Nape atofautiana na Jaji Warioba Bunge la Katiba

Nape ndio tank thinker wa C.c.m?inasikitisha sana!rasimu ya katiba ni mawazo ya wananchi,bunge halina uhalali wa kubadili maoni na matakwa ya wananchi,bali ni kuboresha
 
wamekula kodi zetu bure walichotoa hakina maana!!

ila wenyewe wanadai kamati ya rasimu kazi yake ilikuwa ni kutoa tu mwanga wa kianzio, eti bunge hilo ndo litatunga katiba
ndiyo swali la kujiuliza, kama Tume ya Waryoba ndiyo kila kitu , kwa nini Bunge la Katiba? tuache mbwembwe, Bunge la Katiba inaweza kukubaliana/ kubadili na hata kukataa kabisa kilichomo kwenye rasimu zote mbili. Kile ndicho chombo cha kutunga sheria na hakiwezi kupitisha kila kitu ambacho wananchi wengine walitoa maoni yao waliandaliwa kwa maslahi ya baadhi ya watu wachache. BIG NO.
 
Safi sana Mkuu, na warejee miswada ya serikali ambayo imekuwa ikiwasilishwa bungeni , siyo yote inayopita kama ilivyowasilishwa na wakati mwingine hukataliwa kabisa na kurudishwa. Nawashangaa sana wanaoabudu rasimu wakati ile ni sawa na mswada tu.

Ni kweli kabisa, lakini kutulazimisha serikali2 na sisi wananchi tuna uhuru wa kukataa serikali2, sawa na wale wanaokataa 3, sawa na wale wanaokataa 1. Kura ya maoni itaamua.! Hatutaki kuhubiri kulinda Muungano kwa viini macho na hadaa, tunataka dhati kutoka moyoni. Dhati halali kuliko zote ni Serikali1, 3 zenyewe nazo ni mashaka, 2 ndo kelele nyingi sana kama wote tunavyofahamu.
 
Nape ndio tank thinker wa C.c.m?inasikitisha sana!rasimu ya katiba ni mawazo ya wananchi,bunge halina uhalali wa kubadili maoni na matakwa ya wananchi,bali ni kuboresha

Hahaaa, sasa wanakwenda kufanya nini DODOMA? safari hii mtalia sana , MBOWE hana nafasi tena ya kugoma bungeni akiondoka tu bado kuna takribani wabune zaidi ya 500 watafanya vizuri sana hiyo kazi.
 
Umeipenda kwa kutoju kasema nini. Na kama Kamati ya WARYOBA ndiyo kila kitu, kwa nini Bunge la Katiba kimeundwa?

Binafsi tangu mwanzo sikuona umuhimu wa hilo Bunge, ni ufujaji wa kodi zetu bure. Ilitakiwa maoni ya kamati ya warioba yaletwe kwa wananchi moja kwa moja kwa ajili ya kura ya maoni, period!
 
Habri yote iko bungeni tupende tusipende, hizi zingine kelele tu.
 
una mawazo kama yangu mku hapo kwa red
 
Ni akili ya matope sana kuamini kuwa mabadiliko ya Kipengele kimoja cha Katiba tena kwa personal interests za watu eti ndiyo mabadiliko. Pole sana Dada yangu.

Kwangu mimi ukiangalia maneno yako yanakutafsiri tabia uliyonayo,so kubishana na wewe au kuendelea kukujibu nitapoteza muda wangu.Ni bora kuitwa nina akili ya matope lakini mwisho wa siku nina kubali mabadiliko na pia nina uzalendo na utaifa,kwangu mie utaifa kwanza ubabaishaji baadaye,tunachohitaji ni KATIBA ya watanzania na si KATIBA ya CCM.
 
Binafsi tangu mwanzo sikuona umuhimu wa hilo Bunge, ni ufujaji wa kodi zetu bure. Ilitakiwa maoni ya kamati ya warioba yaletwe kwa wananchi moja kwa moja kwa ajili ya kura ya maoni, period!

ndiyo ujue sasa kwamba Bunge la Katiba ndiyo kila kitu.
 
