Nape Nnauye: Mwenyezi Mungu ameamua ugomvi

Nape Nnauye: Mwenyezi Mungu ameamua ugomvi

Yeye Magufuli alipokuwa hai mbona hakuwaacha wenzie wapumzike kwa amani?

Yuko wapi Ben Saanane? Azori Gwanda, Lissu Lema na wengineo tusiojua majina yao.

Acha watu waseme ya moyoni, kama alifanya mazuri atasemwa kwa mazuri na kama alifanya maovu atasemwa kwa maovu yake, kila mtu ana hadithi yake.
Kwahiyo imani za dini zenye kukataza kumsema marehemu zinakosea kwa kufanya hivyo?
 
Ni kweli alichosema Nape, Mungu amelata amani

Na kifo chake sio kimeleta amani kwa CCM tu, bali kwa vyama vingine na kwa nchi kiujumla, vyama vya upinzani walikuwa wakiwindwa kama swala,

hata ugomvi wetu na nchi jirani umeisha na sasa Tz inafanya biashara na majirani zetu vizuri

Na sio nchi jirani tu, hata jamii kubwa ya kimataifa ilikuwa na ugomvi na Tanzania ila baada ya Mungu kufanya yake, sasa hivi Tanzania ni rafiki wa kila nchi, za Mashariki na Magharibi

Ama kweli Mungu ameleta amani, MUNGU NI FUNDI
Mungu ni wa ajabu sana, maana Mungu huyo huyo amewachukulia kipenzi chao wazanzibari Maalim seif.
Sijui alikuwa na makusudio gani?
 
Nape anaongea sio kesi.Mungu yupo na hajafa bado ataendelea kuamua kesi Nape na wote wanaomkebehi marehemu Magufuli kwani wao wataishi milele? hata wao Mungu aweza amua kesi anytime. mahakama kuna ya mwanzo,mahahakama kuu na rufaa Nape na wakebehi Magufuli sijui wanaongelea mahakama ipi?
Anyway Mungu hakimu na Jaji tunakuachia wewe ujuaye nani muovu na nani siyo uendelee kutoa hukumu ya haki iwe kwa Nape au kwa yeyote ni haki yako kutoa hukumu

Na tutaipokea kwa mikono miwili
 
Habarini JF GT!

Jana wakati Membe akirudishiwa kadi ya CCM, Mbunge wa Mtama na Wazari wa Habari nchini aliongea kauli mbaya Sana Na Yenye kufedhehesha kwa Marehemu.

Kwa tamaduni za kitanzia Sio sawa kumsema Marehemu, na hata Ukitaka kumsema Marehemu utamsema kwa Mazuri. Lakini hii imekuwa Tofauti kabisa kwa baadhi ya Wanachama wa CCM na Viongozi wa CCM, wamekuwa Wakimsema Hayati Magufuli Hadharani mbele ya wananchi waliomchagua kwa kura nyingi. Hakika CCM inajiua Yenyewe

Jana Ndugu Nape (Namuita Ndugu kwasababu kwangu mimi sioni kama Anafaa kupewa heshima ya Jina Mheshimiwa) wakati wa Sherehe zile alisimlia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na Yeye alivyo nusurika kufukuzwa CCM na Membe kumsadia, kipindi hicho naamini Magufuli hakuwa Kiongozi mkubwa wa CCM, Nape aliongea kumaanisha kuwa Magufuli alikuwa chanzo kikubwa cha Membe kuondoka CCM na Kutengeneza ugomvi mkubwa na Wana CCM wengine.

Nape akaenda mbali zaidi na Kusema Kuwa Ugomvi huo Mungu ndio ameamua na sasa bahari imetulia iko shwari, akimaanisha Kifo cha Magufuli ni Maamuzi ya Mungu katika Kutatua ugomvi wa Wana CCM na Membe… Akaendelea mbele na Kusema nani Kama Rais Samia Suluhu.

Ikumbukwe kuwa Huu utamaduni uliopo sasa kwa kumsifia rais hata pale anapo fanya Baya ulianza kipindi Cha Magufuli na Umeendelea hadi awamu hii kwa kusema Mama anaupiga mwingi. Nyakati za Kikwete, Mkapa hakukuwa na huu ujinga.

Turudi kwenye mada, Nape Nauye ni lini Ataacha kuwa na Kinyongo na Marehemu? Nilini ataacha Kumsema Marehemu? Huu umekuwa muendelezo wake toka Awe Waziri tena Wa Habari, Je aliteuliwa kuja Kumsema Marehemu?

Ni wakati sasa Wa Nape kumuacha Marehemu Apumzike Mahali pema na kwa amani. Asitafute chuki na watu zisizo za msingi
Mbona kama wewe ndio umetoa tafsiri hiyo!
 
MUNGU yupi huyo anayemtaje? labda mwenye herufi ndogo m!!! mungu aliamua ugomvi au watu fulani waliamua ungomvi!! bora kunyamaza .damu ya mtu haimwachi mtu salama iko siku mtaanza kuropoka.time will tell.
Na kuropoka kwenyewe ndiyo huko!, kwani JPM ndiye alimzuia Membe au joka la mdimu asipate nafasi yakugombea urais?
 
