Nape: Muda mnaotumia kulalamika kuhusu bei za bando mngefanya shughuli nyingine

Nape: Muda mnaotumia kulalamika kuhusu bei za bando mngefanya shughuli nyingine

Waziri yupo sahihi
Watu kama nyinyi ndiyo aina ya viongozi tulionao ambao wanafanya Tanzania bado inahangaika na maji, afya na elimu.
Tangu 1961 hakuna jambo la maendeleo serikali ya CCM iliyofanikiwa 100%. Umeme wa mgao, maji ya mgao, ukienda vijijini huko ndiyo balaa, afya hakuna kitu, elimu ndiyo hakuna kitu watoto bado wanakaa chini.
Serikali ya CCM iliyofanikisha 100% ni kuiba kura, kukandamiza wapinzani, kula rushwa, kuwajibu wananchi wanavyojisikia bila kujua hicho kitu kina umuhimu gani.
Wewe utakuwa ni wale wazee TTCL wa miaka 50 ambao hawajui nini maana ya internet. Internet imefungua ajira kwa vijana na pia sehemu ya kupata elimu.
 
Kazi yake ni Ushauri kwa wananchi au kusimamia Wizara ya Habari na Mawasiliano ?

Anyway binafsi navyojua Bundle kupanda sio sababu ya mitandao bali Serikali kuingilia Mitandao na watu wangemwambia Nape sio Serikali iingilie bali iache kuingilia....

Kile kipindi cha mwendazake pia yeye si alikuwa analia Lia kwanini asingetafuta kazi nyingine??muone na uso wake.........kama show ya raum
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema kuna watu wanamkosoa kuhusu gharama za bando mtandaoni naye anawajibu kuwa muda huo wangeutumia kufanya kazi nyingine wasingelalama kuhusu bando.

Kauli hii ya waziri, imeenda kinyume na sera ya TEHAMA 2016 inayotaka kukuza fursa za mtandaoni kwa kuwa na gharama nafuu za data na mtandao unaopatikana daima.

Waziri ametoa kauli hii katika Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari 2020 lililofanyika JNICC, Desemba 17, 2022
Nape ni mfano mzuri wa mtu ambaye kabla ya uomgozi alikuwa mtiifu lakini baada ya kupata nafasi anawadharau wasio viongozi
 
Halafu mtu anapojiunga bando kama hela haitoshi Kwanini kampuni za mitandao zisiseme kuwa salio lako limebaki kiasi fulani?

Kwanini waishie kusema salio lako halitoshi hapo hapo ?
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema kuna watu wanamkosoa kuhusu gharama za bando mtandaoni naye anawajibu kuwa muda huo wangeutumia kufanya kazi nyingine wasingelalama kuhusu bando.

Kauli hii ya waziri, imeenda kinyume na sera ya TEHAMA 2016 inayotaka kukuza fursa za mtandaoni kwa kuwa na gharama nafuu za data na mtandao unaopatikana daima.

Waziri ametoa kauli hii katika Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari 2020 lililofanyika JNICC, Desemba 17, 2022
Jamaa kiburi halafu ignorance

Shughuli za watu zinategemea mawasiliano, ndio maana wadau wana complain kuhusu bando. Sasa wafanyeshughuli gani wakati shughuli zao unazikwamisha.
 
Mungu ambariki sana kwa hii nafasi aliyo nayo aishi milele, asante sana mheshimiwa waziri tumekuelewa mheshimiwa.
 
Back
Top Bottom