Nape Nnauye: Mwenyezi Mungu ameamua ugomvi

Hivi Zitto alisemaje vile???
 
Mtoto wa moses! inabidi huyu mheshimiwa asilewe madaraka bali atafakari 2025 uchaguzi mkuu. ajihadhali na kumsema vibaya John. hayati John Pombe magufuli hapaswi kuchafuliwa maana inawakera mamilion ya watu waliovutiwa na uongozi wake. hivyo hao watu nao hulipiza kisasi kumsema vibaya mama akiwa madarakani. sasa jiulize 2025 kitatokea nini? maandiko yanasema thamani ya kumpenda umchukiaye ni sawasawa na kumchukia tuu. hivyo haina maana kumsema vibaya JPM maana hayupo sasa utafaidika na nini kumsema vibaya? mimi sio mshabiki wa John ila nataka uchaguzi wa 2025 uwe shwari na uvutie africa.
 
Magufuli qna wafuasi wake..Wengi tu hata kama ni kweli alitenda ubaya kuweni makini kumsema vibaya....
 
Kama Nape kasema ukweli bila kupindisha maneno ndio kutii amri za Musa,hana la kujutia.
Vile vile Chosa Shakespeare katika kitabu alichoandika, Julius Ceasars,tunamwona Mark Antony alipokuja kumzika rafiki yake Julius Ceasars alisema mazuri au mabaya atendayo binadamu yanaishi hata akisha kufa.
Hilo ni fundisho kubwa kwa binadamu.
Kama Mjomba Magu aliwatenda mazuri tutayasifia na tuendelee kuyasifia.
Lakini kama Mjomba Magu aliwatendea maovu wananchi hatuwezi kumpaka kilemba cha ukoko, watamtungia hata vitabu vya historia yake ili liwe funzo hata kizazi cha mbeleni.
 
Maneno ya nape ni maono toka kwa Mungu
 
Jamani chonde chonde huyu Nape si alishaomba msamaha kwa JPM na akapewa? Sasa kitu gani zaidi? Tulimuona akitembea kwa miguu kwenda ikulu ndipo alipoonyesha kilema chake sasa leo amerudi kwenye ubingwa wake na aliyemteua anakaa kimya maana yake anafurahia basi tusubiri 2025
 
Magufuli qna wafuasi wake..Wengi tu hata kama ni kweli alitenda ubaya kuweni makini kumsema vibaya....

Wafuasi wake watafanya nini, njia nzuri ilikuwa ni box la kura kuheshimiwa ili hizo hasira za wafuasi wake zionekane. Kwa bahati mbaya yeye alikuwa mlevi wa madaraka, na hakuheshimu box la kura. Sasa hawa wengine hawawezi kuheshimu box la kura, hizo hasira zao zitaonekanikia wapi?
 

Alienda kuomba msamaha ili abaki kwenye ulaji. Ifahamike Nape hakuwa na makosa bali hofu ya kukosa ulaji ndio yalimfanya aombe msamaha wa kinafiki.
 
Mi nashangaa ule uhaini wa kumuita raisi mshamba sijui kwanini system ilimuacha
 
Imagine ni wangapi walikuwa kwenye hit list yake? Na kifo chake wameokoka? Kama jakaya alikuwa ni nxt target nani mwingine angekuwa salama? Tunavuna tunachopanda.
Yaani kuna watu mazoba sana.
Yaani unaondoa watu unaojua kuwa watakuwa kikwazo kwenye mpango wako wa kujitwalia ufalme mmoja mmoja, kisha unataka wao wajue na wakuache tuu.
Lazima wakuwahi kukutanguliza.
 
Kuna ambae anampa kiburi Nape aropoke na kumtukana rais alietangulia mbele ya haki.
 
Wewe ni mataga hata kama huna kadi mfukoni.
Lini mimi nikawa mwanachama wa chama cha siasa? Sijawahi na sitegemei! Vyama vina unafiki ambao siuwezi nitaporwa kadi siku hiyo hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…