Nape ataka Akaunti ya Deni la Taifa ichunguzwe na iwekwe bayana Fedha hizo zilikopwa na kupelekwa wapi?

Nape ataka Akaunti ya Deni la Taifa ichunguzwe na iwekwe bayana Fedha hizo zilikopwa na kupelekwa wapi?

Alafu ikichunguzwa!!!??
hajui kwamba Baraza la Mawaziri ndio serekali yenyewe?
 
Ni muendelezo wa kusaga kunguni awamu ya 5

24C4157D-C0DC-4467-8A3A-D9EFBF66DF5F.jpeg
 
Nape anataka kumfanya nini makamu wa rais Dr Mpango ambaye alikuwa waziri wa fedha?

Usilete uchonganishi; Nape ametoa hoja ya msingi na uchunguzi huo lazima uanzie awamu zote za nyuma. Nakumbuka enzi za Kikwete na Waziri wake wa fedha Mustapha Mkullo walifloat bond in foreign currency na fedha zile hazikujulikana zilitumika kwa miradi gani!! Zitto alijaribu kuulizia akazibwa mdomo!!! Uchunguzi ukifanyika professionally tutajua mambo mengi yanayokwamisha maendeleo yetu.
 
Inatafutwa Huruma Tu Ukweli Hakuna Wa Kuthubutu Hilo
Anaongea Tu Kutufanya Sisi Wajinga
Haoni Serikali Itaanguuka Mchana Kweupe Kuku Wanaona
Mzilankende Kwenye Msiba Ile Report Ya Hazina Ukaguzi Ina Majibu Yote Lakini Ilizimwa Tu
 
Mbunge wa MTAMA Nape Nnauye amesema deni la Taifa limekuwa kwa kasi sana ndani ya miaka 5 iliyopita na kusema japo Serikali inadai ni himilivu hali sio nzuri

Nape ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya 5 ilikopa mikopo mingi huku asilimia 40 ya mikopo hiyo ikiwa ni ya kibiashara hivyo kuwa na riba kubwa

Ameongeza kwa kutaka uchunguzi ufanyike jjuu ya mikopo hiyo na ilinganishwe na thamani ya miradi ambayo mikopo hiyo ilifanya

Ameipongeza Serikali ya awamu ya 5 kwa kuweka wazi mkopo wa 1.3 trilioni iliyokopa kitu ambacho hakikuwepo kipindi kilichopita na kutaka uwazi huu uigwe

Nawaza kwa sauti tu:
[emoji830]︎Ujenzi wa Meli mpya na ukarabati wa meli za zamani kwenye Maziwa makubwa nchini kurahisisha usafiri wa mizigo (mazao ya wakulima) na abiria ukaboreshwa;
[emoji830]︎ ujenzi SGR itakayorahisisha usafiri na kupunguza uharibifu wa barabara;
[emoji830]︎ ujenzi wa Bwawa la Nyerere kutoa umeme wa kutosha na kuondoa adha ya kukatikatika;
[emoji830]︎ ujenzi wa madaraja makubwa kurahisisha usafiri mijini na maeneo mengine yenye shida za usafiri wa majini;
[emoji830]︎ uboreshaji wa huduma za jamii (elimu, afya na maji) hasa vijijini na kupunguza gharama kwa wanavijiji
[emoji830]︎ nk
 
Mbunge wa MTAMA Nape Nnauye amesema deni la Taifa limekuwa kwa kasi sana ndani ya miaka 5 iliyopita na kusema japo Serikali inadai ni himilivu hali sio nzuri

Nape ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya 5 ilikopa mikopo mingi huku asilimia 40 ya mikopo hiyo ikiwa ni ya kibiashara hivyo kuwa na riba kubwa

Ameongeza kwa kutaka uchunguzi ufanyike jjuu ya mikopo hiyo na ilinganishwe na thamani ya miradi ambayo mikopo hiyo ilifanya

Ameipongeza Serikali ya awamu ya 5 kwa kuweka wazi mkopo wa 1.3 trilioni iliyokopa kitu ambacho hakikuwepo kipindi kilichopita na kutaka uwazi huu uigwe

Cccm janga la taifa tunataka katiba mpya
 
Mbunge wa Mtama Nape Nnauye ametaka ufanyike uchunguzi wa akaunti ya deni la taifa na iwekwe bayana kila senti ilikwenda wapi na ilifanya nini?

Source: ITV habari
Kwani huyu Nape ile Taarifa ya BOT iliyoagizwa iandaliwe na Mama hajaiona? Kama ameiona haiamini?
 
Usilete uchonganishi; Nape ametoa hoja ya msingi na uchunguzi huo lazima uanzie awamu zote za nyuma. Nakumbuka enzi za Kikwete na Waziri wake wa fedha Mustapha Mkullo walifloat bond in foreign currency na fedha zile hazikujulikana zilitumika kwa miradi gani!! Zitto alijaribu kuulizia akazibwa mdomo!!! Uchunguzi ukifanyika professionally tutajua mambo mengi yanayokwamisha maendeleo yetu.
Siyo uchonganishi ,ukichunguza madeni ya nyuma lazima umuhoji Dr Mpango
 
Mwendazake alisikika akisema tunatekeleza miradi kwa fedha zetu za ndani kisha akaondoka zake.
 
Mimi nadhani bora ungetaka uthibitisho wa hoja zake badala na wewe kuvurumisha maneno ya kwenye kanga.
Tuhuma alizotoa ni nzito zinahitaji kuwekwa wazi zaidi kwa vielelezo.
Huyo alipaswa kua jela KWA Sasa,ni JPM tu alimstahi. In short hana Morality ya kuongea chochote na ndo Mana alichagua kukaa kimya.

Thread za maovu yake zimejaaa humu if,unaweza kusearch
 
Nape anataka kumfanya nini makamu wa rais Dr Mpango ambaye alikuwa waziri wa fedha?
Unatuuliza sisi ili iweje nyie mchwa na nzige? Professor Assad alishaweka wazi wizi wenu. Kajadili huko kivyenu.
 
wana nia ya kuzidi kumchafua JPM aonekane hafai kabisa na ajabu viongozi wanaompenda makufuli wamekaa kimya
 
Back
Top Bottom