya kazi hao watu. Vita hii itachukua muda sababu wao ndio wenye silaha.
Madawa kuvuta usione hatare hata ganja ni dawa.
 
Tunakoelekea sasa hata polisi wakija kutukamata inabidi kuambatana na jamaa wengi mno tusijepotea
 


Ikiwa leo ni siku ya pili tangu ilipotolewa taarifa kuwa msanii Roma Mkatoliki alitekwa na watu wasiojulikana akiwa pamoja na Moni Centrozone, mtayarishaji wa muziki wa Tongwe Records, Bin Laden katika studio za Tongwe Records, Waziri wa zamani wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amemlilia msanii huyo.

Nape emetoa kilio chake kupitia ukurasa wake wa Twitter, akitumia maneno matatu pekee yanayosomeka kwa hisia za ndani kuwa ni mtu anayemlilia mpendwa wake.

“Roma! Oooooh No!” ametweet Nape.


Mbunge huyo wa Mtama ameongeza nguvu kwa kilio cha wadau wa muziki pamoja na wasanii waliotumia mitandao ya kijamii kushinikiza ifahamike alipo msanii huyo na wenzake.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa jana na uongozi wa Tongwe Records, watekaji walifika katika studio hizo na kuwahoji waliokuwepo, kisha kuondoka nao wote pamoja na baadhi ya vifaa vinavyotumika kurekodia muziki, kwenda kusikojulikana.

Mke wa Roma, Nancy ameeleza kuwa alifika katika vituo kadhaa vya polisi jijini Dar es Salaam kuulizia taarifa za mumewe, lakini alielezwa kuwa taarifa za Roma hazikuwepo.

Akizungumza kwa uchungu kwenye vyombo mbalimbali vya habari, Nancy aliwaomba Watanzania kwa ujumla pamoja na vyombo vya usalama kusaidia kufahamu alipo mumewe.

“Serikali, waandishi wa habari, Watanzania, yeyote aliyeona, aliyesikia, anayeweza kutusaidia Roma yuko wapi naombeni msaada wenu,” alisema.

Leo mchana, wasanii wamekutana katika studio za Tongwe Records kwa lengo la kuzungumzia suala hilo zito ambalo limevunja mioyo ya wadau wa muziki, familia na ndugu wa Roma na wenzake.
Hivi awamu ya 5 inadhani itaua watanzania wangapi ?
 
Huyo nape mnafiki, kavuliwa uwaziri bado tu kimbele mbele
 
Hali ya tanzania kwa sasa ni ya kuripoti UN security Council, dunia ijue nini kinaendelea Tanzania. Hawajui ndiyo hata jana balozi wa EU alionekana happy with Tanzania which is contrary to EU human rights policy!
Hili lifanyike haraka sana

Tume huru idaiwe mapema Tanzania
 
Daaaah...!!! Mbona haya mambo kipind cha nyuma hayakuwepo kwann kipind hiki ndo yamekuwa yakitokea na hakuna anayechukua hatua stahiki si vyombo vya dola wala si viongozi wanaohusika na masuala haya...!!! Tunaelekea wapi watanzania...?????

Umemsahau Dr Ulimboka,Umemsahau Dr Mvungi?Umemsahau Kubenea? umemsahau Kibanda??Ni vizuri kuwa na kumbukumbu
 
Watanzania wengi hawana akili kama yako, wengi wanaangalia upande mmoja na ndio wanaitwaga nyumbu!!


mtu yeyote anaweza kufanya uhalifu na akataka ukitokea muwaze aliyefanya ni mwingine
In this case, nani amepose kama nani?
 
Haya ni mambo ya kawaida sana kwenye madola ya kiimla !
 
Back
Top Bottom