Nape ataka Akaunti ya Deni la Taifa ichunguzwe na iwekwe bayana Fedha hizo zilikopwa na kupelekwa wapi?

Jiwe alikuwa kidume cha nguvu! Huyu alikunjia mkia matakoni! wakati ule! asingekohoa Ona mishipa ya shingo ilivyokakamaa sasa
Bora alijikalia kimya kuliko angesema Jiwe na genge lake wakamnywa damu, bora nini?
 
Wera wera wera nafuu umeongea NAPE kuliko wale wakusfu pambio!!!
Ujue kuna madudu nyuma ya pazia!!!
Kwa nini hakuongea mapema wakati mikopo ikiwa inakopwa? Leo anakuja kulalamika alitakiwa aachie ngazi kuonesha kutokukubaliana.
 
Nape anataka kumfanya nini makamu wa rais Dr Mpango ambaye alikuwa waziri wa fedha?
Kwa nini wasijadili kwenye vikao vya chama cha mapinduzi huko? Ili wakipata majibu wayajadili huko huko, kwa sababu akiliweka wazi hivi bado hata ikijulikana itafichwa tu kama ambavyo walitaka bunge lijadili gizani, hawakutaka bunge liwe LIVE, ilihali wanasema wao ni "wawakilishi wetu"

Hao ndio CCM, wameona bunge limepoa halifuatiliwi na mtu, wameamua kipiga kelele tuwasikie.
 
Kuchukua mikopo kwa siri ni Dalili tosha kuwa ni wizi
Unachukua mkopo kwa siri, unatumia kwa siri, halafu mbele ya wananchi unawaambia nchi hii ni tajiri sana, mabeberu hatuwataki.

Jamaa alikuwa bonge la msanii.

Pamoja na mapungufu ya Nape, lakini kwa hili namuelewa.

Uchunguzi ufanyike ili kubaini matumizi ya mikopo hiyo.
 
Nape anapayuka tu kutafuta attention ya bunge lililopoteza mwelekeo
 
Anarudia kile alichoongea John Heche kwenye medani ya Siasa
 
Mbunge wa MTAMA Nape Nnauye amesema deni la Taifa limekuwa kwa kasi sana ndani ya miaka 5 iliyopita na kusema japo Serikali inadai ni himilivu hali sio nzuri...
Kweli kabisa, maana tulikuwa tunaambiwa maendeleo maendeleo yanayofanyika yanatokana na pesa zetu za Kodi na wakaanza kutangaza mapato kila mwezi kwa mbwembwe sana, sasa Deni linatoka wapi maana hatukuwahi kuambiwa Kuna mkopo hata siku moja zaidi ya kupewa maneno ya kojuha tu.

Tuweke Mambo bayana ili tumalize utata, na kama kweli hakukuwa na deni basi tuwaulize hao wanaotudai waseme walimkopesha Nani na ziliingia nchini kwa utaratibu gani?

Yawezekana wengine tusioelewa tukapata ukweli wa Mambo tukaelewa, otherwise itakuwa ni porojo za watu wale.
 
Mbunge wa MTAMA Nape Nnauye amesema deni la Taifa limekuwa kwa kasi sana ndani ya miaka 5 iliyopita na kusema japo Serikali inadai ni himilivu hali sio nzuri...
Wanafiki wakubwa hawa. Kesho utamuona kageuka kama vile sio yeye kabisa
 
Hawa ni viongozi wenye maarifa madogo sana! Ngoja hizo shule zenu zitakapokuwa substandard na fedha kupotea ndio mtajua umuhimu wa kufuata utaratibu, sheria na kanuni na pia professionalism.
 
Upande huu tunaambiwa Magufuli aliharibu uhusiano na mataifa/taasisi wakopeshaji, upande mwingine tunaambiwa Magufuli alikopa sana; so which is which? Alikuwa anakopa wapi sasa kama alikosana na wakopeshaji? Alikopa kwa wafanyabiashara wa ndani?
 
Nape asisahau waliokuwa viongozi waandamizi wa hiyo serikali anayoilaumu ndio hawa waliopo kwenye serikali mpya anayojipendekeza kwao ili apate teuzi...
Nape ni mnafiq mkubwa, hana msimamo, anachofanya ni ubinafsi wa kupambania tumbo lake tu.
 
Nape ni mnafiq mkubwa,hana msimamo, anachofanya ni ubinafsi wa kupambania tumbo lake tu.
Hajawahi kuwa mkweli na hii ndiyo sifa yake kuu.

Nashangaa watu walimuonea huruma kipindi kile anataka kupigwa pyuuuu pyuuuu
 
Tanzania haijawahi ku issue bonds kwenye masoko ya mikopo ya kimataifa kama vile EuroBond.

It was through a consortium of many International banks!! I am sure of this, Mustapha Mkullo was finance Minister.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…