Nape Nnauye: Kiroboto ulishindwa akiwepo godfather, utaweza leo?

Nape Nnauye: Kiroboto ulishindwa akiwepo godfather, utaweza leo?

Nimesikitika, angenyamaza ingekuwa bora zaidi. Mheshimiwa nape anaonekana ni mtu wa bifu sana asiyependa kunyamaza. Matokeo ya anachokifanya hapa ni kuibuka kwa mivutano zaidi...
Sawa, sema , polepole na Nape wako na bifu personal,, itakuwa polepole alikuwa akiwachongea sana kina Nape kwa jpm,,, ujue polepole amekaa kaa kichawa sana.. [emoji23][emoji23]
 
Mpuuzi sana huyu, aliyewaibia kura wapinzani, genge lake limerudi anajiona yuko juu, salama.

Ushauri Nape, jiajiri, piga zile dili za korosho. Maisha yako yasitegemee sana kodi zetu...
Hahahahahahah nani atakaekubali adhabu zi date back huyo😅! Hamna mjinga wa kukubali hilo katiba inaweza ikaja ila geresha tu
 
Mkuu hii ya kurudi nyuma miaka 30 ndicho nakitafurahia zaidi kuliko yote endapo katiba mpya itapatikana.

Fuentte, tuna watu hawajui, labda wanajua wajibu wao lakini hawataki kutekeleza.

Katiba mpya itakuwa, lazima iwe na kipengele cha kuwaondoa madarakani watu wasio fanya kazi kuanzia mwenyekiti wa Mtaa hadi Rais. Napendekeza tuwe na katiba kama ya Switzerland, kila kitu muhimu kinapigiwa kura, Rais akizingua,akiwa hana uwezo anaondolewa fasta, kwa kutokuwa na imani naye.

Rais akifa Madarakani tuwe na uchaguzi mpya, serikali ya mpito. Yote yatakuwa kwenye katiba mpya. Hiyo ndio real, proper democracy.
 
Hapa ndipo inapoonekana tofauti kati ya Nape na Polepole, wakati Nape anajiweka mbele kila wakati ili akumbukwe kwenye ufalme wa ulaji aliotolewa, Polepole anasema anachokiamini bila kujali kama anachosema mbele ya safari kitamgharimu nafasi aliyonayo serikalini, kwasasa Nape ndie kiongozi wa kundi la wachumia tumbo wa nchi hii.
Tofauti ni kuwa, Nape alitolewa ukatibu mwenezi akawa kimya, Polepole kuna kitu kinamuwasha na hii ni kwasababu polepole ni mhamiaji ccm,, deep down, Polepole ni mpinzani wa CCM, cheo tu ndio kilimfanya vile alivyokuwa na alitumia hicho cheo kukihujumu CCM kimkakati, yeye na yule mtusi aliekuwa katibu mkuu
 
Zamani enzi zetu wakati super star wa Kijiji alikuwa ni yule anayeweza kutembeza kichapo kwa kila mtu na asiwepo wa kumzuia kulikuwa na aina flani hivi ya kuanzisha ugomvi, kanatumwa ka dogo flani kukuchokoza makusudi ili ukikapiga tu hutajua njemba zilizoshiba zinatoka wapi?

Utapigwa hadi uzimie kwa kumpiga dogo "chambo"...Ila wajanja tulikuwa tunaangalia vichaka vilivyo jirani kabla hatujajibu mashambulizi ya "andunje" Nape umewahi Sana....Kuna mapandikizi nyuma ya huyo uliyemuita kiroboto!
 
Hahahahahahah nani atakaekubali adhabu zi date back huyo😅! Hamna mjinga wa kukubali hilo katiba inaweza ikaja ila geresha tu

Yote itagemea akili za Watanzania. Ngoja vyums viendelee kukaza, bodaboda elfu tano kwenda kilomita mbili, chakula chsa siku moja 30K,
 
Tofauti ni kuwa, Nape alitolewa ukatibu mwenezi akawa kimya,, polepole kuna kitu kinamuwasha,, na hii ni kwasababu polepole ni mhamiaji ccm,, deep down, polepole ni mpinzani wa ccm,, cheo tu ndio kilimfanya vile alivyokua, na alitumia hicho cheo kukihujumu ccm kimkakati, yeye na yule mtusi aliekuwa katibu mkuu
Akawa kimya hadi zile audio zake na Kinana na Makamba zikatoka "mawingu studio"
 
Acha waparurane wamepitia cheo kimoja walivurugana acha waendelee...yetu macho
 
Fuentte, tuna watu hawajui, labda wanajua wajibu wao lakini hawataki kutekeleza.

Katiba mpya itakuwa, lazima iwe na kipengele cha kuwaondoa madarakani watu wasio fanya kazi kuanzia mwenyekiti wa Mtaa hadi Rais. Napendekeza tuwe na katiba kama ya Switzerland, kila kitu muhimu kinapigiwa kura, Rais akizingua,akiwa hana uwezo anaondolewa fasta, kwa kutokuwa na imani naye.

Rais akifa Madarakani tuwe na uchaguzi mpya, serikali ya mpito. Yote yatakuwa kwenye katiba mpya. Hiyo ndio real, proper democracy.
Yah hii demokrasia ya kurithishana mikoba kama waganga wa jadi haitufai😅
 
Nape hamkumuekewa,, kumbuka Polepole alikuaga TLP kabla hajapewa ukatibu mwenezi ccm, Bashiru alikua CUF kabla hajapewa ukatibu mkuu, ccm
Kwa kauli hii, unataka kusema Pole Pole na Bashiru si wana ccm?

Na je vipi kuhusu kina Mbowe na lipumba ambao walikua wana CCM na wakaondoka, bado tuendelee kuwaita wana ccm?

Au sijakuelewa pia?

Anaposema Ccm kina wenyewe, ni kina nani hasa?
 
Fuentte, tuna watu hawajui, labda wanajua wajibu wao lakini hawataki kutekeleza.

Katiba mpya itakuwa, lazima iwe na kipengele cha kuwaondoa madarakani watu wasio fanya kazi kuanzia mwenyekiti wa Mtaa hadi Rais. Napendekeza tuwe na katiba kama ya Switzerland, kila kitu muhimu kinapigiwa kura, Rais akizingua,akiwa hana uwezo anaondolewa fasta, kwa kutokuwa na imani naye.

Rais akifa Madarakani tuwe na uchaguzi mpya, serikali ya mpito. Yote yatakuwa kwenye katiba mpya. Hiyo ndio real, proper democracy.
Hawa jamaa mali wanazolimbikiza sasa itabidi tuwarudie hata wajukuu wao kufidia maumivu wanayotusababishia makusudi kabisa. Kwa sasa wanatuona wajinga hadi wanajipa majina ya ina wenyewe ila kuna siku kama sio wao basi damu zao zitalipia haya makosa yao
 
Kumbe nayeye alikua makini akisubiri press ya Polepole...😇
Hii inaonyesha ni kiasigani wana CCM walikua wakisuburi kwa ham kusikia Polepole akitangaza kung'atuka ehhhh...😜
Ebu nitoshe kumkumbusha Nape atunze akiba ya maneno, asije akaponzwa masikio kuzidi kichwa..

Kazi ipo kwani naye kakomaa. Bado yupo yupo sana - wamzowee tu 😁😁.
 
Back
Top Bottom