Nape: Sina kinyongo na uamuzi wa Rais Magufuli; Akasirishwa na aliyemtishia Bastola

Nape: Sina kinyongo na uamuzi wa Rais Magufuli; Akasirishwa na aliyemtishia Bastola

Vitendo vyote vya Daudi Albert Bashite kuanzia kuwadhalilisha watumishi wa umma,wafanyabiashara wakubwa, viongozi wa dini, wanasiasa, viongozi wenzake wa CCM, kuwachapa vibao baadhi ya viongozi wetu wa serikali wastaafu ( Warioba), tuhuma za kugushi vyeti vya shule, kudharau bunge na kulidhalilisha, kuonyesha dharau kwa Waziri mkuu na mawaziri wengine,kudhalilisha viongozi wa vyama vya upinzani.

Na kitendo cha juzi juzi tu cha kuvamia kituo cha TV ya clouds kwa mtutu wa bunduki, na kitendo cha Nape kudhalilishwa kwa kutumbuliwa kwa kile kinachoaminika kumgusa Daudi Bashite kuvamia Clouds, kisha akadhalilishwa na askari kanzu wa Serikali hiyo hiyo akisukumwa hadharani,akatolewa bastola mchana mchana kama jambazi sugu.

Kama kweli, Nape kwa moyo wa dhati kaamua kufanya " kitu" kwa maslahi mapana ya nchi hii, kama kweli ameondoa "ukatibu mwenezi" kichwani mwake, kama kweli alijipanga vizuri kabla ya Jana.

Kama kweli hayuko "peke yake", kama kweli " hajakurupuka"

Ni wakati Sasa, Nape na " wenzake" naamini hayuko peke yake, UKAWA, bunge, (hasa baadhi ya wabunge wa CCM) ,Viongozi wa dini, wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo ( walioathirika), Vyombo vya habari,asasi za kiraia, kutumia fursa hii ya Bashite na Fursa ya NAPE kulikwamua taifa.

Fursa hii ikipita hivi hivi,naona giza mbele ya yetu kama taifa.

Kati ya makundi niliyoyataja, inabidi kuanzia Leo au tangu Bashite na wenzake walipo anza kufanya "maajabu yao" kuna taasisi inayojijua kuwa inawajibu wa kuunganisha taasisi nyingine zote nilizozitaja ili kuunganisha " ideas" na "kukwamua hili taifa".

RAI YANGU;
Hata kama Nape alifanya madudu kiasi gani kuiharibu UKAWA au chadema au bunge au mh. Lowassa, vijana hatuna budi kuwa makini na kutafakari sana na kuibua hoja na fikira nzuri za kutumia hii fursa vizuri zaidi kuliko kujikita kupambana na Nape na kufurahia kilichotokea kwake.

Washaurini, wataalam wa vyama vyetu wafanye kazi usiku na mchana kuakikisha hii "fursa " isikimbie jamani.

Naona "mwangaza kwenye hili" likifanyiwa kazi kitaalam, lakini pia naona giza mbele kama likiachwa lipite hivi hivi tu kama matukio mengine.

Tukiona la Bashite na tukio la Nape ni matukio makubwa sana yanayo karibia na nguvu na kishindo japo hayalingani na tukio la mh.Lowassa kuhamia CHADEMA na baadae Sumaye na Kingunge kujitoa CCM.

Mzee wetu wa "kubadili gia angani" hii ni nafasi tena kwake.

Mshaurini vizuri acheze vizuri mchezo utakuwa umeisha!
 
Kiongozi yoyote anae jiamini hawezi kuyumbishwa na kelele.Magu ni Raisi anae jiamini all mteuwa nape awe waziri kisha kaona hawezi kufanyanae kazi kamtoa hakuna maswali hapo.

A
 
Ebu pazeni sauti zenu SANAANE AONEKANE...haya ya BASHITE tayari MZEE ameishaonyesha msimamo wake.....
 
Mbona kitwanga alipotumbuliwa haukuhamasisha mawaziri wajiuzuru?

Magu haangalii usoni wala ulikotoka wala unanini yeye ukimpinga kaa pembeni hataki shurba
 
Hee mbona ndani ya chadema hakuna anayekinusa kiti cha uenyekiti. Nape mlishamuita vuvuzela, mtoto but kathibitisha juzi kwa kuhandle mambo kitoto.
Kuna jinsi ya kuhandle mambo unapokuwa ndan ya system, syo serikalin tu but popote pale utafukuzwa ukifanya mambo kama nape.
Use the right approach.
Wewe umeshangazwa yeye kusimamia haki bila kujali kupoteza uwaziri. Ukadai kuwa hiyo nafasi anaweza asiipate hata miaka 15 ijayo. Yeye kafikiria mbali zaidi ya urefu wa pua. Credibility yake imeongezeka zaidi machoni pa wapiga kura. Future yake kwenye siasa iko brighter zaidi Mungu akimpa uzima atawatumikia wananchi kwa mapana zaidi. Akili yako wewe ama kama ni kufikiri kwa urefu wa pua, unaona alitakiwa awe selfish tu kulinda ugali wake na aende na flow kama a dead fish. Hizo siyo skills za leadership. BTW mimi sina chama, nashangaa unaninasibisha na political parties. Unaspin kwenye no spin zone...
 
Nape wakaribishwa UKAWAAAAAAAAAAAAAAAAAAaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Magufuli na Ujinga
IMG_-9mpb01.jpg
 
Bro NAPE kokote ulipo Nathubutu kabsa kusema ya KUWA sisi WAFUASI NA WANACHAMA wa CCM...kamwe hatujarurahishwa na kuondolewa kwa WEWE kwenye UWAZIRI maana to be honest kwa kipindi hicho kifupi ulichokuwa hapo WIZARANI umeitendea haki nafasi yako na ninaamini hata RAIS MAGUFULI HILI KAMWE hawezi pinga....na pia HATA RAIS MAGUFULI kamwe hawezi pinga moja ya WATU WATANO waliofanikisha ushindi wake 2015 wewe ni mmoja wao ya hao watano.

Sasa tuje kwenye suala la kwanini RAIS MAGUFULI amekuondoa kwenye UWAZIRI...kwa hisia zangu naaamini kabsa haujawai pishana kauli wala kutofautiana na RAIS MAGUFULI ila inawezekana HILI SUALA LA MAKONDA NDIO LIMEKUONDOA....sasa limekuondoaje.

Ni hivi...bila kupepesa macho ni kweli kabsa MAKONDA anastahili kuwajibishwa kutokana na hayo makando kando anayotuhumiwa ila tatzo kubwa linalompa RAIS ugumu wa kuchukua MAAMUZI juu ya MAKONDA ni AINA YA WATU WANAOSUKA HUU MPANGO WA KUMTOA MAKONDA si watu sahihi kabsa kwa mustakabali wa nchi yetu na hapa ndipo ambapo naamini kabsa KUPITIA INTELENJIA YA IKULU imekukuta KAKA NAPE UKITUMIKA NA HAO WABAYA WA MAKONDA KUTAKA KUMWAJIBISHA MAKONDA(na ambao si watu wasafi kabsa au watu wema kwenye nchi yetu na napo sema si watu safi nadhani naeleweka vizuri kwenye hili)....NA HII NDIO SABABU KUBWA INAYO MFANYA RAIS MAGUFULI ASHINDWE CHUKUA MAAMUZI JUU YA MAKONDA maana iwapo tu akimwajibisha MAKONDA huu utakuwa ni ushindi mkubwa sana kwa hao WACHAFU.
Kingne inawezekana pia kuwa kuna sababu AWAY FROM this Mzee alikuwa anakulia Timing na ameisha kuchunguza akaona HAUPO upande wake(Mambo ya TEAM fulani) sasa kwa hili ulilo FANYA ukamvuruga kabsa.....

hivyo naamini kabsa either RAIS mwenyewe alikuonya au alitumia baadhi ya watu wakuonye ya kuwa usiwe mstari wa mbele kutaka kumwajibisha MAKONDA maana si watu wema wanaolishupalia hili either kupitia MITANDAO..MAGAZETI na REDIO PIA...sasa ndio maana RAIS alivyoona UNAENDELEA NA HII TUME ULIYOUNDA(Na ambayo kwa kiasi kikubwa tume yenyewe ilikuwa si tume ya kumtendea HAKI MAKONDA) NA HATA KUTANGAZA HIYO RIPOTI naamini he was very dissapointed with you NA HATA KUPELEKEA YEYE KUCHUKUA HAYA MAAMUZI....na ndio maana narudia kusema RAIS MAGUFULI hawezi akawa ni MTU asiyeweza au kushindwa kutambua mchango wako kwa CCM...hapa nakataa kabsa.

