Nape Nnauye: Tuachane na hii habari ya "Sisi Wanyonge", kauli hiyo inatulemaza

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Hii ni sehemu ya nukuu ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akizungumzia marekebisho ya Kanuni ya Maudhui ya Mitandao ya Mwaka 2020, leo Machi 14, 2022. Msome kisha uniambie tuitafakari hii kauli ya WANYONGE.

Watanzania wameanza kuwa wanaongea barabarani wakiongea na simu haloo haloo kama wanapigishana kelele na mtu, hata msikilizani, hakuna smooth connection na mazungumzo.

“Niwaombeni tuwape muda TCRA wakati wakitafuta ufumbuzi, wakati huo tupate huduma lakini zilizo bora, ni jambo linazungumzika.

“Tuondoe hii habari ya sisi wanyonge, sisi wanyonge, inatulemaza, nataka niwaombe, tuondoke katika baadhi ya mambo, ukiambiwa tulipo na tunakotaka kwenda inahitaji muujiza wa ajabu sana…”
 
Mbona kipindi cha marehemu hakusema hiyo kauli ni mbaya?
Mkuu umesahau kua mwendazake amejivika cheo cha izilaili.

Waislam wanasema ukiona mtu anafanya kitu kibaya hatua ya kwanza mkataze kwa mdomo,kama huwezi hatua ya pili tumia nguvu zako,kama humuwezi tena hatua ya 3 na mwisho chukia lile tukio na mchukie na anaetenda.

Kipindi cha mwendazake watu wengi walibaki kwenye kuchukia maana hawakua na ubavu tena.ukithubutu kwa hatua yoyote unaweza kunyofolewa roho.

Hivyo mkuu usimulaumu mtu kwa kutoongea kitu kwa wakati ule.
 
Inaweza kuondoka endapo kutakuwa na usawa kati ya wenye nacho na wasio nacho. Kama kuna matabaka, neno 'wanyonge' haliwezi kuondoka. Kama kuna tofauti ya maskini na tajiri, wanyonge watakuwepo tu.
Zab 41:1 Heri amkumbukaye mnyonge; Bwana atamwokoa siku ya taabu.

Mnyonge ni mtu anayetamani kutendewa haki pasipo masharti, lakini hana uwezo. Leo hii kwenye mitandao wanakata salio kablaa hata halijatumika, wanyonge watakosaje kuwepo?
 
Hu
Hii ni sehemu ya nukuu ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akizungumzia marekebisho ya Kanuni ya Maudhui ya Mitandao ya Mwaka 2020, leo Machi 14, 2022. Msome kisha uniambie tuitafakari hii kauli ya WANYONGE.

Watanzania wameanza kuwa wanaongea barabarani wakiongea na simu haloo haloo kama wanapigishana kelele na mtu, hata msikilizani, hakuna smooth connection na mazungumzo.

“Niwaombeni tuwape muda TCRA wakati wakitafuta ufumbuzi, wakati huo tupate huduma lakini zilizo bora, ni jambo linazungumzika.

“Tuondoe hii habari ya sisi wanyonge, sisi wanyonge, inatulemaza, nataka niwaombe, tuondoke katika baadhi ya mambo, ukiambiwa tulipo na tunakotaka kwenda inahitaji muujiza wa ajabu sana…”
Yo ni.mjinga tu!

Yupo kujiosha lakini hana usafi wowote! Anakauli za ajabu ajabunkama Gori la mkono!

Na alifungia bunge live! Anajifanya kimkosoa Magufuli lakini hakuna hata chembe anaweza kumfikia kwa utendaji!

Kwa vile mama Samia anapenda watu kama huyu wanaomtukana kila siku Magufuli huku bibi ushungi anashangiria! Hajui kuwa siku zinaenda hazigandi!
 
Amwambie bosi wake kwanza anaesisitiza mikopo ya bei nafuu ndio kila kitu, bosi akiachana na mentality ya kinyonge ndio mambo mengine yataendelea vizuri.
 
Na yeye waziri wangu apunguze kulitaja Jina la Rais kwa kila kitu, amelitaja Jina la Rais zaidi ya mara 20 kwenye Ile press conference na hii inaonyesha kutojiamini na unafiki aliokua nao waziri Nape, ni serikali ya CCM ndio iliyofanya hayo SIO president Samia.
 
