Tetesi: Nape na Membe wahusishwa kuhujumu nguvu ya Magufuli ndani ya CCM

Tetesi: Nape na Membe wahusishwa kuhujumu nguvu ya Magufuli ndani ya CCM

Wakifanikiwa kuua upinzani kwa kuhujumu vyama vya upinzani, roho ya upinzani haitawaacha salama. Itaendelea hata kama ni ndani ya chama kimoja. Na hapo huenda ikawa mbaya zaidi kiasi cha kufikia kupinguana kwenye madaraka. Hivi vyama wanavyovihujumu vinawapa fursa na nafasi ya kutolea nyongo, sasa vikifa unafikiri watu watafanyaje kutoa dukuduku zao?
Wapinzani ni watanzania na siyo mamluki. CCM ikiua upinzani ambao upo kikatiba hakitabaki salama. Upinzani utahamia ndani ya ccm. Tusije tukafurahia sana hii biashara inayoenelea hivyo sasa. Ina madhara makubwa mbele ya safari.
 
Wakakodi hata drone walivurumuwe hili jiwe maana ghalika inakuja likiachwa na uzuri likishafyeka upinzani likwenda na kwenye chama chao litafyekelea mbali mahasimu wake kama huo mpango upo wachangishe fedha tuchangie tumfurumushe nduli
 
CCM haipo salama na hawa wafia njaa wanaomiminikia huko wajiandae siku za misukosuko hazipo mbali ni 2020..
 
kama hii habari ni kweli "... basi naomba harakati zao zifanikiwe
 
Wafadhili wa Mheshimiwa Membe wamempatia kitita cha kutosha kufanya mapinduzi ndani ya CCM

Hii ni Mpango Na utitiri wa wakwepa kodi watenge Tshs triolini moja kununua wabunge wa ccm kwa bilioni tano tano na bunge loote kuwa la upinzani kwa wingi kwa kwa hila ya pesa...SANDUKU la kura wanaona hawawezi sasa wanataka kutumia pesa chafu $400M zilizochangwa na Group 20

mapinduzi yenyewe ni kupigania katiba inabadirishwa ili mbunge akihama ahame na ubunge wake, maana inaonekana wabunge wengi wangependa kuhama kutokana na maoni ya chini chini, ila tatizo wanahofu ya kupoteza ubunge wao.

Heri wanaohama kutoka upinzani kwenda CCM hao watapewa nafasi na Magufuli,.au saa nyingine kurudi bungeni kupitia uchaguzi wa mabavu, lakin wanao tamani kuhama CCM kwenda upinzani ndo watakuwa wamepoteza kabisa,

Point ya Membe ni target 2020 kwamba wabunge wengi wa CCM kabla ya 2020 watashinikiza baadhi ya mambo yanayombeba membe kugombea maana watakuwa huru wakizinguliwa wanahama, wakihama na ubunge wao,

Hivi navyoongea mambo yanaratibiwa na Nape nyuma ya Membe, kuhakikisha Magufuli anakwama kwa aina yeyote ile

Nakili kwamba CCM inataka mkombozi wa kuitoa kwenye meno ya Magufuli lakin njia anayotumia Membe inaweza isizae matunda maana intelligence ya Magufuli ni kali mno na ina mzizi mrefu,

Nape hivi karibuni ameonekana akibeza na kutoa maoni juu ya wanaohama na kurudia uchaguzi, ni kweli point anazosimamia nape zina mantiki ila lengo lake siyo kuokoa hela ya uchaguzi ila ni nyingine.

Amerushiana na Makonda maneno ,simtetei Makonda maana hata mimi Nina mashaka na elimu yake na uelewa pia, ila Nape utakwama tumia njia nyingine,

Hatimaye CCM yetu itaurudi
Huoni aibu kuzua hekaya ya kufikirika kweupeee...bila hata ya chembe ya uthibitisho.
 
Point ya Membe ni target 2020 kwamba wabunge wengi wa CCM kabla ya 2020 watashinikiza baadhi ya mambo yanayombeba membe kugombea maana watakuwa huru wakizinguliwa wanahama, wakihama na ubunge wao,

Lisemwalo lipo, kama halipo basi laja.
Tungojeee....
 
Back
Top Bottom