Nape: Kampuni za simu haziibi vifurushi vya intaneti vya wateja

Daaaaaaah
 
Nape pamoja na watanzania walio wengi hawawezi kuwa na ubongo wa kuweza kuyajua hayo, wao husubiri tu zile sms za "umetumia 75 ya bando lako"

Yeye anafikiri tunaposema tunaibiwa anafikiri hatupati hizo sms anazo subiri! Hawa makampuni wanatakiwa wawe wanaangaliwa kujua kweli kama wanachotoa kinaendana na walichosema.....

Sisi tutujuaje kuwa ni GB 5 na sio tatu? Kama Nape anategemea asubiri sms ndio kujua ukweli basi ni mtupu sana kichwani yani haya makampuni waibe kirahisi hivyo? Hawa watu wana akili sana awawezi kuiba kwa njia rahisi ni lazima wakubandike Gb 5 hewa kumbe GB 2 sasa swali kwa TCRA na Nape Nnauye wanawezaje kutambua vifurushi hewa?

Kama watu wanakwenda kwenye vituo vya mafuta wanawekewa hewa tupu halafu mtambo unasoma umeweka lita 10 kumbe 3 ni hewa ...sasa hawa wamitandao watashindwa vipi kutupa vifurushi hewa?
 
Wizi ni pale unaponunua bando kisha unapangiwa siku za kutumia kwa kawaida unaponunua kitu hutakiwi upangiwe muda wa kutumia bando la siku la wiki la mwezi huu ni wizi waache bando mpaka liishe
 
Hii nchi only vitukuu vyetu labda baada ya kutucheka ancestors wao watajaribu kusahihisha wakati kizazi chote cha walafi na wanamtandao kimeisha!
 
Mitandao ya simu imekaa kiwizi wizi sana kwahiyo kuitetea na kutuona sisi wananchi ndo washamba nikutukosea heshima.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Watanzania wengi hawajui matumizi sahihi ya bando. Kuna watu wanaruhusu apps kuji-update na ku-run at the background hivyo kupelekea bando kutumika.
How do you shut down those self updating apps and background running apps.
 
Wizi mkubwa uko hapa,unaweka kifurushi,speed ya inakuwa kubwa kama nusu saa,baada ya hapo inashuka kwa kiwango cha kobe,inaendelea kusumbua hivyo mpaka kifurushi kinaisha,na jinsi inavyotumia muda mrefu kutafuta mtandao bila mafanikio unakuja tu kushtukia Mb zimeisha,hivyo kukulazimisha ununue tena kifurushi...
 
Mkuu huko kutokujuwa kwa watz kumeanza juzi? Simu janja zimekuja juzi nchi hii ni kwanini hayo malalamiko hayakuwepo before? Kiungwana unapaswa kuwataka radhi watz.
Simu janja zimekuwepo muda, lkn matumizi ya mb yamepanda hv karibuni kwa watanzania walio wengi.

Siku za nyuma watu walikuwa wanaingia Facebook tu na wakawa wanatambiashiana kupost picha huko
 
Labda atakuwa ndiye Nape mwenyewe
 
Ni heri angenyamaza tu kwanza hana hadhi ya kuwa Waziri ni mpigaji mbobezi
 
Wanaochambua ni wataalamu wa IT, Nape si mtaalamu wa IT ni mtaalam wa majukwaa ya siasa, nitamuelewa kama atasema anakwenda kufanya uchambuzi yeye binafsi lakini siyo kuwatumia watu wengine ambao hatujui wanainterest gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…