Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
"Sheria hii ya mwaka 2016 ambayo mimi niliisimamia nikiwa waziri, imelenga kuifanya tasnia ya habari kuwa taaluma, ukikosea tukuchukulie hatua wewe, na ndio maana tumesema tutoe leseni, najua kuna maneno mengi lakini tukifika hapo pakutoa leseni maana yake tuna uwezo wa kuichukua leseni yetu kwa huyu mtu mmoja ambaye amehusika kutengeneza stori ambayo ina matatizo, lakini chombo kikabaki salama, ni kama ilivyo hospitali, daktari akikosea, hatufungi hospitali, tunamshughulikia daktari hospitali inaendelea kufanya kazi, kimsingi hatuna mpango wakufungia chombo chochote cha habari lakini tuna mpango wa kushughulika na wale ambao wanatupeleka kwenye kutengeneza stori mbaya". Waziri Nape Nnauye