Nape Nnauye: Tuhangaike kujenga mifumo imara na siyo kutumainia mtu mmoja

Ndugu Nape alipohojiwa kuhusu vuguvugu la kumuongezea Rais Magufuli muda wa utawala wake amesema haya yafuatayo.

1. Kwanza anashangazwa na kwamba ndiyo kwanza miaka mitano ya muhula wa pili wa utawala wa Rais Magufuli umeanza halafu watu wanaanza kuzungumza ya baadae, wakati haya waliyoomba kura kwayo hawajayamaliza.

2. Pili anashangazwa na watu wanaowaza utadhani wana ahadi na Mwenyezi Mungu kuhusu kujua nani atakuwepo kesho na nani hatakuwepo.

3. Anasema, Kilicho cha msingi ni kujenga mifumo imara ili hiyo mifumo iweze kulinda mafanikio yaliyopatikana na tusigeuze mtu kuwa ndo mafanikio yenyewe maana watu huja na kuondoka na Mungu ndo anapanga uhai wa watu.

MY TAKE
Msimamo wa Nape ni msimamo mzuri, wanaotaka Magufuli abaki madarakani kinyume cha katiba ya sasa hao wanajali maslahi yao binafsi na si ya nchi yetu. hawana tofauti na wale ambao Nyerere alisema kila alipotaka kung'atuka walimwambia Mzee endelea bila wewe nchi itayumba kumbe ikaja kugundulika walikuwa wanajali matumbo yao binafsi, walikuwa hawana uhakika kuwa akitoka madarakani basi Rais ajaye atawalindia nyadhifa zao!

Msikilize wewe mwenyewe hapa:

View attachment 1697614

MSIMAMO WA RAIS MAGUFULI KUHUSU KUONGEZA MUDA NI HUU HAPA CHINI

View attachment 1697758

Tatizo wanasiasa ni vigeugeu leo anaongea maneno ya busara kesho anakuja kuongea utumbo kwa jambo hilo hilo.
 
Hizo fine zenyewe unajua utozwaji wake?

Mwenyekiti hatozi fine ndugu, yeye nikupeleka lalamiko/tukio kwa Afisa Afya Kata kisha Afisa Afya anaandika fine ili huyu mtuhumiwa aende mwenyewe Manispaa kulipia kwasababu kwenye Kata hakuna POS.

Unajua nini kinafuata? Afisa Mazingira wa Manispaa Mwanasheria akiona dodo zuri tena saa sita anakula mkwaju na anaupa nauli.

Ahahahah afu ukikutana naye kesho yake anakusonya!

Yaani utakata tamaa mpaka basi,matokeo yake na we utageuka mla rushwa ambaye ndani ya siku kadhaa utachezea midomoni mwa TAKUKURU ambao wanawinda kama radi iwindavyo ng'ombe na pembe zake.

Na hivi posho ya wenyeviti ni elfu 50 kwa mwezi..utajikuta wife anazaa watoto hata sura zao huzijui ndo utajua kwanini Nazi humtangulia mkwezi.
Ameongea ukweli sio sahihi kumtegemea mtu mmoja, tatizo lenyewe tunaenda mwaka wa sita culture ya ufanyaji kazi serikalini aijabadilika pamoja na kwamba amejaribu kuwaacha wakurugenzi na wakuu wa wilaya/mikoa wale wale ulitegemea by now wawe na experience ndio kwanza ata kusimamia miradi yao shida.

Wizarani wataalamu pia awajabadilishwa ovyo lakini bado hakuna consitent serikalini matatizo aliyoyakuta mpaka leo yapo kwa percent kubwa inabidi aanze trouble shooting kila mara anaposimama kukutana na wananchi mpaka yeye mwenyewe anajiuliza kazi za watu wengine serikalini ni nini kama kila anapofika ni yeye ndio atupiwe shida.

Mtu pekee anaelekea kuweza kuendesha wizara aliyokabidhiwa ni Dr Gwajima ila apunguze mapepe. Huyo mrithi wa Magufuli given the social contexts za jamii yetu aonekani.

Hao mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya; raisi akinyuti na wao uwaoni tena kwenye camera mpaka aibuke.

Let’s face it ignorance is another major issue watanzania bado awajajua ku deal na consequences of their action ppl take life so easy in Tanzania; ningekuwa naishi mjini nikapata ata wenyekiti wa mtaa watu ndio wangeelewa I do not tolerate stupidity ukitupa taka mtaani unakula fine hapo hapo au nakupa fagio ufagie mtaa mzima.

In short serikali imejaza mapambo kwa majina ya wasimamizi wasio na managerial skills husika za kuendesha wizara yaani wewe waziri mpaka ufike site ndio ujue mradi upo 40% badala ya 90% kama ulivyoambiwa huna supervision matrix ya kila mradi na communication zako za watu chini je.

