Kwanza Mama hajagawa Bandari yoyote!, pili, sio kila anachosaini Mama she is the initiator!
Hilo jambo ni sahihi kabisa!, mimi naliunga mkono
Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?
Please!.
Ukiwa unafanya jambo jema, hata watu wapige kelele vipi, unashikilia msimamo.
Naendelea kusisitiza hili jambo ni zuri,
Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe. Je DPW Tunapigwa?
Duh...!.
P
Swala si kuangalia mama ni initiator au lah! Mama ni Rais wa nchi. Yupo kulinda maslahi ya nchi na si vinginevyo. Mama hamuwezi muondoa katika hii lawama wakati katika mkataba yeye mwenyewe kakubali kutoa bandari za Tanzania (Tanganyika).
Sikukatalii saana, make Urais huu wakati mwingine unakuwepo tu ukienda kinyume wanashughulika nawe. Yeye kama anaona maji yanamzidi ni heri tu anatangaza kujiuzuru, au akomae na uzalendo afe nao.
Ukisema mama hajagawa bandari ni ushabiki tu ndugu Pascal. Katika mkataba hakuna mahala popote panapoeleza Tanzania tutanufaika kivipi. Tukiuliza mnakalia kupinga.
Ebu leteni hapa majibu na makubaliano ya kisheria yanayoonesha Tanzania itafaidika kivipi katika huu mkataba si maneno tu.
Ndo maana hapa nasisitiza kagawa bandari zetu.
Swala la kusema Watanzania tukubali tunaposhindwa hili sikubaliani nalo. Watanzania tunaweza sana. Shida ni mfumo uliopo. Nchi hii imejengwa katika mfumo wa kujuana, kulindana, kupiga au kula fedha ya serikali kwa wachache wenye nafasi.
Mfumo huu ndo unao iuwa Tanzania na kuleta visingizio kwamba watanzania hatuwezi hivyo tukubali kusaidiwa.
Hakuna nchi itakayo iletea maendeleo nchi nyingine hata siku moja. Hilo watanzania msahau. Hii ni sawa unafamilia baada ya kushindwa kuendesha familia yako, basi unaomba jirani au mtu mwingine aje akuendeshee familia. Mke atakuwa si wako tena. Kama ni mwanamke akaomba msaada kwa mwanamke mwenzie mume atakuwa si wake tena.
Tulitoa reli tusaidiwe, tulitoa shirika la ndege, tukatoa hadi Tanzanite, ebu nieleze huko kusaidiwa kulileta manufaa gani?
Kwa nini tunapenda kukiri haraka kushindwa? Nchi hii inawatu wana nia nzuri sana na niwazalendo. Shida waliomo kwenye system hawataki kutoka. Ni Tanzania pekee mtu anasema anastaafu akiwa Katibu Mkuu wa Chama. Baadae mtu huyo huyo anarudi kwa mgongo wa Makamu mwenyekiti wa Chama. Nini maana ya kusitaafu?
Yaani watu ni wale wale, kama si wale wale ni watoto wao, au ndugu zao. Vyeo vinatolewa kwa kujuana. Hata hao wanao pewa vyeo unaweza jiuliza hata huyu? Ndiyo sababu mambo mengi na miradi mingi Tanzania inafanyika kwa mazoea kwani wahusika wao wanajali kupiga pesa kisa wanajuana na kutumika na wakubwa.
Hii nchi inahitaji kufumuliwa upya na kusukwa upya.