Nape Nnauye: Tuhangaike kujenga mifumo imara na siyo kutumainia mtu mmoja

Hii hoja ya kuongezewa mda haina mantiki yoyote Wala haijengi zaidi inabomoa, muhimu kutengeneza mfumo ambao utaendelea kukuza taifa hata akitawala kiongozi mwingine, Hawa wanao taka aongezewe mda ni wanao tetea matumbo yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nape apongezwe na nani, hapa baadhi ya watu wanasifu alichoongea maana ni ajabu kwa mnafiki kama yeye kuongea kinyume na lugha za kumtukuza yesu wa ccm.
Mkuu tindo Nape japo aliomba msamaha na sasa akarudi kwenye kundi la ''kuabudu'' lakini rohoni hajakaa sawa na anajua kabisa huyu jamaa uongozi hauwezi. Ni kwamba hana namna tu ya kufanya kwani aliyeshika makali ni bwana yule. Hata Kinana. Ilkuwa tu hamna jinsi. Kifupi ni kuwa CCM kuna watu wengi tu wanaugulia chini chini ila ''ukichaa'' wa bwana yule ndiyo unawafanya wakae kimya. Na mbaya zaidi wanajua wananchi wa Tanzania ni watu wasio na msaada kama watakwenda against mungu mtu. Listi iko ndefu hata kina Makamba J wako ndani. Kufanya mambo kuwa mabaya zaidi wanajua mungu mtu akiendelea kuwepo eg kuongezewa muda ndiyo maangamizi yao kwani anaonekana hana mpango nao kabisa.
 
Kwa mtu duni kama wewe kutumia nembo ya Taifa ni matusi kwa raia wa Tanzania , nachukua nafasi nafasi hii kuiomba JF ipige marufuku hiyo nembo kutumiwa na wajinga
Wewe bado unamsoma huyu jamaa? Mimi nilishamuweka kwenye listi ya watu ninawa-ignore na chochote anachoandika sikioni.
 
Kwa mtu duni kama wewe kutumia nembo ya Taifa ni matusi kwa raia wa Tanzania , nachukua nafasi nafasi hii kuiomba JF ipige marufuku hiyo nembo kutumiwa na wajinga
Endelea kuosha vyombo na kusafisha nyumba ya Lema akija akukute na kabendi akutoe baru
 
Mchanganyiko wa pumba na mchele kwenye andiko. Ujumbe ni kwamba tujenge mifumo bora na sio kumtegemea mtu mmoja ambaye ukiangalia style yake ya uongozi pia ina mapungufu mengi
Mifumo ni tatizo pamoja na deficiency skills za wasimamiaji wenyewe.

Ni Nape akiwa kama mwanakamati wa bunge wa maswala ardhi alitoka hadharani akatuambia NHC pako safi baada ya kukagua mradi wao kinondoni sikuchache baadae mkurugenzi akatumbuliwa kwa sababu shirika halina cashflow pamoja na kukopewa zaidi ya trillion shillings with government guarantee.

Kamati za bunge zinapewa kila aina ya mtaalamu kuwasaidia kuelewa nyenzo wanazopewa kwenye kazi yao ya kuisimamia serikali.

Pamoja na mfumo imara kazi iliwashinda mbona? Sasa hapo tatizo lilikuwa mfumo au competent skills za Nape mwenyewe.

Kuna issue nyingi sana zaidi ya mfumo kama watu wangekuwa wana weledi wa kazi kutokana na mifumo iliyopo huko serikalini pamoja na mapungufu yake sasa hivi attitude zingekuwa zimebadilika kwa sehemu kubwa sio kwa sehemu ndogo ndani ya miaka mitano.

Jaffo kila anapokutana na madudu chanzo utakuta watu awajafuata mfumo wa manunuzi au usimamizi; ina maana underlying issue watu wanaotakiwa kuisimamia hiyo mifumo pia ni issue in other words working culture ya serikali bado ni tatizo.

Siamini kama hakuna mwingine zaidi ya Magufuli Ila ni wakati sasa mawaziri mpaka wenye viti wa mitaa waonyeshe consistent kwenye kutekeleza majukumu yao hivyo ndio mfumo unavyofanya kazi, sio variation kila sehemu wakati wote wanatumia policy approaches za wizara.

Matokeo yake kila anapofika kiongozi mahala ni malalamiko anatakiwa afanye trouble shooting kisa adverse attitude za wafanyakazi; watu kama hao ata ukiwawekea mfumo unaotumika mbinguni awawezi timiza wajibu because they’re just not committed to changing wao wenyewe.
 
Ndugu Nape alipohojiwa kuhusu vuguvugu la kumuongezea Rais Magufuli muda wa utawala wake amesema haya yafuatayo.

1. Kwanza anashangazwa na kwamba ndiyo kwanza miaka mitano ya muhula wa pili wa utawala wa Rais Magufuli umeanza halafu watu wanaanza kuzungumza ya baadae, wakati haya waliyoomba kura kwayo hawajayamaliza.

2. Pili anashangazwa na watu wanaowaza utadhani wana ahadi na Mwenyezi Mungu kuhusu kujua nani atakuwepo kesho na nani hatakuwepo.

3. Anasema, Kilicho cha msingi ni kujenga mifumo imara ili hiyo mifumo iweze kulinda mafanikio yaliyopatikana na tusigeuze mtu kuwa ndo mafanikio yenyewe maana watu huja na kuondoka na Mungu ndo anapanga uhai wa watu.

