Pre GE2025 Nape Nnauye: Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza, ili mradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe!

Pre GE2025 Nape Nnauye: Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza, ili mradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia na Teknolojia ya Habari Nape Moses Nnauye amewatoa wasiwasi wakazi wa Bukoba na wanachama wa CCM kuwa Mbunge wao Stephen Byabato atashinda uchaguzi ujao na hakuna mwingine.

"Matokeo ya kura siyo lazima yawe yale ya kwenye box, inategemea nani anahesabu na nani anatangaza. Unajua kuna mbinu nyingi za uchaguzi, Kuna halali, nusu halali na haramu na zote zinaweza kutumika ilimradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe" alisema Nape.

Aliyesema hayo katika Soko la Kashai jana Julai 15 usiku alipoalikwa na Mbunge Byabato kushuhudia ramani na michoro ya Soko jipya la Kashai linalotarajiwa kujengwa.

Kauli ya Chama ~
CCM yakataa maneno aliyosema Nape kuhusu ushindi wa kura unategemea na anayehesabu kura

Pia, utetezi wake: Kuelekea 2025 - Nape Nnauye: Kauli ya "Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza" ilikuwa ni ya utani

PIA SOMA
- Mitandao ya simu inapaswa kutoa ufafanuzi hii kauli ya Nape haitakiwi kupuuzwa hata kidogo
Okay
 
Natangaza rasmi Kumdharau Kabisa Nape Nnauye katika kipindi chake chote alichosaliwa nacho hapa Duniani

Huyu alisababisha bunge lisioneshwe live ili wananchi wasifuatilie.

Hadi Leo bunge halioneshwi mubashara na huenda ni kwa bongo tu kwa Ulimwengu mzima.

Kenya waliweza hadi kujua ni mbunge yupi amepitia mkuria ya ndio muswada wa sheria ya fedha wenye utata
 
!
Ni kweli.
Na mwenye jukumu la kuwaelimisha ndio hataki maana udhaifu wao ndio umamsaidia kuwafanya watakavyo.
Mfumo wa elimu ni
Tatizo ni wananchi kuelimika na kutumia haki zao tu.

Kwani hao wakubwa wa vyombo vya dola wako wangapi?
wa hewala, kusifu na kuabudu ,
Hautoi uwezo wa kuhoji na fikra huru nje ya box.
Hata uamuzi wa kuandikwa kwa Katiba imekuwa ni kwa hisani ya raisi au chama fulani tu badała ya wananchi.

Watatokaje hapo?
 
Sidhani kama kauli ya Nape ndio imechangia, na kama imechangia ni kwa kiasi kidogo sana, maana tayari wananchi wameshapuuza chaguzi zetu. Ukiangalia vizuri hamasa ya wapiga kura ilikuwa inaongezeka kila mwaka kabla ya Magufuli kuingia madarakani. Lakini baada ya Magufuli kuingia tukaanza kushuhudia chaguzi za kihayawani mno.

Hata uchaguzi wa 2020 ulikuwa na wapiga kura wachache sana, ukweli unaofichwa, kutokana na maagizo ya Magufuli ya kulazimisha wagombea wa ccm kutangazwa washindi bila kujali box la kura. Na lengo la Magufuli ilikuwa ni kuhadaa umma na dunia kuwa ni kiongozi aliyeiimarisha ccm, na kuifanya kupendwa tena, wakati uhalisia ni kuwa watu walishaichoka ccm. Na kitendo cha sasa ccm kulazimisha tume iwe chini ya mwenyekiti wao huku tukiwa na kumbukumbu ya ya uchafu wa 2019-20, ndio kutachangia zaidi wapiga kura kuwa wachache.

Inshort Tanzania hakuna uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Ccm ishauriwe kuwa sio chama cha kizazi hiki, na haiwezi kuendelea kushurutisha kubaki madarakani bila ridhaa ya umma. Ni aidha machafuko au mapinduzi ya kijeshi, ili heshima ya box la kura irejee.

ChoiceVariable Lucas Mwashambwa

Huwa nakuelewa @ Tindo
 
!
Ni kweli.
Na mwenye jukumu la kuwaelimisha ndio hataki maana udhaifu wao ndio umamsaidia kuwafanya watakavyo.
Mfumo wa elimu ni

wa hewala, kusifu na kuabudu ,
Hautoi uwezo wa kuhoji na fikra huru nje ya box.
Hata uamuzi wa kuandikwa kwa Katiba imekuwa ni kwa hisani ya raisi au chama fulani tu badała ya wananchi.

Watatokaje hapo?
Kosa la kwanza ni kufikiri kuna mtu ana jukumu la kuelimisha wananchi.

Kwanza kabisa, kila mtu ana jukumu la msingi kujielimisha mwenyewe.

Serikali ina dhamana na jukumu la kuweka misingi ya elimu hiyo kuwapo.
 
Hewalaa!
Hapa ndipo tunapopigiwa
 
Nakubaliana na TUNDU LISSU zaidi ya asilimia 100. Hatupaswi kufanya uchaguzi bila kufanya Marekebisho ya KATIBA NA TUME YA UCHAGUZI.

Maneno haya ya Nape ni ushahidi tosha unaopaswa kuwaamsha kutoka usingizini Watanzania wote na kuanza kuunga mkono maazimio ya CHADEMA kuwa No Reform No Election.

CCM wanatuona wananchi wa hii nchi ni wajinga sana.
 
Iko wazi kabisa
 
Back
Top Bottom