Hahaaa, sasa wanakwenda kufanya nini DODOMA? safari hii mtalia sana , MBOWE hana nafasi tena ya kugoma bungeni akiondoka tu bado kuna takribani wabune zaidi ya 500 watafanya vizuri sana hiyo kazi.

Me sizungumzii unachowaza wewe,nazungumzia maoni waliyotoa Watanzania juu ya katiba waitakayo,na sheria iliyowekwa juu kuongoza rasimu ya katiba!hizo porojo unazoleta mimi sipo huko
 
Binafsi tangu mwanzo sikuona umuhimu wa hilo Bunge, ni ufujaji wa kodi zetu bure. Ilitakiwa maoni ya kamati ya warioba yaletwe kwa wananchi moja kwa moja kwa ajili ya kura ya maoni, period!
 
Kwa jinsi watanzania tulio wengi tulivyo (shule ndogo, hatufuatilii kinachoendelea katika siasa, hatujitokezi kupiga kura, etc), hata hilo la serikali mbili litapita tena kwa kura nyingi tu.
 
naona kama unajitukana mwenyewe kwa vile sasa unaona hauna hoja. Hivi kwa akili yako unaweza kutafsiri neno mabadiliko kuwa ni kuwa na serikali tatu? na je zile nchi ambazo hazijaundwa na muungano wa nchi mbili au zaidi haziwezi kufanya mabadiliko? Halafu nakushangaa sana unaposema huna sababu ya kubishana na mimi wakati kila ninapojaribu kukuelewesha unaendelea kutoa mapovu badala ya kuishia kabisa na usijibizane na mimi.
 
Kwa jinsi watanzania tulio wengi tulivyo (shule ndogo, hatufuatilii kinachoendelea katika siasa, hatujitokezi kupiga kura, etc), hata hilo la serikali mbili litapita tena kwa kura nyingi tu.

Na kwa mtanzania yeyote anayeutakia mema muungano, lazima aikubali serikali mbili. Wale wenye malengo binafsi na ambao hawautaki muungano lazima watajitumbukiza kwenye janga la serikali tatu.
 
Me sizungumzii unachowaza wewe,nazungumzia maoni waliyotoa Watanzania juu ya katiba waitakayo,na sheria iliyowekwa juu kuongoza rasimu ya katiba!hizo porojo unazoleta mimi sipo huko

Watanzania wapi mkuu, wale waliokuwa wnanunuliwa kwenda kusema hivyo kwa nguvu bila kujua wanaowatuma wana malengo gani? Subiri vichwa vimekwenda DODOMA na vitakuja majibu mazuri tu.
 
Uelewa wa Nape na akili yake kwa ujumla hana uwezo hata kidogo wa kubishana na Mhe. Jaji Warioba. Anachoweza Nape ni kuongea pumba majukwaani, kupiga ngoma ama gitaa na kukoleza maharage kwa wali pekee. Hayo mambo ya kitaalam na yanayohitaji weledi na akili iliyotulia awaachie wahusika wenyewe.
 
Bunge litaingiliwa tu ktk maamuzi yake kwa kura ya maoni.
 
kuna tofauti kubwa kati ya uandaaji wa miswada ya serikali na hili la katiba mpya! kumbuka kuwa bunge huwakilisha maoni ya wananchi na hii huwa pale wananchi wenyewe hawawezi kupata fursa ya kutoa maoni yao,tofauti na sasa ambapo tayari wananchi wenyewe wametoa maoni yao kupitia tume ya mabadiliko!!!! Hivi wabunge watawezaje kutuwakilisha ili hali sisi wenyewe tumetoa maoni yetu?????
Bunge la katiba ni kwa ajili ya kurekebisha dosari ndogondogo tu na si kubadili maudhui ya rasimu ambayo kimsingi ndiyo maoni ya watz!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…