Nape: Sheria ya Habari inalenga kufungia mtu na sio chombo cha habari

Nape: Sheria ya Habari inalenga kufungia mtu na sio chombo cha habari

Shetani wako ndiye aliyezitaka hizo sheria Nape kama waziri hakuwa na namna.

Ndiyo maana hata mama alikuwa makamu wa rais lkn hakuwa na sauti hivi sasa anazifuta sheria za shetani
Sheria gani imefutwa wewe taahira?
 
Safi sana mhe waziri. Huu ndiyo uongozi Sasa. Siyo kama zile enzi za yule shetani mpenda shari.

Keep on going mhe tuko nyuma yako!
Sheria ilitungwa mwaka 2016 hiyo enzi za shetani utekelezaji wake ndiyo uo, Sheria iliyokuwa inataka kufingia chombo cha habari chote ilitungwa miaka ya 1970+
 
"Sheria hii ya mwaka 2016 ambayo mimi niliisimamia nikiwa waziri, imelenga kuifanya tasnia ya habari kuwa taaluma, ukikosea tukuchukulie hatua wewe, na ndio maana tumesema tutoe leseni, najua kuna maneno mengi lakini tukifika hapo pakutoa leseni maana yake tuna uwezo wa kuichukua leseni yetu kwa huyu mtu mmoja ambaye amehusika kutengeneza stori ambayo ina matatizo, lakini chombo kikabaki salama, ni kama ilivyo hospitali, daktari akikosea, hatufungi hospitali, tunamshughulikia daktari hospitali inaendelea kufanya kazi, kimsingi hatuna mpango wakufungia chombo chochote cha habari lakini tuna mpango wa kushughulika na wale ambao wanatupeleka kwenye kutengeneza stori mbaya". Waziri Nape Nnauye
no no si jambo la heri tunajua mnataka kuwamiliki waandishi wa habari na kuwatawala milele, habari au makala ni gazeti limeongea na si mtu. Very narrow and useless Nape, pole bado una akili za karne ya Liulo
 
Ameeleweka...

Siyo kama ilivyo sasa, Gigi money kakaacha uchi kwa mapenzi yake, kituo kizima kinafungiwa...
 
Back
Top Bottom