Hiyo ni kauli ya katibu mwenezi wa Ccm Nape aliitoa alipokuwa akiwahutubia wananchi wa sengerema na kunukuliwa na Gazeti la Mwananchi la Juni 23/2015
Hizi kauli za nape ni kauli za kibabe na zakichonganishi,Inawezekanaje kama unajiamini na unaamini wananchi wanakikubali chama chako uingie kwenye uchaguzi utarajie ushindi wa dhuluma.
Ccm kwenye uchaguzi huu wa 2015 ni kuwa nao makini,La sivyo wataliingiza taifa kwenye machafuko yasiokuwa ya lazima maana washaonyesha kutokubali kuachia madaraka hata wakishindwa kwenye sanduku la kura.
Kwa kauli ya Nape ni kuwa ccm wapo tayari kushinda uchaguzi mkuu kwa rafu bila kuheshimu maamuzi ya wapiga kura hata ukawa hatuko tayari kulinda ufedhuli huo.
Wakishinda kwa goli la mkono,Ukawa tutakata rufaa kwa wananchi.Kwasababu tunaamini nguvu ya uma na haki sawa kwa wote.