Ule msamaha alioenda kuomba akachukuliwa na makamera unafanya haya maoni ya Nape kukosa msingi,zaidi kujionyesha alivyo mnafiki. Alivyo tayari kwenda kinyume na nafsi yake Ili tu asipoteze nafasi za kisiasa hasa ubunge.
Kwakuwa aliyemuomba msamaha kwa kukosoa utawala wake hayupo tena basi anaanza tena kukosoa mambo yaleyale ambayo yalimfanya aombe msamaha!Nape ni miongoni mwa wanasiasa wachache wa CCM ya sasa ambaye anaweza kusema ukweli hata kama ni kinyume na wanachama walio wengi.Kinachomwaribia ni tabia yake ya uoga,kufikiria zaidi kesho yake kisiasa kuliko kusimamia anachokiamini.
Hii inafanya hata aseme nini,watu wenye upeo wasimtilie maanani.Kwakuwa hasemi hivyo kusaidia au kurekebisha.Bali kujaribu kuendana na maono ya serikali iliyopo Ili kukidhi haja zake za kisiasa na maisha yake binafsi kwa ujumla.Laiti kama angekubali kupigwa na utawala wa Magu na hata akakosa huo ubunge,lakini akaendelea kuwa critic wa serikali ya Magu bila kurudi nyuma wala sijui kuomba msamaha,angejenga bonge la legacy na hata mie ningekuwa shabiki wake kisiasa.Lakini hii kujaribu kuendana na upepo unavyovuma Ili kukidhi matarajio yake binafsi kisiasa kunamtoa katika kundi la wanasiasa muhimu wanaohitaji kufuatiliwa....