narudia tena kwa hili la Nape, mawaziri wa CCM kaeni kimya! tena mkae kimya kabisa kama hamna uwezo wa kujiuzulu! ni aibu sana kujifanya mnamuonea huruma mwenzenu wakati leo mtajitokeza kwa wingi wakati wa kuapishwa!!
Mh Mwigulu Nchemba, ujasiri wako na uzalendo wako wa kuvaa skafu na Tai ya bendera ya Tz, ujasiri huu unaishia kwenye twitter pekee?
Mh January ujasiri wako ulioonyesha kwenye inshu ya viroba , uko wapi katika hili?
Mh Mwakyembe, unajisikiaje moyoni kwenda kukaa kwenye kiti cha Nape?
mawaziri wa CCM, kuna maisha baada ya uwaziri, katika hili kama mimi ningekuwa waziri ningejiuzulu nibaki na ubunge wangu!
acheni unafiki wa kuumia gizani na kushangilia gizani!!
mimi ni mtu ninayeichukia CCM kwa moyo wangu wote, kwa akili zangu zote, na kwa nguvu zangu zote, ni kweli nilikasirika sana Nape kupewa wizara ya habari na hata inshu ya bunge live nilichukia sana.... lakini kitendo alichofanyiwa mh Nape, hakika nitawashangaa mawaziri wa CCM wakiendelea kukaa kimya katika hili....