Pre GE2025 Nape Nnauye: Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza, ili mradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Uchaguzi una mambo mengi, kama Chadema walimuibia kura Mchungaji Msigwa kwenye uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kanda, mpaka akachukia akahama Chama.

Ila Byabato hatarudi Bungeni, analalamikiwa sana na wapiga kura, hapokei simu ili aelezwe kero.
Nashindwa kuamini kwamba Msigwa aliibiwa kura ndiyo sababu akahamia CCM, na kama ilikuwa hivyo basi ni ujumbe ulikuwa unafikishwa kwamba tumeshapata habari unahitajika urudi kundini, wanakuita.
 
Kwa kauli alizozitoa hata wananchi wa jimbo lililomchagua kama wanaoufahamu wa kutosha hawatampigia kura zaidi ya moja, ya kwake mwenyewe. Kwa kifupi amewadhalilisha wananchi wa jimbo lake.
 
Nimesikitishwa sana na kauli hii ya Ndugu Nape. Kumbe ushindi wa CCM huwa kila uchaguzi ni nje ya boksi. Nape hatakiwi kuendelea kukalia kile kiti cha uwaziri na ninamshauri mteule wake amtengue mara moja kwa kuwa kauli yake imeleta sintofahamu ndani ya jamii inayoongozwa na Mhe. Rais.
 
Kaniacha hoi hapo aliposema

"Milioni mia tatu (300) ni fedha ndogo sana"

😂😂😂... Ngoja nijichange nikimbillie mtoni, nikawe cheap labour, tuwaache wenye nchi yao.
 
Nape safari hii Hatutakubali, Nakuhakikishia kwamba Nchi utaipasua wewe na wenzako, hatutakubali ujinga tena, Waambie kabisa wanaokutuma

Safari hii Patachimbika

Safari hii hamkubali.

Kwa hiyo safari zile mlikubali.

Kwa nini mlikubali ??????????
 
uwizi hata shuleni ndo ilikuwa mchezo wake, hata sasa pale open university
Kwa kweli ukiangalia clip nyingine inayosambaa ikihusu jinsi alivyoshiriki kwenye uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki unapata wepesi wa kukubali unayoyosema, kwamba hakuna alicho nacho ambacho ni cha halali. Hivi ana elimu ya level gani huyu kijana?
 
Inaonekana kauli ya Nape na nyingine zinazotolewa kuwa kwa hali ya mifumo ya uchaguzi iliyopo upinzani hauwezi kushinda kutokana na wizi wa Mzee wa Nusu Halali na Haramu,kwa hali ilivyo wapenda haki kwenye uchaguzi wanaweza wasishiriki kwenye uchaguzi na kusababisha wapinzani kupigwa chini. Tafuteni mbinu ya kisayansi kuikabili kauli hii,vinginevyo wengi tutaona haina maana kushiriki uchaguzi kuanzia serikali za mitaa. Mutuhakikishie wizi hautatokea.
 
Huyu mshenzi kachafua hali ya hewa vibaya sana.
 

Sidhani kama kauli ya Nape ndio imechangia, na kama imechangia ni kwa kiasi kidogo sana, maana tayari wananchi wameshapuuza chaguzi zetu. Ukiangalia vizuri hamasa ya wapiga kura ilikuwa inaongezeka kila mwaka kabla ya Magufuli kuingia madarakani. Lakini baada ya Magufuli kuingia tukaanza kushuhudia chaguzi za kihayawani mno.

Hata uchaguzi wa 2020 ulikuwa na wapiga kura wachache sana, ukweli unaofichwa, kutokana na maagizo ya Magufuli ya kulazimisha wagombea wa ccm kutangazwa washindi bila kujali box la kura. Na lengo la Magufuli ilikuwa ni kuhadaa umma na dunia kuwa ni kiongozi aliyeiimarisha ccm, na kuifanya kupendwa tena, wakati uhalisia ni kuwa watu walishaichoka ccm. Na kitendo cha sasa ccm kulazimisha tume iwe chini ya mwenyekiti wao huku tukiwa na kumbukumbu ya ya uchafu wa 2019-20, ndio kutachangia zaidi wapiga kura kuwa wachache.

Inshort Tanzania hakuna uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Ccm ishauriwe kuwa sio chama cha kizazi hiki, na haiwezi kuendelea kushurutisha kubaki madarakani bila ridhaa ya umma. Ni aidha machafuko au mapinduzi ya kijeshi, ili heshima ya box la kura irejee.

ChoiceVariable Lucas Mwashambwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…