Nape na ombi la CAG kukagua mikopo; kuna watu wamepanic!

Wewe muongo!!!!!!!! Mbweni ni magofu tu. Sema awamu ya nne
 
Naunga mkono hoja. Isiwe Awamu ya tano tu. Ianze awamu ya nne uone watu. watakavyoumbuka
 
Ni kama unamsema Dr.Mpango aliyekuwa pale wizarani. Hiki ndio sababu kubwa ya kina Dotto kuhakishwa wizara tu na Bashiru kupunguziwa ulaji
 
Kuna waliofaidika na JPM kwa kula cha juu kikubwa!
Utawasikia wakienda kwa waganga ili kuzuia uchunguzi🙂🤣🤣
Mbegese yaani hayati vile alivyokata ile budget ya ukaguzi mwaka Juzi, hakuna mkaguzi anafagilia ule uzombi...ni kwamba jamaa watachambuliwa zaidi ya karanga!!!
 
Pia anasahau kuwa Mama naye alikuwepo kwenye system.
 
Usililojua nape sio mtu ni taasisi kwaio io ni meseji imetumwa upande wa pili
 
Mkuu ni Mkwere, prince na Membe wamemtuma abwatuke
 
Huyo CAG Kichere naye kwa nini asubiri maelekezo? Katba imeshatoa maelekezo tayari
Kama uchunguzi ukifanywa na Bunge kwa kuamriwa hivyo, basi utakuwa uchunguzi dedicated kwa hiyo mikopo tu ya Awamu ya Tano, kama alivyoomba Nape!
Kumbuka CAG alifungishwa virago alipohoji Trillioni 1.5 zimeenda wapi!
 
Awamu ya 5 si tulikua tunaongozwa na mzalendo, kiongozi wa malaika,mh. 'mungu' Kama Kabudi alivyomuita?Madudu yanatokea wapi Sasa?
Hivi wewe na akili yako ulimuona JPM anaweza kuficha hela hata Billion moja wewe? Azifiche wapi? Huelewi jinsi walivyokuwa wanamuwinda kumuumbua? Aipeleke benki ipi? Angalikuwa ni JK sema huyo ni mjanja tangu awamu ya pili na Barick yake.
 
Hoja yake ina mashiko? Tuanzie hapo.
Mashiko sana,
Kwa hiyo ukaguzi ufanyike au usifanyike?

Kwanza nakubali kabisa hoja hiyo ina mashiko, na pia ukaguzi huo ufanyike. Lakini je, unadhani kwa mazingira yaliyopo utafanyika? Ni sawa na mbwa anabweka, halafu ukimfuata anakimbia, au mwanasiasa kama Nape kwenda kwenye jukwaa la siasa na kuongea hayo. Inakuwa ni kutaka tu kusikika kuwa yupo, lakini in reality hata yeye anajua hilo halitafanyika, ila anajua atakumbukwa na kuzungumzwa kwa kuongea hivyo na pengine ataitwa mezani.
Kumbuka walio fanya hayo ndio waliopo serikalini kwa sasa tena kwenye nafasi kubwa. Hizo ni siasa tu.
 
Awamu hiyo kuna watu walipiga hela za kufuru
Sijui nilikuwa wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…