Mtu mwenye akili hawezi kuongea upupu Kama huo.Kwani mwenyezi Mungu ni wa Nape na Membe tu?Hiyo ni akili ya chooni.Watu Kama hawa huwa wanaumbuliwa ili akili za chooni ziwakae vizuri.Kama kweli Mungu ni wa Nape na Membe,tusibiri tutaona.Tutakuja kuandika Tena hapa hapa.
Yawezekana ni Mungu wao wawili tu.
 
Kwani uongo. Referee Mungu alimaliza Moira kabla watu wengi hawajaumia uwanjani
Watu walilia hadi wakazimia

Katika_Historia%3A%0APamoja_na_kwamba_ALIZIMIA_baada_ya_kuuona_mwili_wa_mpendwa_wetu_MFUKO_hak...jpg

Ila hawakuachia mifuko ya sato
 
Ila kina Nape haya maneno ya shombo yatawacost ikitokea Rais Ajaye akawa na akili atawapiga chini wote

Ningekuwa Rais uchaguzi ujao Kuna majimbo Bora niwape wapinzani tu, Nape ni mropokaji
This is very stupid and dangerous!
Kwenye uchaguzi mkuu sio kazi ya rais kugawa majimbo kwa chama tawala au upinzani! Huu ni upumbuvu!
Uchaguzi unapaswa kuwa huru na wa haki, sio wa rais kugaia chama chochote majimbo yoyote.
 
Habarini JF GT!

Jana wakati Membe akirudishiwa kadi ya CCM, Mbunge wa Mtama na Wazari wa Habari nchini aliongea kauli mbaya Sana Na Yenye kufedhehesha kwa Marehemu.

Kwa tamaduni za kitanzia Sio sawa kumsema Marehemu, na hata Ukitaka kumsema Marehemu utamsema kwa Mazuri. Lakini hii imekuwa Tofauti kabisa kwa baadhi ya Wanachama wa CCM na Viongozi wa CCM, wamekuwa Wakimsema Hayati Magufuli Hadharani mbele ya wananchi waliomchagua kwa kura nyingi. Hakika CCM inajiua Yenyewe

Jana Ndugu Nape (Namuita Ndugu kwasababu kwangu mimi sioni kama Anafaa kupewa heshima ya Jina Mheshimiwa) wakati wa Sherehe zile alisimlia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na Yeye alivyo nusurika kufukuzwa CCM na Membe kumsadia, kipindi hicho naamini Magufuli hakuwa Kiongozi mkubwa wa CCM, Nape aliongea kumaanisha kuwa Magufuli alikuwa chanzo kikubwa cha Membe kuondoka CCM na Kutengeneza ugomvi mkubwa na Wana CCM wengine.

Nape akaenda mbali zaidi na Kusema Kuwa Ugomvi huo Mungu ndio ameamua na sasa bahari imetulia iko shwari, akimaanisha Kifo cha Magufuli ni Maamuzi ya Mungu katika Kutatua ugomvi wa Wana CCM na Membe… Akaendelea mbele na Kusema nani Kama Rais Samia Suluhu.

Ikumbukwe kuwa Huu utamaduni uliopo sasa kwa kumsifia rais hata pale anapo fanya Baya ulianza kipindi Cha Magufuli na Umeendelea hadi awamu hii kwa kusema Mama anaupiga mwingi. Nyakati za Kikwete, Mkapa hakukuwa na huu ujinga.

Turudi kwenye mada, Nape Nauye ni lini Ataacha kuwa na Kinyongo na Marehemu? Nilini ataacha Kumsema Marehemu? Huu umekuwa muendelezo wake toka Awe Waziri tena Wa Habari, Je aliteuliwa kuja Kumsema Marehemu?

Ni wakati sasa Wa Nape kumuacha Marehemu Apumzike Mahali pema na kwa amani. Asitafute chuki na watu zisizo za msingi
Huo ndio uhuru wa kutoa maoni tunaoutaka
 
ni kwel
Lazima tuwaze JANA ili kuifanya LEO na KESHO yetu kuwa BORA ZAIDI. Ikiwa hujui utokako (JANA) utafahamu vipi ulipo (LEO) na uendako (KESHO).Ikiwa hujui wapi tatizo lilipoanzia huwezi kupata utatuzi juu yake. Hatma bora huja kwa kurekebisha jana yetu.

Hivyo basi, mema husafiri POLEPOLE lakini hudumu vizazi, mabaya husafiri kwa KASI zaidi hufutika mapema moyoni.

Tujitathimi jinsi tunavyoishi na wengine,duniani sote tuko njiani.

MIAKA 80 IJAYO WATAKAOKUWA HAI HUMU JUKWAANI NI WACHACHE MNO,AU WASIWEPO KABISA.
ni kweli lakini tunatumia muda mrefu mno kwenye visasi na muda hautusubiri na kushughulikia mihemko yetu na wakati mwingine bila kujali tunalo jukumu la leo la kuwavusha wengine.
 
Back
Top Bottom