Nape Nnauye: Tuhangaike kujenga mifumo imara na siyo kutumainia mtu mmoja


Tatizo wanasiasa ni vigeugeu leo anaongea maneno ya busara kesho anakuja kuongea utumbo kwa jambo hilo hilo.
 
Hizo fine zenyewe unajua utozwaji wake?

Mwenyekiti hatozi fine ndugu, yeye nikupeleka lalamiko/tukio kwa Afisa Afya Kata kisha Afisa Afya anaandika fine ili huyu mtuhumiwa aende mwenyewe Manispaa kulipia kwasababu kwenye Kata hakuna POS.

Unajua nini kinafuata? Afisa Mazingira wa Manispaa Mwanasheria akiona dodo zuri tena saa sita anakula mkwaju na anaupa nauli.

Ahahahah afu ukikutana naye kesho yake anakusonya!

Yaani utakata tamaa mpaka basi,matokeo yake na we utageuka mla rushwa ambaye ndani ya siku kadhaa utachezea midomoni mwa TAKUKURU ambao wanawinda kama radi iwindavyo ng'ombe na pembe zake.

Na hivi posho ya wenyeviti ni elfu 50 kwa mwezi..utajikuta wife anazaa watoto hata sura zao huzijui ndo utajua kwanini Nazi humtangulia mkwezi.
 
Sidhani kama ni muda muafaka kuanza mjadala usio rasmi wa kutaka kumuongezea JPM ukomo wa uongozi wa Taifa letu.
Naona wenye uchu huo hawana ufahamu,wanadhani nchi hii inaongozwa na kichwa kimoja, nchi inaongozwa na mifumo tuliyojiwekea wenyewe.
Kama wanataka mabadiliko wadai katiba mpya ili twende kwenye referendum, huko ndiko kwenye wengi wape.
 
Imebidi nicheke tu, imagine mtu anaanza kazi sehemu ya kupokea fines, halafu trainer mwenyewe ndio wewe na mtazamo wako si balaa hilo.

Yaani ni kama unamwambia uzalendo wako mjomba autakupeleka popote serikalini, bora ujifunze kukwepa viunzi vya TAKUKURU kama wenzako uendeshe maisha.
 
Ahahahaha hapana Mkuu, inakatisha tamaa sana! Afu utakuta huyo jamaa wa Manispaa anatembelea Vogi la maana kupitia juhudi zenu na kuanza kukuoneni ninyi visado tu!

Anyways tupambane kuijenga inchi, maana Ufalme wa Mungu u-waja!
 
CCM inaweza kuja kupasuka vipandevipande endapo huu upuuzi wakaufanyia kazi. Natamani itokee na iwe kweli ili tushirikiane kupambana na mkoloni mweusi

Haitokaa itokee......chawa hawawezi kumpinga bosi wao km atataka iwe ivo
 

Gwajima nae yupo kwenye genge la wanafiki hastahili hizo sifa.
 
Hakuna tofauti kubwa ya ufanisi kati ya huyu na watangulizi wake. Ubunifu pekee alionao ni vitisho na kupambana na watoa habari. Rais ajaye akitokea kambi tofauti, itabidi kupanua magereza zetu kukabiliana na waliotenda makosa chini ya utawala huu.
Japo ni ngumu kutokea kambi pinzani kutokana na mifumo iliyopo , ila hata huyo atakayetokea kambi kuu ana kazi nzito ya kulipa madeni makubwa ya nje na kurudisha umoja wa Watz.
 
Nape, miaka ya nyumba ukiwa Mjumbe wa vikao vikubwa ndani ya CCM, je ulishindwaje kuwasisitiza wajumbe kujenga mfumo wa kitaasisi badala ya kumpanda mtu mmoja mmoja? leo ndiyo unaiona hoja hii ya CDM kuwa ina mshiko? kwa nini leo? funguka zaidi?
 
Nape, miaka ya nyumba ukiwa Mjumbe wa vikao vikubwa ndani ya CCM, je ulishindwaje kuwasisitiza wajumbe kujenga mfumo wa kitaasisi badala ya kumpanda mtu mmoja mmoja? leo ndiyo unaiona hoja hii ya CDM kuwa ina mshiko? kwa nini leo? funguka zaidi?
Hoja ya chadema ipi tena hapo?
 
Na yeye ni miongoni mwa chanzo cha matatizo tunayokumbana nayo, ajifunze kuwa mkuki huuma kwa binadamu kama kwa nguruwe
 
Matukio ya hivi karibuni ya kisiasa inatuwia vigumu kuwaamini wanasiasa na kauli zao.......
 
Japo ni ngumu kutokea kambi pinzani kutokana na mifumo iliyopo , ila hata huyo atakayetokea kambi kuu ana kazi nzito ya kulipa madeni makubwa ya nje na kurudisha umoja wa Watz.
Kuna haja ya kufanya marekebisho ya Sheria ili hata kama rais awe impeached hata kama kamaliza muda wake ili awajibike na uhalifu alioufanya akiwa madarakani.
 
Kuna watu wananufaika na huu utawala na ndiyo maana wanajaribu kutaka katiba ibadilishwe ili Magufuri atawale milele
 
Huyu waziri mollel anahangaika nini na kitochi chake waziri mzma anatumia kitochi
 
Nchi sio mtu,Kama aliondoka Mwalimu na pengo lake limezibwa aje nani mwingine asiyezibika ukitoka tu unasaulika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…