Nimezisikia na kuzisoma hoja za Nape ila, ukweli kuwa Nape kwa kujua au kutokujua amemuonea mzee mkapa(apumzike salama).
Nape akiwa na confidence ya Hali ya juu amesema mkapa kwa miaka 10 alikopa dola Bilioni 9.
Hii si kweli kabisa, na sijajua kwa nini mh.Nape aliamua kusema hivi.
Mkapa aliingia madarakani 1995 Deni lilikuwa ni dola bilion 7.37. na hadi anaondoka madarakani kwa mwaka wa fedha alioishia nao Deni lilikuwa ni dola Bilioni 8.4
Hivyo kwa miaka 10 mkapa alikopa dola bilion 1 tu ambayo ni sawa na trillion 2.3 ya sasa na sio bilion 9 ambayo ni sawa na trillion 20 Kama alivyosema mh.Nape.
Kutokana na mpango wa kufutiwa madeni Deni lilifutwa na kufikia dola bilion 4 mwaka 2006 mwanzoni, ila likatoka hapo na kufikia dola bilion 15 Hadi kikwete anaondoka.
Hivyo kikwete alikopa dola bilion 11 na sio Bilioni 7 Kama alivyosema Nape
Mh.Nape kwa hesabu ulizopiga unaenda kumhukumu mama Samia bila kujua, maana kwa kipindi chake Cha miezi 6 tu ameshakopa zaidi ya Trillion 4 ( 2.7 za world Bank na 1.3 za IMF).
Mh.Nape umesifia mikopo hii kwa mama, lakini jua kwa kipindi Cha miezi 6 mkopo kwa mama samia umezidi mkopo wa mkapa kwa kipindi chake cha miaka 10.
Lakini mimi sitamhukumu jiwe mwendazake, mama Samia na atayekuja. Kwa sababu;
Kipindi cha mkapa na mwanzoni mwa kikwete mfumuko wa bei ulikua mdogo sana na pesa yetu ilikuwa na thamani kwenye dola 1.
Mfano: kipindi Cha mkapa ili kujenga darasa 1 ilihitaji si zaidi ya mil 5. Hivyo akienda kukopa atakopa pesa kidogo na deni kwa sasa litaonekana dogo kipindi chake.
Sasa hivi kujenga darasa moja si chini ya mil 20, bati kipindi cha mkapa liliuzwa sh.5,000 Ila leo bati ni sh.25,000 hivyo mama Samia akienda kukopa ni lazima atakopa kingi.
Mfano mwingine rahisi tu, Kuna kipindi Cha mkapa bajeti ya nchi ilikuwa Trillion 4 tu.
Lakini sasa hivi hizi trillion 4 ukiweka kwenye barabara tu zote zimeisha kutokana na thamani ya pesa kwa sasa.
Hivyo kwa hesabu rahisi tu kwa kipindi Cha miaka 5 inayokuja mama samia atakopa hadi trillion 30(huu ni ukweli). Na atayekuja baada ya mama Samia nae atakopa zaidi ya hizo 30.
Nini kifanyike ili deni lisikue;
- kupandisha thamani ya shilingi dhidi ya dola. mfano dola moja iwe sh.1200. na hapo Deni letu litakuwa limeshuka kwa nusu. Badala ya trillion 64 litakuwa trillion 32.
- kupunguza mfumuko wa bei, mfano bati liwe sh.8000, cement sh.7000, nondo sh.9000.
Hayo yote yanawezekana Ila kwa serikali ambayo itakuwa na vision na watu wenye akili kubwa sana
View attachment 2003889View attachment 2003890