Nape Nnauye: Niliomba Ubunge na Mungu ndiye mpaji, amenipa!

Nape Nnauye: Niliomba Ubunge na Mungu ndiye mpaji, amenipa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mbunge wa Mtama mkoani Lindi mh. Nape Nnauye amewataka Wanasiasa na Wananchi kuwaheshimu viongozi kwani urais hutoka kwa Mungu.

Nape ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter kwamba yeye aliomba ubunge na Mungu amempa.

Maendeleo hayana vyama!
 
Siku zote Nape ni wa hovyo tu. Kiongozi bora siku zote anatakiwa awaombe anaowangoza kushirikiana kwa pamoja ili kusukuma maendeleo mbele.

Sasa yeye anataka aheshimiwe ndio ujinga ninaolalamika hapa kila siku. Akili zetu waafrika bado zina usokwe au dume la nyani.
Yaani mwafrika akipata kanafasi anajiona ni kama mungu anazalau ote waliochini yake.

Kuna shida kubwa sana hapa tanzania.

Mtu akiwa mwana CCM akikutana na mtu ambae sio CCM anamuona kama hana haki ya kuwa mtanzania, atafanyiwa figisu hata kama ana kabiashara kake wanakikisha wanakaua.

Na akipewa wadhifa huko CCM ndio usiseme.
Mimi nachukia sana tabia hizi.

Bora angesema mwenyez mungu amewaongoza watu wa mtama kumuamini kupata nafasi ya kuwaongoza na hivyo waendelee kumuombea waweze kushirikia ili kusukuma maendeleo mbele zaidi.
 
Ah wapi!

Hakuna cha mungu wala nini.

Mungu gani huyo anayeachia uporwaji wa demokrasia utendeke waziwazi namna hiyo?

Mungu wa wapi huyo?

Bila Tume Huru tusahau demokrasia Tanzania.

Watanzania tulifanya kosa kipindi cha mchakato wa katiba mpya kwenye utawala wa JK ndo kipindi ilitakiwa tuwe na katiba nzuri inayowasemea wananchi. Tulitakiwa kungangana mpaka katiba ipatikane.

Kwa sasa itatuchukua muda sana kumpata mtu ambaye angalau atawaza kufanya tena mchakato kama huo!!
 
Ifikapo 2025 utawasikia ‘twende na Shangazi’.

Watashiriki tena uchaguzi.

Na baada ya kupigwa, wataanza tena kulia, kana kwamba kuna jipya walilofanyiwa ambalo hawajawahi kufanyiwa huko nyuma!
 
Kiongozi bora ni yule anaechaguliwa na wengi na sio na tume baada ya mahera kutii maagizo toka juu
 
Mungu huyuuu! Kwann anampa huyu anamnyima yule, anyway kama riziki ni mafungu naomba langu lijazwe
 
Mbunge wa Mtama mkoani Lindi mh. Nape Nnauye amewataka wanasiasa na wananchi kuwaheshimu viongozi kwani urais hutoka kwa Mungu.

Nape ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter kwamba yeye aliomba ubunge na Mungu amempa.

Maendeleo hayana vyama!
Nape asimkufuru Mungu hata kumwingiza kwenye mambo ya kishetani yaliyofanywa na CCM, serikali, na Mr. Jiwe.

Nape amshukuru shetani maana naye amepewa mamlaka katika Ulimwengu wake wa giza ambao umekuwa Ulimwengu wa CCM kwa kiasi kikubwa.
 
Ifikapo 2025 utawasikia ‘twende na Shangazi’.

Watashiriki tena uchaguzi.

Na baada ya kupigwa, wataanza tena kulia, kana kwamba kuna jipya walilofanyiwa ambalo hawajawahi kufanyiwa huko nyuma!

Upinzani Tanzania walitakiwa waweke mkakati wa kujipanga kudai tume huru mapema kabisa badala ya kusubiri kuzima moto kipindi cha uchaguzi.

Wakija na hoja nzito nina uhakika watasikilizwa ingawa hawana platform ya kusemea tena.

Tusema tu kwa ujumla kuwa na tune huru, ni baada labda ya miaka kumi au zaidi ijayo!
 
Marekani wana Tume huru lakini Trump anawapelekesha isivyo kawaida!
 
Back
Top Bottom