Nape Nnauye: Tuachane na hii habari ya "Sisi Wanyonge", kauli hiyo inatulemaza

Nape Nnauye: Tuachane na hii habari ya "Sisi Wanyonge", kauli hiyo inatulemaza

Sio km kunq ttZo na kujiita mnyonge km ww ni mpumbavu why usijiite mpumbavu na km ww ni mnyonge bas jiite mnyonge ni haki yako kulingana na katiba
 
Kamwe usije niita mnyonge, jiite wawe na familia yako au na wale wenye imani kama yako. So jiwe alipokuwa anawaita kuwa nyie ni wanyonge alikuwa anamaanisha nyie ni wanyonge kwa sababu za uchaguzi wa 2020 ambao hata wew wajua alichofanya?
Unatumia jina ambalo siyo lako hapa JF kwasababu unaogopa wakubwa
 
Unatumia jina ambalo siyo lako hapa JF kwasababu unaogopa wakubwa
Nani kasema siyo langu? Au kila mtu humu lazima atumie jina fake? Ok hao so called "wakubwa" niwaogope kwa sababu gani au kipi kibaya nichopost mpaka niogope?
 
Hii ni sehemu ya nukuu ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akizungumzia marekebisho ya Kanuni ya Maudhui ya Mitandao ya Mwaka 2020, leo Machi 14, 2022. Msome kisha uniambie tuitafakari hii kauli ya WANYONGE.

Watanzania wameanza kuwa wanaongea barabarani wakiongea na simu haloo haloo kama wanapigishana kelele na mtu, hata msikilizani, hakuna smooth connection na mazungumzo.

“Niwaombeni tuwape muda TCRA wakati wakitafuta ufumbuzi, wakati huo tupate huduma lakini zilizo bora, ni jambo linazungumzika.

“Tuondoe hii habari ya sisi wanyonge, sisi wanyonge, inatulemaza, nataka niwaombe, tuondoke katika baadhi ya mambo, ukiambiwa tulipo na tunakotaka kwenda inahitaji muujiza wa ajabu sana…”
Naunga mkono hoja.
Kukubali kuitwa mnyonge ni kuidhalilisha nafsi yako. Mungu aliumba binadamu mkamilifu mwenye nguvu za mwili na ubongo.

Yeyote akizitumia akili zake na nguvu zake vizuri ana uwezo wa kupiga hatua kiuchumi na kijamii.

Usikubali kuitwa Mnyonge, utapata LAANA kama aliyoondoka nayo Mwendazake
 
Probably wewe hukuwemo kwenye hiyo list ya wanyonge ya jiwe. Siyo wote ni wanyonge, na alipokuwa akisema anawetetea wanyonge hakuwa ana include watu kama akina Azam, MODewji au wewe. Chuki dhidi ya Magufuli hazina faida yoyote sasa kwani zinaweza kusababisha mtu afanye maamuzi mabaya ili tu kuyafanya yawe ni tofauti na ya Magufuli.
Acha kutetea upumbavu, hakuna mnyonge hapa. Magufuli aliwafanya mtaji wa kuendeleza UDIKTETA wake, na nyinyi mukaanza kumuita mungu.

Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu!! (Yeremia 17:5)
 
Nape yupo sahihi. Mtu akikuita mnyonge, anakuwa amekufukarisha. Wazungu wanasema..you have been disempowered!
Hii kauli ya wanyonge ilikuwa ni kuwadanganya watu na kuwatumia kisiasa.
Hata kama sina kitu...usiniite mnyonge kamwe!
Hivi serikali inapoamua kwa makusudia kukuibia pesa yako hata iwe senti moja bila ridhaa yako kwa kisingizio cha tozo na tumelalamika wakajibu lazima watachukua na kweli wanachukua je huo sio unyonge? Haijapata kutokea katika awamu zilizopita kufanyiwa kitu Kama hiki, tu kwa vile wameshika mpini na tukiandama tutapigwa je huu si unyonge? Au tuutaje?
 
Acha kutetea upumbavu, hakuna mnyonge hapa. Magufuli aliwafanya mtaji wa kuendeleza UDIKTETA wake, na nyinyi mukaanza kumuita mungu.

Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu!! (Yeremia 17:5)
Well hata Moses Nnauye na Julius Nyerere nao walitufundisha kuwachukia mabeberu wasituonee wanyonge.
 
Back
Top Bottom