Nape Nnauye: Mwenyezi Mungu ameamua ugomvi

Kweli Maamuzi ya Mungu yameliponya Taifa pamoja na Nape.
 
Kinyongo hakiwezi kuisha kamwe maana Marehemu alimvua uwaziri kwa hila na ukabila na mwisho akataka kumpoteza kama alivyompoteza Ben Saanane.
 

Jinsi ulivyoishi na binadamu wenzako ulipokuwa hai, ndivyo utakavyokumbukwa ukiwa mfu. Msilazimishe mazuri, kama yapo yatasemwa tu. Nimecheka hapo unaposema "mbele ya wananchi waliomchagua kwa kura nyingi " 😀
 
It is total foolishness kucoment juu ya marehemu vibaya. Hata kama alikuwa mbaya. Kifukua makaburi unaweza ukafukua na hasira na chuki na vita. Magu alikuwa na wafuasi wengi innocent na chuki ikiibuka hakuna wa kupona. It is wiser kumzika marehemu na mambo yake yote. Nape is a fool na hana sifa ya kuwa kiongozi wa umma
 
Mbona na wewe mchochezi,mbona nawewe unawasema vibaya🤔
 
Japokuwa Nape namdharau sana lakini katika hili yuko sahihi, marehemu alileta siasa za kishenzi za kuhasimiana na umwagaji damu,kwa jinsi alivyokuwa anatumia vibaya vyombo vya dola kuwamaliza wapinzani wake ndani na nje ya CCM ilikuwa vigumu kumuondoa, lakini Mungu kwa alivyolipenda taifa letu alimalizana naye bila makeke wala umwagaji damu. Mungu Fundi sana.
 
Hadithi aliitengeneza mwenyewe kuziba watu midomo ni kuwaonea.
 
Kinyongo cha Nape kwa Marehemu JPM, ni kutumbuliwa uwaziri wa wizara ya habari. Siku Rais Samia Suluhu atakapomwondolea uwaziri wake, kinyongo chake hicho atakielekeza kwa Samia vile vile. Yeye anaamini cheo hicho cha uwaziri, kwake ni cha kidumu na ni haki yake.
 
Hakuna mtu nimewahi kusoma sehemu yoyote akikejeri kifo Cha Hitler Wala Idd Amin, HAKUNA !!!
Kwanza Hitler aliamini hawezi kuuliwa na ni vigumu Sana yet kufa,aliwahi hata kutaja hadharani kwamba yeye hawezi kufa,
Watu hawakejeli kifo. Wanakejeli mate do yao maovu.

Ukitenda mabaya tutayasema hata kama umededi
 
Nape kinachomuuma zaidi ni kitendo cha yeye kwa kujipendekeza kutembea kwa,magoti Ikulu huku akirekodiwa alipokwenda kumuomba,msamaha Magufuli. Hiyo rekodi haifutiki milele. Magufuli hakumwambia Nape atembee kwa magoti bali kiherehere chake cha kinafiki. Nafikiri hilo jambo linamtesa sana. Laiti angejua .Magufuli angekufa punde baadae asingefanya lakini too late.

Nape aliwahi kufukuzwa CCM na mzee Makamba huku akitamba kuwa amemfuta duniani na mbinguni, isingekuwa Jk kumuokoa angekuwa historia mbona hamuwekei kinyongo Makamba;

Kuendekeza nja kubaya sana.
 
Haya ukitoa Nape na hasira zake kwa Mwendazake lakini chama pia kinayabariki. Amezungumza hadharani na viongozi wakiwepo. Hizi mbegu wanazipanda wenyewe tena kwa msisitizo! Hicho chama visasi havitakoma, bahati mbaya vitagharimu Taifa.
 
Usifikiri Nape hana akili kama wewe fikra zako ni fupi sana uwaziri unateuliwa lakini upumbavu na dharau ni sifa za Mwendazake.
 
Ila kina Nape haya maneno ya shombo yatawacost ikitokea Rais Ajaye akawa na akili atawapiga chini wote
Ningekuwa Rais uchaguzi ujao Kuna majimbo Bora niwape wapinzani tu,Nape ni mropokaji
Sema ikitokea rais ajaye akawa kichaa na mwendawazimu Kama jpm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…