MY TAKE
Msimamo wa Nape ni msimamo mzuri, wanaotaka Magufuli abaki madarakani kinyume cha katiba ya sasa hao wanajali maslahi yao binafsi na si ya nchi yetu. hawana tofauti na wale ambao Nyerere alisema kila alipotaka kung'atuka walimwambia Mzee endelea bila wewe nchi itayumba kumbe ikaja kugundulika walikuwa wanajali matumbo yao binafsi, walikuwa hawana uhakika kuwa akitoka madarakani basi Rais ajaye atawalindia nyadhifa zao!

Msikilize wewe mwenyewe hapa:

View attachment 1697614

MSIMAMO WA RAIS MAGUFULI KUHUSU KUONGEZA MUDA NI HUU HAPA CHINI

View attachment 1697758
.
 
Hoja namba 2 na 3 nimeshaziandika sana hapa.
Mkuu kwa iyo unaamini Mungu yupo? Kwasababu hoja namba mbili 'Pili anashangazwa na watu wanaowaza utadhani wana ahadi na Mwenyezi Mungu'.

Hongera sana mkuu kwa kukubali uwepo wa Mungu.

Ubarikiwe hadi ushangae.
 
Nape CCM yenu ishawatema hamna chenu... yaani wewe na wenzako ni kama sisi tu...uliopokonywa form za uteuzi njiani.

tena shukuru mno bila kupiga magoti hata hako ka ubunge ungekasikia kwa radio.
Duuuuuh hatareeeh sana.
 
Nimekosa cha kuandika kwa kweli. Nakuwa mtazamaji tyuuh.
 
Ndugu Nape alipohojiwa kuhusu vuguvugu la kumuongezea Rais Magufuli muda wa utawala wake amesema haya yafuatayo.

1. Kwanza anashangazwa na kwamba ndiyo kwanza miaka mitano ya muhula wa pili wa utawala wa Rais Magufuli umeanza halafu watu wanaanza kuzungumza ya baadae, wakati haya waliyoomba kura kwayo hawajayamaliza.

2. Pili anashangazwa na watu wanaowaza utadhani wana ahadi na Mwenyezi Mungu kuhusu kujua nani atakuwepo kesho na nani hatakuwepo.

3. Anasema, Kilicho cha msingi ni kujenga mifumo imara ili hiyo mifumo iweze kulinda mafanikio yaliyopatikana na tusigeuze mtu kuwa ndo mafanikio yenyewe maana watu huja na kuondoka na Mungu ndo anapanga uhai wa watu.

MY TAKE
Msimamo wa Nape ni msimamo mzuri, wanaotaka Magufuli abaki madarakani kinyume cha katiba ya sasa hao wanajali maslahi yao binafsi na si ya nchi yetu. hawana tofauti na wale ambao Nyerere alisema kila alipotaka kung'atuka walimwambia Mzee endelea bila wewe nchi itayumba kumbe ikaja kugundulika walikuwa wanajali matumbo yao binafsi, walikuwa hawana uhakika kuwa akitoka madarakani basi Rais ajaye atawalindia nyadhifa zao!

Msikilize wewe mwenyewe hapa:

View attachment 1697614

MSIMAMO WA RAIS MAGUFULI KUHUSU KUONGEZA MUDA NI HUU HAPA CHINI

View attachment 1697758
Ndugu Nape alipohojiwa kuhusu vuguvugu la kumuongezea Rais Magufuli muda wa utawala wake amesema haya yafuatayo.

1. Kwanza anashangazwa na kwamba ndiyo kwanza miaka mitano ya muhula wa pili wa utawala wa Rais Magufuli umeanza halafu watu wanaanza kuzungumza ya baadae, wakati haya waliyoomba kura kwayo hawajayamaliza.

2. Pili anashangazwa na watu wanaowaza utadhani wana ahadi na Mwenyezi Mungu kuhusu kujua nani atakuwepo kesho na nani hatakuwepo.

3. Anasema, Kilicho cha msingi ni kujenga mifumo imara ili hiyo mifumo iweze kulinda mafanikio yaliyopatikana na tusigeuze mtu kuwa ndo mafanikio yenyewe maana watu huja na kuondoka na Mungu ndo anapanga uhai wa watu.

MY TAKE
Msimamo wa Nape ni msimamo mzuri, wanaotaka Magufuli abaki madarakani kinyume cha katiba ya sasa hao wanajali maslahi yao binafsi na si ya nchi yetu. hawana tofauti na wale ambao Nyerere alisema kila alipotaka kung'atuka walimwambia Mzee endelea bila wewe nchi itayumba kumbe ikaja kugundulika walikuwa wanajali matumbo yao binafsi, walikuwa hawana uhakika kuwa akitoka madarakani basi Rais ajaye atawalindia nyadhifa zao!

Msikilize wewe mwenyewe hapa:

View attachment 1697614

MSIMAMO WA RAIS MAGUFULI KUHUSU KUONGEZA MUDA NI HUU HAPA CHINI

View attachment 1697758
Hii ni moja ya hoja nzito na yenye mashiko tangu bunge linaloendelea lianze,nchi ikiwa na mifumo imara na inayoeleweka Taifa haliwezi kuwa na hofu na yajayo.
 
Back
Top Bottom