Tetesi: Nape Nnauye kufukuzwa uanachama wa CCM

Tetesi: Nape Nnauye kufukuzwa uanachama wa CCM

Status
Not open for further replies.
Tatizo ccm hamna akili, sasa Nape akifukuzwa nani atakuwa looser hapo? Hili ndo kosa ambalo hata upinzani wamekuwa wakilifanya (fukuza fukuza), sasa ccm mkiiga hiyo tabia mtakufa mapema sana na hivi tumemchoka sizonje. Mfukuzeni ikifika 2020 mtalia na kusaga meno
 
jina na imani aliyojijengea nape kwa jamii inayojitambua hata akisimama na magufuli ktk uchaguzi basi magufuli anaondoka bila wasiwasi. hakuna atakayesimamia ukweli akashindwa ila atawekewa vizingiti. ktk hili nape amewashinda bashite na baba yake vibaya mno. NI BORA UWE MASKINI KULIKO KUWA MTUMWA WA BINADAMU. kazi zliyoifanya nape Kwa CCM hakuna yoyote ktk baraza la mawaziri ukijumlisha na rais wao ameifanya.
 
Nape ni mmoja wa mzizi mkuu wa mtawala yule, alihakikisha mtawala anaota wakiwa na makamba+mwigulu. Hivyo awe makini kuukata mzizi huu
Unajua Sophia Simba alikuwa na mizizi kiasi gani CCM?

Mwaka 2010 JK alipiga kampeni yeye na familia yake coz alikuwa kama ametengwa lakini alishinda

Siku zote inapotokea mgogoro wa kikazi kati yako na boss wako ni lazima mmoja wenu aondoke aidha kwa kuhamishwa au kufukuzwa mara nying wafanyakazi ndio huwa wanaumia sana ktk jambo hili kama likitokea so ni ukweli usiofichika Nape na Boss wake hawakuwa na mahusiano mazuri ya kikazi na kiutekelezaji
 
Naona enzi ya zidumu fikra za Mwenyekiti zimerudi rasmi. Si jana zilikotoka fikra za zidumu za mwenyekiti walikuwa Bongo?
 
Ametimiza wajibu wake, ameonyesha uadilifu na uzalendo, ameondoka kwenye nafasi yake kama shujaa.
 
Akifukuzwa kwa kutetea haki Mungu yupo atamtetea kwan nn nape anatenda haki nlikuwa simpend now nape wew ni shujaaaaaaaaa
 
Mkomoaji mkuu anaweza kufanya hilo, roho izidi kusuuzika!
 
aaaa...nimeamini "ZIMWI LIKUJUALO HALIKULI UKAKWISHA"
sipati mkuu vasco da Gama huko msoga bay anasikitikaje.
Pia baba kinana mbona hatukuoni ukijitokeza kuokoa jahazi linalozidi kujaa
maji kiasi cha kuanza kupoteza uzania (EQUILIBRIUM) au wataka yatokee yale ya
meli ya Titanic ndipo uibuke..?? Tafadhari sana naomba ujitokeze kokote kule uliko
mshitue na babu philip Mangula
Hao wazee wa CCM Magufuli hawasikilizi kabsa mshauri wake Mkuu ni Daud bashite pekee, ina maana Bashite akisema afukuzwe hata Waziri mkuu anafukuzwa kwa sasa CDF, IGP , mkuu wa Usalama wote wanamwogopa Makonda hakuna mfano, ebu fikiria mpaka mkuu wa majeshi alienda kwenye kamati ya maadili ilikuwa ni wazo la Makonda ili wamdhibiti asije akapindua Nchi , kwa sasa watanzania wapo ndani ya Utawala wa wasukuma wawili watakomaje !!
 
Visasi hivi ccm inakwenda kufa na watakao ua ccm ni wana ccm wenyewe. Kwanza kwa kumchekea Rais ambae hashauriki. Mbili kwa kuruhusu visasi viendeleee . niliwahi sema hivi viongozi wenye weredi wa utawala wapo wapi?
Mzee Mwinyi
Mzee Kikwete
Mzee mangula
Mzee Warioba
Mzee kinana
Kwanini mnaburuzwa na mnaaibisha chama kwa kunyamazia kimya mwenendo huu unaoendelea?
Hivi Daudi A. Bashite amefanya jambo gani ambalo linafanya aone yeye ni bora? Kwanini mawaziri wanaogopa? Kwanini wale think tanker nao wamefyata mkia?.
Nahisi watanzania wote tupaze sauti iwe kwenye Facebook, tweeter,Instagram na mitandao yote tudai utawala wa sheria.
Nape ni kiungo mkubwa sana kwa chama hiki Rais awe makin sana
 
Tukumbuke aliyosema Rais Mstaafu Mh. Kikwete hivi majuzi wakati wa Mkutano mkuu maalumu wa CCM. Alisema, Mh. Kinana alikijenga sana chama muda mfupi kabla ya uchaguzi mkuu wa Rais wa awamu ya tano.
Msaidizi mkuu wa kinana alikuwa Nape. Alijitoa mhanga kweli kweli na kwenye uchaguzi wa Rais alipambana usiku na mchna kuhakikisha CCM inapata ushindi wa kishindo.
Lakini wahenga wanasema Uongo na makosa ya mkubwa yana maana zaidi kuliko ukweli na utii wa mtu mdogo. Huko Arusha Tajiri akienda kwenye ofisi ya Tajiri mwenzake na kukutana na mhudumu wa ofisi huwa hapendi kuulizwa shida yake na mhudumi.
Mhudumu akiuliza hujibiwa na Tajiri kwa maneno yafuatayo. " SIONGEI NA MBWA, NAONGEA NA MWENYE MBWA"
Nape ameingia kwenye Serekali lakini bado ana hulka ya kisiasa kuliko ya Kiserikali ambayo imemwathiri. Serikalini unatakiwa kufanya kila jambo kwa kufuata kanuni na sheria. Unaweza kufanya jambo jema lakini bila kufuata kanuni na sheria, utawajibishwa. Kwenye Siasa unatenda lililo sahihi kwa umma kwa wakati ule bila kujali sana kanuni na sheria.
Arudi kwenye chama akakijenge upya.
 
Sina shaka ya namna ya kuelewa kuwa kuna tofauti kati ya kuchafuka kwa matope na kuwa ndani ya dimbwi la matope
 
Napa hongela mueshimiwa Nape kwakujalibu..lkn ukweli umezihilika kua chama chake ccm kimemsaliti.. Nahii ndio tabia ya ccm hawajamaa huwa wanatabia yakumutumia mtu nawakisha fanikisha wanamtupa pembembeni..mueshimiwa Nape wamekutumia nasasa wamekutupa pembembeni bila hata kuangalia kazikubwa uliyoifanya kuuweka utawala huu madalakani nakumbuka iliupigania huu utawala hadi ukasema hata kwa goli lamkono ccm itashinda nakweli mlishinda kwagoli lamkono. Yotehayo yalikuwa mawazoyako lkn leo umeonekana huna lolote lamaana..hiyo ndio siasa ya ccm
 
Mimi sijalibiwi na 2020 nitachaguliwa na kura ya bashite
Bashite alikuwa mjumbe kwenye kile kikundi kiliiba kura pia mali za Mkulu zote zinatunzwa na Daud bashite zipo siri nyingi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom