Nape: Sina kinyongo na uamuzi wa Rais Magufuli; Akasirishwa na aliyemtishia Bastola

Nape: Sina kinyongo na uamuzi wa Rais Magufuli; Akasirishwa na aliyemtishia Bastola

Hii Nchi ni yetu sote, hakuna haja ya kuhofia MTU.......maadam hatuvunji sheria, naamini EFM watadumu na kupiga kazi kama kawaida.......Mh.Nape Jana ametuasa vijana kutoogopa chochote.
 
Umesema Sawa, Ushauri: wanasheria wakadai haki ya kikatiba ya mikutano ya siasa mahakamani badala ya kuendelea kulalamika majukwaani na kutoa matamko ambayo hayatekelezeki kama UKUTA
Zimbabwe walizuiwa wakaenda mahakamani wakaruhusiwa.hawa wetu wanasubiri events za kiki
 
1490340493981.jpg
 
Ndalichako mpaka saivi.ananiumiza kichwa....huyu mama alisie sema anataka kuipa elimu heshima mbona kwenye hili kapata kigugumizi
 
Wasomi ndilo kundi linaloongoza kwa woga.
Hivi prof.uiabudu sanamu ili tu upate kula inakuja kweli?
Hivi mtu anayeitwa daktari wa falsafa au prof. anaweza kufa njaa akiwa na akili timamu kabisa?
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Hii inaitwa Maji hayasahau Baridi......
 
NI WANAWAKE...zaidi ni wa kitanzania...
hawajiamini wamejaa uoga
Wamekuzwa kioga uoga..
Unadhani atathubutu hata mmoja wao .....
Usisahau ni VITI MAALUM
uthubutu tu wa kuomba kura hawana
 
NI WANAWAKE...zaidi ni wa kitanzania...
hawajiamini wamejaa uoga
Wamekuzwa kioga uoga..
Unadhani atathubutu hata mmoja wao .....
Usisahau ni VITI MAALUM
uthubutu tu wa kuomba kura hawana
Mkuu tofali kwani Wanawake hawana maamuzi katika kusimamia wajibu wa kazi zao?
 
Wengi ambao wana madaraka, wana akili kama yako ndo maana mabadiliko hakuna. Watu wasiokuwa na principle. Wasiokuwa na leadership skills.
Hee mbona ndani ya chadema hakuna anayekinusa kiti cha uenyekiti. Nape mlishamuita vuvuzela, mtoto but kathibitisha juzi kwa kuhandle mambo kitoto.
Kuna jinsi ya kuhandle mambo unapokuwa ndan ya system, syo serikalin tu but popote pale utafukuzwa ukifanya mambo kama nape.
Use the right approach.
 
Dah mbona habari za kusutwa Nape na matendo yake ya zamani ziko nyingi
 
Kati ya siku ambayo nimeipenda ni leo, pamoja na kulaani vitendo vilivyofanywa na bashite clouds FM, pamoja na kutema cheche baada ya kuzuiwa kuhutubia kuwa ccm uliitoa shimoni mpaka ukavunja mkono, pamoja na kueleza kuwa ulikiokoa chama cha mapinduzi kisipate kichapo na kushindwa vibaya, lakini leo hakuna mtu ambaye amekunyoonyeshea vidole kwenye chama chako kukanusha yale uliyosema, nimesikia wanazungukazungukaa tu. WEWE NI JEMBEEEE
 
Habari ya Mchana Ndugu Zangu,

Kwa Wale walio na Imani ya kikristu katika dhehebu mama la romani catholic watakua wanaelewa maana ya njia ya msalaba, lakini kwa wengine kipindi hiki ni kipindi cha mfungo na toba kwa ajili ya kukumbuka mateso ya bwana wetu Yesu kristu, mateso aliyopata kwa ajili ya kutuokoa katika dhambi, katika kipindi hiki yesu kristu anapitia mateso yote kuanzia kuhukumiwa mpaka anashinda kifo na kufufuka katika wafu,

Nimeandika baadhi ya Majina ya Viongozi vijana kabisa ambao ni Tunu kwa Taifa hili letu, Vijana hawa wanapitia kipindi kigumu sana hasa katika Uongozi huu ambao mimi naufananisha na utawala wa Roma kipindi kile cha maisha ya Yesu kristu, Katika Historia kipindi kile kulikua na Herode kama mkuu wa Mkoa na Pilato kama Msimamizi Mkuu wa shughuli za Mfalme wa Roma, Kipindi hiki kila aliekua tishio aliweza kuweka ndani na hatimae kuuliwa kwa ajili ya kulinda maslahi ya Mfalme, hii ilitokana na uwazi kwamba wananchi waliishi katika maisha ya taabu na dhiki, ulipaji wa kodi uliopitiliza, kwa kifupi yalikua maisha ya mijeledi,

Mawaziri hawa wanaishi katika kipindi ambacho rais wa Tanzania ameonyesha wazi nia na lengo lake katika kutawala kwa kutumia mijeledi kama utawala wa Roma, Hivyo basi nawaomba vijana hawa wenzangu tutembee katika njia hii ya Msalaba walau kwa Vituo Vitatu Muhimu.


KITUO CHA KWANZA
Pilato Anamuhukumu Yesu.

Pilato anamuhukumu Yesu ili kuendelea kubembeleza urafiki wake na kaisari, Japo kua pilato hakuona kabisa makosa ya Yesu kristu, lkn kwa kubembeleza urafiki wake na Kaisari anaamua kumuhukumu Yesu kristu aweze kuuawa.

Nape avuliwa uwaziri na Rais,
Hii japokua Rais hakuona kosa lolote la waziri wake wa sanaa na Michezo inamlazimu kumuhukumu kwa kumtoa cheo chake ili aweze kumlinda rafiki yake Mkubwa Ndg Paul Makonda,pamoja na jitihada zote alizofanya katika kujenga chama, Nape leo siyo lolote, hii inatufundisha tuache kutenda ubaya kwa ajili ya kuogopa watu, tusimame wima na kutenda yalio mema bila kumfurahisha mtu, hii itatujenga zaidi katika makuzi yetu ya kidunia na kiroho


KITUO CHA PILI.
Yesu Anachukua Msalaba.
Y
esu anachukua Msalaba wa dhambi zetu, Kristu anakubali kupokea msalaba huu mzito kwa ajili ya watu wake (wakristu), kituo hiki kinatufundisha sisi tuweze kutenda mema ili kumpunguzia yesu kristu mateso ( dhambi Zetu)

NAPE,MWIGULU,JANUARY,JAFO,KINGHWAGALA.
Ninyi ndio ambao mnatakiwa kupokea msalaba huu wa watanzania, kuhakikisha mateso yote tunayopitia mnaweka sawa, udhalimu wote unaoendela katika nchi hii ninyi mna nafasi kubwa katika kuhakikisha nchi inaenda mbele na watu wanajivunia utanzania wao,
Nape ameshaonyesha mfano, sasa tunasubiria niyi wengine masimame imara na sisi kama vijana wazalendo tuko tayari kutenda mema kupunguza mateso kwenu.


KITUO CHA TATU.
Yesu Anaanguka kwa mara ya kwanza.

Yesu anazidiwa na msalaba mzito anaanguka kwa Mara ya kwanza,Hili kwetu ni fundisho kwamba sisi ni binadamu, hatuna ukamilifu, tunaweza kuanguka dhambini ila inatakiwa usimame na uendelee na safari,

NAPE,MWIGULU NA JANUARY.
Dunia nzima inajua kabisa ninyi ndio mlioweka uongozi huu madarakani, ninyi ni binadamu na mlianguka katika dhambi, nawasii sana msimame na tuendelee na safari hii ya ukombozi,Nape kashaona madhara ya bao la mkono, kashakiri ni kwa namna gani alihakikisha CCM inakaa madarakani, ni kwa mbinu zote halali na haramu.

Mwisho napenda kuwapa moyo vijana hawa kama ambavyo Yesu alipewa moyo, there is nothing to fear except fear itself, ninyi ndio tunu ya nchi hii, simamemi imara, Sisi tupo pamoja nanyi.

SIMAMENI IMARA NA MTASHINDA UMAUTI KAMA YESU KRISTU.
 

Attachments

  • hqdefault.jpg
    hqdefault.jpg
    17.9 KB · Views: 53
  • IMG_4534.JPG
    IMG_4534.JPG
    23.4 KB · Views: 49
Hivi mtu ambaye ni profesa anaogopa kufukuzwa kwamba ataishije? Na mwenye degree 1? Wao kila siku wanaubiri tujiajiri vijana wao kuishi nje ya system kwa kusema ukweli wanaogopa.
 
Back
Top Bottom