Akiondoka Magufuli tunarudi square 1 jumlisha na hizi pressure za wafanyakazi wa serikali atakaefuata akiendekeza kelele za hawa watu atakuta mapato yote anawapa wao kama mishahara na marupurupu; hana kinachobaki kwa ajili ya miradi ya kimkakati ya maendeleo.
 
Sidhani kama ni muda muafaka kuanza mjadala usio rasmi wa kutaka kumuongezea JPM ukomo wa uongozi wa Taifa letu.
Naona wenye uchu huo hawana ufahamu,wanadhani nchi hii inaongozwa na kichwa kimoja, nchi inaongozwa na mifumo tuliyojiwekea wenyewe.
Kama wanataka mabadiliko wadai katiba mpya ili twende kwenye referendum, huko ndiko kwenye wengi wape.
 
Hizo fine zenyewe unajua utozwaji wake?

Mwenyekiti hatozi fine ndugu, yeye nikupeleka lalamiko/tukio kwa Afisa Afya Kata kisha Afisa Afya anaandika fine ili huyu mtuhumiwa aende mwenyewe Manispaa kulipia kwasababu kwenye Kata hakuna POS.

Unajua nini kinafuata? Afisa Mazingira wa Manispaa Mwanasheria akiona dodo zuri tena saa sita anakula mkwaju na anaupa nauli.

Ahahahah afu ukikutana naye kesho yake anakusonya!

Yaani utakata tamaa mpaka basi,matokeo yake na we utageuka mla rushwa ambaye ndani ya siku kadhaa utachezea midomoni mwa TAKUKURU ambao wanawinda kama radi iwindavyo ng'ombe na pembe zake.

Na hivi posho ya wenyeviti ni elfu 50 kwa mwezi..utajikuta wife anazaa watoto hata sura zao huzijui ndo utajua kwanini Nazi humtangulia mkwezi.
Imebidi nicheke tu, imagine mtu anaanza kazi sehemu ya kupokea fines, halafu trainer mwenyewe ndio wewe na mtazamo wako si balaa hilo.

Yaani ni kama unamwambia uzalendo wako mjomba autakupeleka popote serikalini, bora ujifunze kukwepa viunzi vya TAKUKURU kama wenzako uendeshe maisha.
 
Ahahahaha hapana Mkuu, inakatisha tamaa sana! Afu utakuta huyo jamaa wa Manispaa anatembelea Vogi la maana kupitia juhudi zenu na kuanza kukuoneni ninyi visado tu!

Anyways tupambane kuijenga inchi, maana Ufalme wa Mungu u-waja!
 
CCM inaweza kuja kupasuka vipandevipande endapo huu upuuzi wakaufanyia kazi. Natamani itokee na iwe kweli ili tushirikiane kupambana na mkoloni mweusi

Haitokaa itokee......chawa hawawezi kumpinga bosi wao km atataka iwe ivo
 
Ameongea ukweli sio sahihi kumtegemea mtu mmoja, tatizo lenyewe tunaenda mwaka wa sita culture ya ufanyaji kazi serikalini aijabadilika pamoja na kwamba amejaribu kuwaacha wakurugenzi na wakuu wa wilaya/mikoa wale wale ulitegemea by now wawe na experience ndio kwanza ata kusimamia miradi yao shida.

Wizarani wataalamu pia awajabadilishwa ovyo lakini bado hakuna consitent serikalini matatizo aliyoyakuta mpaka leo yapo kwa percent kubwa inabidi aanze trouble shooting kila mara anaposimama kukutana na wananchi mpaka yeye mwenyewe anajiuliza kazi za watu wengine serikalini ni nini kama kila anapofika ni yeye ndio atupiwe shida.

Mtu pekee anaelekea kuweza kuendesha wizara aliyokabidhiwa ni Dr Gwajima ila apunguze mapepe. Huyo mrithi wa Magufuli given the social contexts za jamii yetu aonekani.

Hao mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya; raisi akinyuti na wao uwaoni tena kwenye camera mpaka aibuke.

Let’s face it ignorance is another major issue watanzania bado awajajua ku deal na consequences of their action ppl take life so easy in Tanzania; ningekuwa naishi mjini nikapata ata wenyekiti wa mtaa watu ndio wangeelewa I do not tolerate stupidity ukitupa taka mtaani unakula fine hapo hapo au nakupa fagio ufagie mtaa mzima.

In short serikali imejaza mapambo kwa majina ya wasimamizi wasio na managerial skills husika za kuendesha wizara yaani wewe waziri mpaka ufike site ndio ujue mradi upo 40% badala ya 90% kama ulivyoambiwa huna supervision matrix ya kila mradi na communication zako za watu chini je.

