Nape Nnauye: Niliomba Ubunge na Mungu ndiye mpaji, amenipa!

Nape Nnauye: Niliomba Ubunge na Mungu ndiye mpaji, amenipa!

Mbunge wa Mtama mkoani Lindi mh. Nape Nnauye amewataka Wanasiasa na Wananchi kuwaheshimu viongozi kwani urais hutoka kwa Mungu.

Nape ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter kwamba yeye aliomba ubunge na Mungu amempa.

Maendeleo hayana vyama!
Kapewa na NEC.Aaache kumuingiza Mungu katika mambo ya kihuni!
 
Ah wapi!

Hakuna cha mungu wala nini.

Mungu gani huyo anayeachia uporwaji wa demokrasia utendeke waziwazi namna hiyo?

Mungu wa wapi huyo?

Ushahidi ni muhimu, Nyani tusaidie ushahidi wa wazi ili tuweze ku concreting malalamiko yetu kisheria, naona mpaka sasa tume paralyse.
 
Mbunge wa Mtama mkoani Lindi mh. Nape Nnauye amewataka Wanasiasa na Wananchi kuwaheshimu viongozi kwani urais hutoka kwa Mungu.

Nape ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter kwamba yeye aliomba ubunge na Mungu amempa.

Maendeleo hayana vyama!
Tanzania inachokitafuta itakuja kukipata tu; kumchanganya Mwenyezi Mungu Mungu na shetani-ibilisi. Mtakuja kukipata tu kwani Mwenyezi Mungu kamwe hadhihakiwi na kila mtu apandacho...
Kwa nini nasema hivi?
Ni wazi, 85% ya wabunge na madiwani wanajihusisha na ushirikina pamoja na uchawi kupata nafasi hizo. Wanaloga, wanawanga, wanatoa kafara hata za binadamu wenzio, kwa jina la mungu. Anyway, miungu ipo mingi sijui ni mungu yupi wanayekuwa wanamtaja.
Sasa, wanasiasa wa Tanzania mnapaswa kujua, pamoja na Mwenyezi Mungu kuwa mwenye rehema, huruma, neema, upendo, na fadhili zake ni za milele; kamwe, hachangii utukufu wake na mwingine yeyote akiwemo shetani-ibilisi. Hachanganywi.
Angalieni viongozi wetu mtakuja udumbukiza Nchi kubaya pindi "kikombe cha hasira ya BWANA Mungu" kitakapokuwa kimejaa kutokana na dhambi na uovu wenu mwingi.
Nanyi Watumishi wa Mungu, waambieni ukweli wanasiasa kwani wanachofanya siyo sahihi mbele za BWANA Mungu. Waache kuwa vuguvugu, kuna shida huko mbele. Msipowakemea mkaendelea kujipendekeza kwa faida na manifaa za kimwili kama ilivyokuwa wakati wa utawala wa Constantino; kipindi cha akina Nero; mna la kujibu mbele za Bwana Yesu Kristo. Hizi ni nyakati za mwisho. Shetani-ibilisi yupo seriously kazini.
Nashauri tu.
 
Back
Top Bottom