Sidhani kama kauli ya Nape ndio imechangia, na kama imechangia ni kwa kiasi kidogo sana, maana tayari wananchi wameshapuuza chaguzi zetu. Ukiangalia vizuri hamasa ya wapiga kura ilikuwa inaongezeka kila mwaka kabla ya Magufuli kuingia madarakani. Lakini baada ya Magufuli kuingia tukaanza kushuhudia chaguzi za kihayawani mno.
Hata uchaguzi wa 2020 ulikuwa na wapiga kura wachache sana, ukweli unaofichwa, kutokana na maagizo ya Magufuli ya kulazimisha wagombea wa ccm kutangazwa washindi bila kujali box la kura. Na lengo la Magufuli ilikuwa ni kuhadaa umma na dunia kuwa ni kiongozi aliyeiimarisha ccm, na kuifanya kupendwa tena, wakati uhalisia ni kuwa watu walishaichoka ccm. Na kitendo cha sasa ccm kulazimisha tume iwe chini ya mwenyekiti wao huku tukiwa na kumbukumbu ya ya uchafu wa 2019-20, ndio kutachangia zaidi wapiga kura kuwa wachache.
Inshort Tanzania hakuna uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Ccm ishauriwe kuwa sio chama cha kizazi hiki, na haiwezi kuendelea kushurutisha kubaki madarakani bila ridhaa ya umma. Ni aidha machafuko au mapinduzi ya kijeshi, ili heshima ya box la kura irejee.
ChoiceVariable Lucas Mwashambwa