Binafsi mimi kama mpiga kura wako na mwananchi wa jimbo la Mtama nampongeza Mh. Rais kwa maamuzi ya kutengua nafasi yako kama waziri, Na sisi wanajimbo la Mtama tutakuunga mkono kama wananchi ambao tumekupa kura za kuwa mwakalishi wetu na tunafikiri itakuwa nafasi mzuri kwako kuja kutuhudumia sisi wapiga kura wako ambao kwa kiasi kikubwa ni kama umetutenga kutokana na kivuli cha “UWAZIRI”
Nasema hii kwa kuwa niliona kila dalili za kumfuata mtangulizi wako Bw. Membe ambaye na yeye alikuwa anajificha kwenye kivuli cha “UWAZIRI” na yeye alikula pesa za marehemu na akala zile za kiwanda. Nawe pia nilikuwa nakuona pia upo kwenye kasi ya ajabu kumfuata mtangulizi wako ulikuwa upo busy kuipigania Singida Utd na kumfunga ndg Selemani Methew ambaye alikuwa anaipigania Kariakoo ya Lindi na timu zingine za mkoa wa Lindi. Nafikiri unatambua ni kwa kiasi gani wananchi wa Mtama jinsi wanavyokuchukia na bado yale maneno yako ya kipindi cha kampeni yapo kwa wananchi wa Mtama, si unakumbuka kipindi cha kampeni wananchi walikuzomea mpaka ukatoa Bastola na kuipiga hewani risasi kadhaa..? Na lile tukio la kuzomewa mpaka ukalia ndani ya gari pale PHAISHA LODGE si unakumbuka pia na mpaka wananchi inafikia hatua wanakuombea dua mbaya mpaka unapata ajali haujajifunza tu..? haujui ni kiasi gani wananchi umewakwaza…!
Unakumbuka ahadi zako kupitia “SMS” yako ya Oktoba 11, 2015 kwa wapiga kura wako..? nakukumbusha kwa sababu najua unapita humu kwa Id fake ya __, Ulisema MAJI, BARABARA ZA VIJIJINI, UMEME, MTANDAO WA SIMU, HUDUMA ZA AFYA & SUALA LA ELIMU vitakua historia.
Kuhusu “MAJI” hapa mtangulizi wako afadhali kidogo alianza na mradi wa maji CHIUE kupitia Nyangao na wananchi tulijitolea nguvu zetu kuchimba mitaro, Lakini tangu Utawala wako mbunge wangu umebadili uelekeo sasa unataka kuchukulia maji RONDO ili mradi upitie unakojenga nyumba yako kule Makasini na hakuna dalili yoyote ile ya mradi kuanza, wananchi wako huku wanakunywa maji ya mto Lukuledi ambayo si masafi na si salama achilia mbali wale wa kata za Nyangamara na Mandwanga ambao wanakunywa maji yaliyotuama.
Kuhusu “BARABARA ZA VIJIJINI” hapa ndio mbaya kwa kweli barabara hazipitiki na hakuna halmashauri ambayo ina barabara mbovu kama ya Lindi ikiongozwa na jimbo la Mtama na hata ile barabara ambayo umeichonga ili uweze kwenda kijiji cha SHUKA ambako umenunua zaidi ya ekari 200 nayo sasa hivi haipitiki kabisa na hata watumishi wanapata shida kwa kweli. Uliahidi na umeshindwa kutekeleza.
Kuhusu “MTANDAO WA SIMU” mkuu sana na mh. Mbunge wangu wa jimbo la Mtama hapa napo umefeli kwa kiasi kikubwa, si unakumbuka mwaka 2015 ulivyoenda kule kata ya Mandwanga ambako unasema ni chimbuko la mzee Mosses Nnauye…? Unakumbuka uliwaahidi nini wale ndugu zako kuhusu suala la mtandao wa Simu, achilia huko pia sehemu kubwa ya jimbo lako mawasiliano ni shida.
Kuhusu “HUDUMA ZA AFYA” hapa sitaongelea chochote kwani tangu utoe vile vitanda pale Sokoine mwaka juzi na Wana-CCM kindaki ndaki kutamba mtaani huku wakisema kuwa umeanza kutekeleza ahadi zako sijaona kingine chochote mpaka sasa hivi.
Kuhusu suala la ELIMU, hapa mbunge wangu unafeli na unafanya maamuzi yako kupitia mitandao, tangu kipindi kile ilivyosambaa video na picha ya S/M Msingi Litingi iliyopo Nyangao na ukaikarabati mpaka leo hakuna jambo linguine kuhusu shule. Kuhusu ELIMU kuna Organization inaitwa SEDO inafanya “INSPIRATIONAL VISIT” kwa shule za kusini umeombwa kushiriki umekataa katakata, nakuomba Mh. Sana mfuate jirani yako mbunge wa Nanyamba Mh. Chikotta muulize amewezaje kutembelea shule na kusaidia kupunguza changamoto zinazowakabili wanafunzi na pia kuwapa hamasa au haujamsikia Mh. Bashe alivyowaahidi wanafunzi wa kidato cha nne endapo watafaulu kwenda kidato cha Tano..?
Jambo la kushangaza kuliko yote ofisi yako ya jimbo mpaka leo haina Katibu wa
Jimbo
Njoo jimboni tufanye kazi.