Nije kwenye hili suala la WEWE kuanza kulishwa maneno kupitia MITANDAONI.
Bro nakuhakikishia kabsa kwa karibu asilimia 90 hakuna MWANA CCM mwenye mapenzi mema na CHAMA CHETU hakathubutu kukubali KUTUMIWA KUKUCHAFUA wewe....WE DO RESPECT YOU A LOT.

Hili la kukuchafua wewe kwa karibu asilimia 100 lipo well enginered na hawa WENZETU wa upande wa PILI kwa minaajili ya KUKUPANIKISHA WEWE NA KUFIKIA MPAKA kuchukua maamuzi MAGUMU JUU YA CCM na kuwafaidisha wao maana wewe ni ASSET zaidi hata ya LOWASSA maana bado ni kijana unaeonekana utakuja kuwa KIONGOZI BORA SANA SIKU ZIJAZO maana nyota njema uonekana ASUBUHI.

SASA ushauri wangu kwako ni huu hapa......u just keep quit WATUMIKIE WANACHI WAKO IPASAVYO na wapiganie WANACHI WOTE WATANZANIA pindi utakapo kuwa BUNGENI na achana kabsa na MIHEMKO usifate MIHEMKO KAMA YA BASHE.....Be like kina KANGI LUGOLA wa enzi hizo au ANNE KILANGO MALECHELA wa enzi hizo au KIGWANGALLA wa kipindi hiko.

Na KINGNE CHA MWISHO usithubutu kuhama CCM we do still need you kwa mustakabali wa CCM ya kesho NA FEATURE YAKO KISIASA wewe ni hazina bora kabsa ndani ya CCM.

La mwisho even IF MAKONDA NDIO SOURCE ya wewe KUWA DROPED OUT kwenye UWAZIRI...kaka yangu NAPE nakuomba sana MSAMEHE. MAKONDA ni mdogo wako kisiasa UKITANA NAE we CHEKA NAE. Hapo ndipo utakapojipatia USHINDI kwa mustakabali wa kesho yako KISIASA.
 
Umeeleza kwa hekima sana sababu za JPM kutoMTUMBUA Makonda. Nadhani hata wao wangeekimishana hivyo, huenda wangeelewana mapemaaaaaaaaaa. Kwa sasa, kaufa kameingia CCM.
 
Hivi huu upuuzi kwamba makonda akiwajibishwa ni watu wabaya watakaopata faida mnautoa wapi?! Kumbe mtu akiiba na hao mnaowaita wabaya wakapiga kelele kuwa kuna mtu anaiba mtasimama na mwizi kwa sababu wanaopiga kelele mmewabandika jina wabaya? Poleni.
 
NIMEFUATILIA VZR YA JANA KWENYE PRESS ALIYOANDAA/ANDALIWA MH. NAPE,PAMOJA NGUVU KUBWA ILIYOTUMIKA NIKIRI HAKUKUWA NA ULAZIMA WA MH.NAPE KUONGEA BALI BUSARA-ANGETUMIA NJIA NYINGINE ZA MAWASILIANO.

WW MDAU USHAURI WAKO NI UPI ILI TUJENGE NCHI KWA PAMOJA BILA KUTILIANA MASHAKA NA TENSION ISIYO NA SABABU.
 
Usimdanganye. Acha ahame akatafute marisho bora. Unamchelewesha maana had I 2025 ni mbali mno. Likatiba mmeruharibu.
 
Mkuu kwa hiyo Magufuli hufanya maamuzi kwa kuangalia watu fulani wanasema nini, mbona juzi kasema yeye haambiwi cha kufanya na wala hapangiwi
 
Too late , alimfunika mwigizaji wenu jana. Nape aliongea kitu wanachotaka kusikia watu kutokana na matatizo ya zama hizi.
 
Back
Top Bottom