Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 143,138
- 288,731
Watashindwa vibaya sana !Uhuni huu unaendelea kukua, utaota pembe na kuzaa matunda. Majuto ni mjukuu. Wakati wa kuchukua hatua kuirekebisha nchi yetu na kudai nchi ni sasa.
Alianza na wapinzani, na wao hasa Mh. Lissu walituonya sana tena mapema kuwa huyu dikteta uchwa hataishia kwao (wapinzani) bali ataendelea kadiri tutakavyomruhusu. Leo hii, bila aibu wala woga (mwenyewe anaita kujiamini na ujasiri) tumeona jinsi aliyekuwa Waziri wake wa Habari saa 24 zilizopita, na mtetezi wake mashuhuri wa chama chao, mwasisi wa goli la mkono lililomweka hapo ngomeni alivyomfanyia. Sasa ole wenu mnaoendelea kumshabikia! Ole wenu ninyi mnaokaa kimya wakati mna nafasi na wajibu wa kutenda sasa hivi.
Ni aibu kubwa sana hii, sikudhani ningeishi kuona na kusikia nchi yangu ingefika hapa.
Tumeona na kuujua ubaya wa CCM kwa miongo kadhaa lakini kwa sasa hivi tunaona kiwango kipya kabisa cha uovu na dhuluma. Sasa basi tufanye haya mambo 3 kila mmoja kwa nafasi yake:-
1) Tukatae (udikteta, uonevu na kila aina ya dhuluma na kugawanywa).
2) Tuwapinge (ni haki yetu).
3) Ni wajibu wetu!
Na iwe hivyo kiongozi.Usiwe na wasi wasi mkuu. Huu ni mpango maalum. Unadhani jeuri ya Nape kupingana na Sizonje waziwazi inatokana na nini?
Kazi imeshaanza kufanyika kitambo sana, subiri matokeo.
Wala makombo hawachelewi,kama fisi vile !!Kuna wanasiasa ambao hawajachakachuliwa, wanasiasa hasaa, watu wanaofikiria siasa, wenye malengo ya kisiasa, wapambanaji mpaka tone la mwisho la damu yao, watu ambao maisha hayawezi kuendelea bila wao kuonekana, watu tunaowahitaji kama Nape Nnauye.
Ni watu tunaotumia nguvu nyingi sana kupambana nao wakiwa upande wa pili na kwa haki au kwa mbinu hatujawahi kuwashinda. Nasema hatujawahi kuwashinda maana bado hatujaingia ikulu.
Mhe. Mbowe, Nape is a worthy acquisition!
Sio mbaya tukiwa kama Barcelona, tukawa na Messi, Suarez
na Neymar.
Kama uliweza kumleta Lowasa basi hautashindwa kumleta Nape. Now is the time, we have enough advantage to bring him over, for him and for us. The equilibrium favours us and please don't wait for it to Change.
Investment yoyote itakayoingia kumleta Nape itarudi mara mia . WHY NOT? Ni kijana na ni moja kati ya wale government looking like material, usisahau ana fan base pia.
Mwenyekiti nakukubali, born town kitambo bado watu wanachungulia uchi wa ng'ombe huko Chato. Fanya kweli!
Haya mahaba ya upinzani kwa Nnape yanathihirisha kuwa upinzani huwa wana ugonjwa wa kusahau haraka sana.
Dr Slaa pamoja na kupigania chadema kutoka wabunge wawili hadi wabunge 20, Slaa alivunjwa mkono pamoja na mke wake kuharibiwa mimba wakiwa Arusha.
Mwisho wa Siku Dr Slaa alifukuzwa chadema dakika za mwisho na chama kuuziwa Chadema!!
Leo hii yote hayo chadema wamesahau wako bize kumuonea huruma Nape Nauye kada wa ccm!!
Swali la kujiuliza, tangu lini chadema na upinzani kwa ujumla wakaitakia mema CCM??
very true !"Nge akikosa chakula muda mrefu huanza kujitafuna mwenyewe" CCM itasambaratika muda si mrefu
Wewe umekula fresh gani?Wala makombo hawachelewi,kama fisi vile !!
Endeleeni kusema Wala makombo utajikuta umebaki pekeyako afu kadi zimeishaWala makombo hawachelewi,kama fisi vile !!
Hili halina mjadala lazima aweke cheti mezaniTunahitaji vyeti tu