Nape Nnauye atishishiwa Bastola na kusukumizwa kwenye gari

Nape Nnauye atishishiwa Bastola na kusukumizwa kwenye gari

Nina shaka na huyu askari alipitia mafunzo kikamilifu? Mazingira yepi yaliyomfanya atoe bastola yawezekana hata mwizi wa kuku atamtolea kifaru
 
Hapa alikuwa anaingia viwanja vya Protea Hotel kwa ajili ya kuingia ukumbini kuanza mkutano, ndipo hawa vijana walipomfuata na kumtaka asishuke kwenye gari badala yake aondoke...ila mwishoni alweza kuendelea na mkutano japo kwa mbinde!
napata mashaka sana na utimamu wa nape, hapa kama alikuwa hajala madawa basi alikuwa kajitwika bapa. Naona busara za kijana wa wake wengi maulid wa kitenge, huyu jamaa anaonekana ni mzoefu wa mizozo.
 
Ni aibu kwa taaluma nzima ya usalama,kwa mwanausalama kumvamia kiongozi bila ya kujitambulisha na kuonyesha kitambulisho na kuanza kumtisha kwa bastola ili atii amri yako.
Nakushauri kamanda Sirro umrudishe uyu kijana akasome vizuri sheria za usalama kuliko kulitia aibu jeshi la polisi.

Haapa alivyotolewa bastola, Msanii Harmorapa naye alikuwepo hapo ila alitimua mbiop baada ya Bastola kuonyeshwa


Waziri anaonyeshwa bastola je mtu baki?
 
It is dangerous to be RIGHT when Magufuli's government is WRONG.
 
Kuna MTU kaambiwa na nape atoe kitambulisho akatoa bastola ..,....sasa sijui angeambiwa atoe vyetii si angetupa Bomu......pwAaaaaa....


Mwafwaaaaaaa
 
Nina shaka na huyu askari alipitia mafunzo kikamilifu? Mazingira yepi yaliyomfanya atoe bastola yawezekana hata mwizi wa kuku atamtolea kifaru
tusimlaumu huyu askari alikosewa adabu, mtu kamfuata kistaarabu tena kaonyeshwa na kitambulisho yeye kaanza kupayuka hovyo.
 
Nyie mods na nyie mmetumwa au? Mnaondoaje threads za watu hovyo? Mnaboa sana wakati mwingine.
 
Nape alitaka kuongea na waandishi wa habari kama nani? Yeye tayari status ya uwaziri ilishabadilika asubuhi na mapema na akawa anatambulika tu kama "aliyekuwa waziri wa habari wa zamani...." Busara ya kawaida tu alipaswa kuwa nayo ya kusubiri zipite siku za kutosha ili watanzania wote mpaka huko vijijini wajue kwamba yeye si waziri wa habari tena, maana kuna watu wengi hata Dar es salaam kama wakina Harmorapa bado walikuwa wanadhani wanaenda kumsikiliza waziri.....
 
Dah! Mimi si mpenzi wa CCM na si shabiki wa Nape ila hicho nilichokiona kwenye hiyo video sijakifurahia.Kwangu haki ni haki tu.
Ni nini hasa kilipelekea yote hayo?
Kuna anayejua humu anieleweshe zaidi?
Ni hofu ya watawala na walioogopa kwa dhana potofu kwamba Nape atatangaza "uamuzi mgumu" au "atafanya maamuzi magumu".
Kama unataka habari zaidi sikiliza hapa.


 
Malipo n hapa hapa duniani goli la mkono limemrudia
Uchungu wa machungu ni pale uchungu huo unapo upata na wewe .haya yanayo mpata nape sasa ni matokeo ya kushiriki dhambi nyingi alipo kuwa na mamlaka ya kufanya hivyo.
 
tusimlaumu huyu askari alikosewa adabu, mtu kamfuata kistaarabu tena kaonyeshwa na kitambulisho yeye kaanza kupayuka hovyo.
Wewe eddy una shida kubwa Nape hakupayuka, ww ni kibaraka wa mtoto na baba yake.
 
Nashauri tufanye kweli kwenye uchaguzi wa mwenye kiti ndani ya chama miezi michache ijayo
 
Wenye pistols zilizoonekana wapo wawili hapo. Sasa sijui wewe unamuongelea yupi?
Huyo mwingine mstaarabu kabisa na bastola yake, huyu Mura angemchapa hata makofi Nape pale, mori ulishapanda
 
Back
Top Bottom