Nape Nnauye: Kiroboto ulishindwa akiwepo godfather, utaweza leo?

Nafuu polepole..Nape Ni wa hovyo Sana..Jikumbusheni nape wa bao la mkono..
Anakaribia kupewa kitengo! Kile kikao cha juzi cha kumsifia brigedia Nauye kilikuwa kikao cha kumpaka rangi kijana wake wa bao la Mkono na kuwaandaa kisaikolojia tu😅

Mzee wa Mapapai yuko njema sana 😆katika michakato ya connection!
 
Nimesikitika, angenyamaza ingekuwa bora zaidi. Mheshimiwa nape anaonekana ni mtu wa bifu sana asiyependa kunyamaza. Matokeo ya anachokifanya hapa ni kuibuka kwa mivutano zaidi......labda ndicho anachokitaka. Ccm ni ya wote, nani kasema ina wenyewe?!! Disgusting!

Simpendi polepole sababu ni mnafiki namba moja, mdini na mbaguzi wa kikanda aliyefadhaika, aliyeshindwa kabla hajaanza, asiye na haya na aliyerUkwa na akili lakini bado naamini anapaswa kukaliwa kimya na wenye akili hapaswi kujibiwa lolote aachwe tu na ngonjera zake. Kumjibu polepole ni kutumia vibaya akili yako na muda wako.....ni dhaifu mno kwa sasa!!
 
Hapa ndipo inapoonekana tofauti kati ya Nape na Polepole, wakati Nape anajiweka mbele kila wakati ili akumbukwe kwenye ufalme wa ulaji aliotolewa.

Polepole anasema anachokiamini bila kujali kama anachosema mbele ya safari kitamgharimu nafasi aliyonayo bungeni, kwasasa Nape ndie kiongozi wa kundi la wachumia tumbo wa nchi hii.
 
Muache ateme nyongo unadhani kushikiwa bastola siku amezuiwa kufanya press alijisikiaje?
 
Mpuuzi sana huyu, aliyewaibia kura wapinzani, genge lake limerudi anajiona yuko juu, salama.

Ushauri Nape, jiajiri, piga zile dili za korosho. Maisha yako yasitegemee sana kodi zetu. We

Wewe Nnauye unamuwalikisha nani, umeme, maji,wakulima, kodi za pembejeo, wamachinga hawana kipato, mfumuko wa bei, tozo vifurushi upo kimya. Huoni kama ni kitu muhimu, wanaotetea maslahi ya watanzania unawaambia CCM, Tanzania ina wenyewe. Wenyewe ni Watanzania milioni 60.

Umelewe kwa ule mkutano wa wiki iliyopita kumuenzi baba yako, usilewe sana mwanangu. Kemet, Roma, Greece zimepita.

Tutapata katiba mpya ndani ya miaka kumi, inayowajibisha viongozi wote, waliopo na waliopita. Kinga tutaziondoa, mashitaka tutaenda nyuma hadi miaka 30.
 
Ni n
Ni Nape yule aliyekuwa anatembea saa nane mchana kweupe akitoka jasho?

Tanzania bado tuna miaka zaidi ya mia ili ibadilike na kuchukua uhalisia wa rasilimali zake hadi hiki kizazi kiishe na kisiwepo.
Kuna watu ndani ya CCM wanaishi kwa ajili ya matumbo yao na sio kwa ajili ya nchi yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…