Akiondoka Magufuli tunarudi square 1 jumlisha na hizi pressure za wafanyakazi wa serikali atakaefuata akiendekeza kelele za hawa watu atakuta mapato yote anawapa wao kama mishahara na marupurupu; hana kinachobaki kwa ajili ya miradi ya kimkakati ya maendeleo.

Gwajima nae yupo kwenye genge la wanafiki hastahili hizo sifa.
 
Hakuna tofauti kubwa ya ufanisi kati ya huyu na watangulizi wake. Ubunifu pekee alionao ni vitisho na kupambana na watoa habari. Rais ajaye akitokea kambi tofauti, itabidi kupanua magereza zetu kukabiliana na waliotenda makosa chini ya utawala huu.
Japo ni ngumu kutokea kambi pinzani kutokana na mifumo iliyopo , ila hata huyo atakayetokea kambi kuu ana kazi nzito ya kulipa madeni makubwa ya nje na kurudisha umoja wa Watz.
 
Nape, miaka ya nyumba ukiwa Mjumbe wa vikao vikubwa ndani ya CCM, je ulishindwaje kuwasisitiza wajumbe kujenga mfumo wa kitaasisi badala ya kumpanda mtu mmoja mmoja? leo ndiyo unaiona hoja hii ya CDM kuwa ina mshiko? kwa nini leo? funguka zaidi?
 
Hoja ya chadema ipi tena hapo?
 
MY TAKE
Msimamo wa Nape ni msimamo mzuri, wanaotaka Magufuli abaki madarakani kinyume cha katiba ya sasa hao wanajali maslahi yao binafsi na si ya nchi yetu. hawana tofauti na wale ambao Nyerere alisema kila alipotaka kung'atuka walimwambia Mzee endelea bila wewe nchi itayumba kumbe ikaja kugundulika walikuwa wanajali matumbo yao binafsi, walikuwa hawana uhakika kuwa akitoka madarakani basi Rais ajaye atawalindia nyadhifa zao!
Na yeye ni miongoni mwa chanzo cha matatizo tunayokumbana nayo, ajifunze kuwa mkuki huuma kwa binadamu kama kwa nguruwe
 
Matukio ya hivi karibuni ya kisiasa inatuwia vigumu kuwaamini wanasiasa na kauli zao.......
 
Japo ni ngumu kutokea kambi pinzani kutokana na mifumo iliyopo , ila hata huyo atakayetokea kambi kuu ana kazi nzito ya kulipa madeni makubwa ya nje na kurudisha umoja wa Watz.
Kuna haja ya kufanya marekebisho ya Sheria ili hata kama rais awe impeached hata kama kamaliza muda wake ili awajibike na uhalifu alioufanya akiwa madarakani.
 
Ndugu Nape alipohojiwa kuhusu vuguvugu la kumuongezea Rais Magufuli muda wa utawala wake amesema haya yafuatayo.

1. Kwanza anashangazwa na kwamba ndiyo kwanza miaka mitano ya muhula wa pili wa utawala wa Rais Magufuli umeanza halafu watu wanaanza kuzungumza ya baadae, wakati haya waliyoomba kura kwayo hawajayamaliza.

2. Pili anashangazwa na watu wanaowaza utadhani wana ahadi na Mwenyezi Mungu kuhusu kujua nani atakuwepo kesho na nani hatakuwepo.

3. Anasema, Kilicho cha msingi ni kujenga mifumo imara ili hiyo mifumo iweze kulinda mafanikio yaliyopatikana na tusigeuze mtu kuwa ndo mafanikio yenyewe maana watu huja na kuondoka na Mungu ndo anapanga uhai wa watu.

MY TAKE
Msimamo wa Nape ni msimamo mzuri, wanaotaka Magufuli abaki madarakani kinyume cha katiba ya sasa hao wanajali maslahi yao binafsi na si ya nchi yetu. hawana tofauti na wale ambao Nyerere alisema kila alipotaka kung'atuka walimwambia Mzee endelea bila wewe nchi itayumba kumbe ikaja kugundulika walikuwa wanajali matumbo yao binafsi, walikuwa hawana uhakika kuwa akitoka madarakani basi Rais ajaye atawalindia nyadhifa zao!

Msikilize wewe mwenyewe hapa:

View attachment 1697614

MSIMAMO WA RAIS MAGUFULI KUHUSU KUONGEZA MUDA NI HUU HAPA CHINI

View attachment 1697758
Kuna watu wananufaika na huu utawala na ndiyo maana wanajaribu kutaka katiba ibadilishwe ili Magufuri atawale milele
 
Huyu waziri mollel anahangaika nini na kitochi chake waziri mzma anatumia kitochi
 
Nchi sio mtu,Kama aliondoka Mwalimu na pengo lake limezibwa aje nani mwingine asiyezibika ukitoka tu unasaulika
 
Back
Top Bottom