Hawa ndo wanamuharibia mama na serikali yakeNape Nape Nape.....huu ni utoto..
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hawa ndo wanamuharibia mama na serikali yakeNape Nape Nape.....huu ni utoto..
Yaqn.hili.ndio tatizo.la nape.
Hahahahahahahahahahahahah.......
Hana kolomero kabisa.
Hi hivi unajua Watanzania wengi hawajui maana ya democracy.Yah hii demokrasia ya kurithishana mikoba kama waganga wa jadi haitufai
Kiroboto aka Punda hahahaaaaaaa..Kumbe nayeye alikua makini akisubiri press ya Polepole...[emoji56]
Hii inaonyesha ni kiasigani wana CCM walikua wakisuburi kwa ham kusikia Polepole akitangaza kung'atuka ehhhh...[emoji12]
Ebu nitoshe kumkumbusha Nape atunze akiba ya maneno, asije akaponzwa masikio kuzidi kichwa..
Pole pole atulie tu hawawezi watoto mjini waswahili kwa fitina wako vizuri kama kweli magufuli yalimshinda na ndiye Rais na kila kitu hayupo sembuse yeye, ndio maana Nape kamjibu kuwa yeye ni kiroboto tu atulie.Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza, watu wengi humu JF hawaelewi hata nini kinaendelea kuhusu hii movie.
Ngoja leo hapa JF nifungue code chache.
Sote tunapaswa kujua kuwa kuna vita kubwa sana ya kimaslahi ndani ya CCM kwa sasa baada ya Magufuli kufariki dunia. Vibaraka wote wa JPM wamepangwa kunyofolewa kwenye madaraka ya serikali na chama ili vibaraka wa Hangaya (JK) washike hatamu. Anachokifanya Hangaya ni kutimiza mapatano ya uhuni wa 2015 uliofanywa na JK kupitia genge lake (akiwemo Nape, January, Kinana, Makamba nk) uliohakikisha ufalme haiendi kwa mmasai wala hauendi upinzani kwa kutumia koti la kisukuma (JPM).
Alichokifanya JPM baada ya kuingia madarakani kilikuwa kiko kinyume na mapatano ya kupewa urais wa dezo na genge la Msoga, ule ulikuwa ni uasi dhidi ya JK. Huo ndio ukweli wa kwanza.
Ukweli wa pili ni kuwa, Pole Pole ndio mjumbe rasmi wa kuongea mbele ya umma kuwakilisha Sukuma gang. Pole Pole anatumika kutishia, kutikisa kiberiti na kutuma ujumbe dhidi ya utawala wa Msoga gang. Wale wote waliokuwa ndani ya utawala wa JPM na kwa sasa wako kimya, basi mdomo wao wa kusemea ni Pole Pole. Ukiona ngedere mjini basi ujue kuna mtu anamfuga!
Ukweli wa tatu ni kuwa Pole Pole yuko mbioni kufukuzwa, kusimamishwa au kufungwa mdomo kisiasa (kupewa cheo cha kufungwa mdomo kama ubalozi, RAS nk) na utawala wa sasa, na tayari hilo ameshalijua, press yake ya leo ilikuwa ni "Political strategy" ya kuwatisha watawala waogope kuchukua hatua walizozipanga au wakizichukua iwe more advantage kwake kisiasa, hiyo inaitwa Pre emptying approach. Tetesi za kusema leo Pole Pole alikuwa ajivue uanachama wa CCM mbele ya vyombo vya habari zilianzishwa na team ya Pole Pole, kimakusudi na kimkakati ili kutisha na kupima upepo wa watawala wa sasa. Ni mbinu ya kisiasa.
Ukweli wa nne ni kuwa Nape ndio mwanasiasa aliyepangwa rasmi na Msoga gang kujibizana na Pole Pole kwa sasa. Anachokifanya sasa Nape sio bahati mbaya, ni jambo limepangwa na analitekeleza. Muda sio mrefu Nape naye atakuwa na vipindi vya tv na platform za kuongea mitandaoni. Yaani ngedere atajibiwa na ngedere, maana wote wako mjini wanafugwa!
Mwisho kabisa ni kuwa Nape anarudishwa tena serikalini, muda sio mrefu, na huenda akarudishwa wizara ile ile aliyotolewa au kwenda wizara fulani mpya iliyoanzishwa na Magufuli ikihusika na wizara ile ile aliyokuwepo Nape.
Serikali ya CCM ni failure, katika mambo critical hutolewa majibu mepesi tu na huwa lazima muyakubali tu!Hi hivi unajua Watanzania wengi hawajui maana ya democracy.
Democracy ni utawala wa wengi, tatua matatizo ya wengi, weka mazingira watu wapate riziki kodi, tozo sahihi.
Hakikisha umeme, maji upo siku zote, thibiti mfumuko wa bei. Kiuna wizara inaitwa ya mipango na fedha.
Hivi wanapanga nini, wanawasaidiaje wengi,vijana, maskini, kuwawezesha kusimama.
Pigia mstari "kina wenyewe" it's a matter of time utamuona kwenye Vii eitee...Nafuu polepole..Nape Ni wa hovyo Sana..Jikumbusheni nape wa bao la mkono..
Kwani anayeongoza Nchi kwa sasa ni nani?Samia hataweza kuiingoza hii nchi
Hawa jamaa mali wanazolimbikiza sasa itabidi tuwarudie hata wajukuu wao kufidia maumivu wanayotusababishia makusudi kabisa. Kwa sasa wanatuona wajinga hadi wanajipa majina ya ina wenyewe ila kuna siku kama sio wao basi damu zao zitalipia haya makosa yao
Ila CCM hawajua kinachoendelea mtaani sio? Wafanye tafiti kuna chuki sana inajengeka...watakuja washangae akitokea mwanasiasa ana nguvu...watashangaa sana watu kama kina Nnape. Just someone to ignite
Imefeli sana, hakuna ulazima kukubali chochote.Serikali ya CCM ni failure, katika mambo critical hutolewa majibu mepesi tu na huwa lazima muyakubali tu!
Mjinga katudharau watanzania wote kwa hii kauli yake.Kwamba CCM ina wenyewe?
Mjinga katudharau watanzania wote kwa hii kauli yake.
Hapa ndipo inapoonekana tofauti kati ya Nape na Polepole, wakati Nape anajiweka mbele kila wakati ili akumbukwe kwenye ufalme wa ulaji aliotolewa.
Polepole anasema anachokiamini bila kujali kama anachosema mbele ya safari kitamgharimu nafasi aliyonayo bungeni, kwasasa Nape ndie kiongozi wa kundi la wachumia tumbo wa nchi hii.