Nape: Bando ni huduma ya ziada, ukitaka lisiishe tumia salio la kawaida. Mbunge ataka liwe kisheria

Waziri wa habari, Nape Nnauye amewataka wabunge kuacha kutuhumu wizi kwenye mitandao ya simu kwa ujumla.

Nape amesema bando ni huduma ya ziada ambayo ina masharti ya muda, mtu akitaka lisiishe uko utaratibu wa kutumia 'Main Tarrif' akitolea mfano tiketi za kusafiria za mwezi ambayo hauwezi ukadai hata ukitumia mara moja.

Nape amesema hofu yake ni kutumia Bunge kushutumu uwekezaji mkubwa kuna wizi inakwenda kuharibu huduma ya mawasiliano.

Spika Tulia akifafanua swali la mbunge, alimtaka Nape aeleze kama ni sheria au utaratibu na kama Bunge linao uwezo wa kubadilisha au haliwezekani.

Nape amesema ni utaratibu wa kibiashara ndio maana bei yake ni ndogo kulinganisha na kutumia salio na sio suala la sheria.

====

Akitoa hoja, mbunge Franscis Mtinga ametaka bando ziwe kisheria na Nape kama ambavyo alileta muswada wa kulinda habari binafsi, alete muswada wa kulinda haki kwani mashirika ya simu yanaibia wananchi sana. Mbunge ametaka kutopangiwa jinsi ya kutumia bando alilonunua.

Ubawa wa Nape... ni kufikiria kila kitu kisiasa zaidi ya kiutalamu
Ivi nape huyu si ndiyo alishinikiza Buge ... lisiwe live..,
Once akitolewa kwenye nafasi yake ndio anangundua matatizo kwenye ishu usika
Hawa wakina nape, na underperformance Minister hawapaswi kuwa kwenye nafasi kubwa kama hiyo aliyonayo.....
 
Mfano Airtel kama una salio la kawaida haikubali Data lazima ujiunge bando, hapo unasemaje?
... hiyo sasa ni kazi ya regulator (TCRA) kutoa majibu na solution. Iko hivi, Serikali inamiliki kampuni ya mobile (TTCL) ni opportunity kwao kuweka bando bila expiry date ili wananchi tukimbilie huko then automatically na wengine hawatakuwa na options zaidi ya kuiga ili wabaki sokoni.

Hiyo ndio maana ya competion sio ushindani kutungiwa sheria za kijinga anazo propose huyo mbunge.
 
Nape yuko sahihi katika hili japo ni kweli lina maumivu kwa watumiaji wa bando. Lakini ni maumivu yasiyo na uhalisia. Bando ni mfumo wa promotion katika biashara, sasa vipi promotion uiwekee sheria au umlazimishe mtoa promotion au offer iwe endelevu au ya kudumu? Tuwe objective wakati mwingine.

watu sjui wanataka izi kampuni zipate hasara zifunge ofisi ndo wafurahi
 
... hiyo sasa ni kazi ya regulator (TCRA) kutoa majibu na solution. Iko hivi, Serikali inamiliki kampuni ya mobile (TTCL) ni opportunity kwao kuweka bando bila expiry date ili wananchi tukimbilie huko then automatically na wengine hawatakuwa na options zaidi ya kuiga ili wabaki sokoni.

Hiyo ndio maana ya competion sio ushindani kutungiwa sheria za kijinga anazo propose huyo mbunge.

huezi kuhudumia nchi nzima mwenyewe lakini pia serikali ikifanya ivo basi uchapa kazi utapungua kwa sababu wako wenyewe hautakua na alternative ingine
 
Waziri wa habari, Nape Nnauye amewataka wabunge kuacha kutuhumu wizi kwenye mitandao ya simu kwa ujumla.

Nape amesema bando ni huduma ya ziada ambayo ina masharti ya muda, mtu akitaka lisiishe uko utaratibu wa kutumia 'Main Tarrif' akitolea mfano tiketi za kusafiria za mwezi ambayo hauwezi ukadai hata ukitumia mara moja.

Nape amesema hofu yake ni kutumia Bunge kushutumu uwekezaji mkubwa kuna wizi inakwenda kuharibu huduma ya mawasiliano.

Spika Tulia akifafanua swali la mbunge, alimtaka Nape aeleze kama ni sheria au utaratibu na kama Bunge linao uwezo wa kubadilisha au haliwezekani.

Nape amesema ni utaratibu wa kibiashara ndio maana bei yake ni ndogo kulinganisha na kutumia salio na sio suala la sheria.

====

Akitoa hoja, mbunge Franscis Mtinga ametaka bando ziwe kisheria na Nape kama ambavyo alileta muswada wa kulinda habari binafsi, alete muswada wa kulinda haki kwani mashirika ya simu yanaibia wananchi sana. Mbunge ametaka kutopangiwa jinsi ya kutumia bando alilonunua.

Wewe Nape ndio maana mzee JPM alikutembeza juani....
Muda utafika tutaheshimiana tu...
 
Ina maana kati ya salio la kawaida yaani vocha na kifurushi kipi kipo kisheria na kipi ni promotion.?
Hebu nielewesheni
 
Screenshot_20221108-231408.png
 
Back
Top Bottom