Nape yupo sahihi. Mtu akikuita mnyonge, anakuwa amekufukarisha. Wazungu wanasema..you have been disempowered!
Hii kauli ya wanyonge ilikuwa ni kuwadanganya watu na kuwatumia kisiasa.
Hata kama sina kitu...usiniite mnyonge kamwe!

Kipi bora kati ya kuitwa maskini au mnyonge?

Kwasababu kwa upande wangu naamini mtu mnyonge ni yule mwenye uwezo wa kutenda au kuamua jambo fulani;lakini hana uwezo wa kutenda kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake.

Hao wazungu wanatuita nchi maskini. Na umaskini asilimia kubwa ni matokeo ya uvivu au ukosefu wa maarifa.
 
Huyu yupo kwenye crusade ya kumdiscredit JPM kila fursa anayopata anamkandia. Sisi tunamcheki tunasema hiiiii!
Ila mkuu, hoja ina ukweli. Ni hakusema mbele ya Mwenda sababu inajulikana. Funika kombe mwanaharamu apite. Kuna pia waliotumikia kafiri...
 
Hii ni sehemu ya nukuu ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akizungumzia marekebisho ya Kanuni ya Maudhui ya Mitandao ya Mwaka 2020, leo Machi 14, 2022. Msome kisha uniambie tuitafakari hii kauli ya WANYONGE.

Watanzania wameanza kuwa wanaongea barabarani wakiongea na simu haloo haloo kama wanapigishana kelele na mtu, hata msikilizani, hakuna smooth connection na mazungumzo.

“Niwaombeni tuwape muda TCRA wakati wakitafuta ufumbuzi, wakati huo tupate huduma lakini zilizo bora, ni jambo linazungumzika.

“Tuondoe hii habari ya sisi wanyonge, sisi wanyonge, inatulemaza, nataka niwaombe, tuondoke katika baadhi ya mambo, ukiambiwa tulipo na tunakotaka kwenda inahitaji muujiza wa ajabu sana…”
Mambo ya wanyonge aliyaleta magufuli kuwadanganya Ili awaibie bahati nzuri mungu akamuwahi
 
Inaweza kuondoka endapo kutakuwa na usawa kati ya wenye nacho na wasio nacho. Kama kuna matabaka, neno 'wanyonge' haliwezi kuondoka. Kama kuna tofauti ya maskini na tajiri, wanyonge watakuwepo tu.
Zab 41:1 Heri amkumbukaye mnyonge; Bwana atamwokoa siku ya taabu.

Mnyonge ni mtu anayetamani kutendewa haki pasipo masharti, lakini hana uwezo. Leo hii kwenye mitandao wanakata salio kablaa hata halijatumika, wanyonge watakosaje kuwepo?
Achaa theories za kijima daima kutakuwa na gap ya kiuchumi si lazima lied na masikini,
 
Inaweza kuondoka endapo kutakuwa na usawa kati ya wenye nacho na wasio nacho. Kama kuna matabaka, neno 'wanyonge' haliwezi kuondoka. Kama kuna tofauti ya maskini na tajiri, wanyonge watakuwepo tu.
Zab 41:1 Heri amkumbukaye mnyonge; Bwana atamwokoa siku ya taabu.

Mnyonge ni mtu anayetamani kutendewa haki pasipo masharti, lakini hana uwezo. Leo hii kwenye mitandao wanakata salio kablaa hata halijatumika, wanyonge watakosaje kuwepo?
Wanakata salio kabla haijatumika?? huo ni wizi, hili lisisubiri serikali watu wanaweza kushtaki hayo makampuni na hata kutumia pressure ya wabunge wao wanaweza kubadilisha huu wizi
 
Hu

Yo ni.mjinga tu! Yupo kujiosha lakini hana usafi wowote! Anakauli za ajabu ajabunkama Gori la mkono! Na alifungia bunge live! Anajifanya kimkosoa Magufuli lakini hakuna hata chembe anaweza kumfikia kwa utendaji! Kwa vile mama Samia anapenda watu kama huyu wanaomtukana kila siku Magufuli huku bibi ushungi anashangiria! Hajui kuwa siku zinaenda hazigandi!
Mama hataki rohombaya ana afadhali
 
Back
Top Bottom