Nape Nnauye: Rais Samia Suluhu aendelee mpaka 2030

Nape Nnauye: Rais Samia Suluhu aendelee mpaka 2030

Naona wananza kujikombakomba yeye makambako na kigwagwara huko twiter wamekuwa wa mipasho utadhani hawakuwa ccm kabisa
 
Ukweli ni kwamba nchi yetu ilitulia sana, tukawa busy na kujitafutia maendeleo na tukichoka akili msanii anapita hapo kati na kiki tunapunguza uchovu na maisha yanasonga.

Ila kwa sasa ile hali ya awamu ya B4 tha late JPM inaanza kujirudia, kila mtu mtoa matamko, kila mtu mshauri mkuu! Kwa kifupi ni ukosefu wa adabu na tunakoelekea tutapoteana!

Kweli JPM alituleta pamoja na kutupa vitu vya kuconcetrate navyo.
 
Enzi za utawala wa jiwe, magamba menzie yakimsifia sifia hata kama ni kwa uongo uongo au kejeli alikuwa anaya awadia shavu la teuzi ( kwa kweli ile ilikuwa style ya nduli iddi amini) sasa mama na yeye tumuone kama ana akili timamu!
 
Kuna wana siasa wa CCM sikujua kama ni minafki,acha waendelee kujitokeza niwajue wote
 
Kitu kimojawapo kikubwa ambacho utawala wa JPM umetuachia ni kuwajua watu katika uhalisia wao !

Viongozi wa Dini wakweli na wanafiki. Wanasiasa matumbo na masilahi. Wafanyabiashara waongo,na wakweli. Wanaharakati waoga na jasiri. Watumishi wazalendo na wanojipendekeza.

Msigwa


Screenshot(31).png
 
Kwa kupitia uchaguzi au kwa mapendekezo yake tu haya?
Kwa utamaduni wa CCM Rais Samia atadumu madarakani hadi 2030.

Huo ndio utaratibu Nape anakumbushia tu maana asije akaibuka Membe mwingine akaleta figisu zake 2025!
 
Ukweli ni kwamba nchi yetu ilitulia sana, tukawa busy na kujitafutia maendeleo na tukichoka akili msanii anapita hapo kati na kiki tunapunguza uchovu na maisha yanasonga....
kutawala milele
 
Utafikiri radio zilizokuwa zimeishiwa battery..., sasa hivi wameziwekea Duracell..., Au mabubu wamepewa sauti (wana mengi ya kusema)
 
Nape anakumbuka shuka kumekucha wakati wenzake wanasifu na kuabudu yeye alikuwa anatukanana na meko [/b]
 
Ule msamaha alioenda kuomba akachukuliwa na makamera unafanya haya maoni ya Nape kukosa msingi,zaidi kujionyesha alivyo mnafiki. Alivyo tayari kwenda kinyume na nafsi yake Ili tu asipoteze nafasi za kisiasa hasa ubunge.

Kwakuwa aliyemuomba msamaha kwa kukosoa utawala wake hayupo tena basi anaanza tena kukosoa mambo yaleyale ambayo yalimfanya aombe msamaha!Nape ni miongoni mwa wanasiasa wachache wa CCM ya sasa ambaye anaweza kusema ukweli hata kama ni kinyume na wanachama walio wengi.Kinachomwaribia ni tabia yake ya uoga,kufikiria zaidi kesho yake kisiasa kuliko kusimamia anachokiamini.

Hii inafanya hata aseme nini,watu wenye upeo wasimtilie maanani.Kwakuwa hasemi hivyo kusaidia au kurekebisha.Bali kujaribu kuendana na maono ya serikali iliyopo Ili kukidhi haja zake za kisiasa na maisha yake binafsi kwa ujumla.Laiti kama angekubali kupigwa na utawala wa Magu na hata akakosa huo ubunge,lakini akaendelea kuwa critic wa serikali ya Magu bila kurudi nyuma wala sijui kuomba msamaha,angejenga bonge la legacy na hata mie ningekuwa shabiki wake kisiasa.Lakini hii kujaribu kuendana na upepo unavyovuma Ili kukidhi matarajio yake binafsi kisiasa kunamtoa katika kundi la wanasiasa muhimu wanaohitaji kufuatiliwa....
 
Hivi mwanasiasa mwenye akili anaweza kweli kusema mtu aongezewe muda mpaka 2030? amesahau Mungu alivyotufundisha watz hata maombolezo hayajaisha,kama Magufuli walitaka kumwongezea na Samia wanataka kumwongezea ina maana watu wazuri wapo haija haja ya kuongezeana muda,tuweke mazingira mazuri tu ya kimfumo.
 
Kwa utamaduni wa CCM Rais Samia atadumu madarakani hadi 2030.

Huo ndio utaratibu Nape anakumbushia tu maana asije akaibuka Membe mwingine akaleta figisu zake 2025!
Tatizo lako hata katiba unaisikia kwenye uhuru na mzalendo na tiibiisiii maana ndiyo vyanzo vyao vya habari
 
Wakashike jembe wanasiasa wa bongo njaa sana.Mtafuteni sugu mkajifunze kwake.Kila siku mnaota kuteuliwa.Mh. Rais tuletee sura ngeni sio hao hao kila siku hakuna asiyetaka kula.
 
Tatizo lako hata katiba unaisikia kwenye uhuru na mzalendo na tiibiisiii maana ndiyo vyanzo vyao vya habari
Kadi yako ya CCM utaichukulia hapo hapo kijijini kwenu Nanguruwe bwashee.

Imeshatumwa!
 
Back
Top Bottom