Nape: Sina kinyongo na uamuzi wa Rais Magufuli; Akasirishwa na aliyemtishia Bastola

Nape: Sina kinyongo na uamuzi wa Rais Magufuli; Akasirishwa na aliyemtishia Bastola

Mi hayo mengine nafahamu tatizo ni Mwana Mfalme lakini kuna jambo nimesikia kwahiyo mwenye maelezo ya kutosha basi nami anijuze!

Inasemekana eti watu wenye ndinga kali town wanaogoa kuzi-drive kwa hofu Daudi akiziona tu, atataka apewe yeye na ukigoma; anakutia kwenye list ya drug dealers!
 
Hakutenda kosa lolote lile ambalo lilistahili afutwe uwaziri. Alifanya kile alichostahili kufanya kama waziri. Cha kustaajabisha huyu uchwara anasema Mawaziri wasimamie haki lakini yeye ndiye kinara wa kupindisha sheria za nchi. Mfano mmoja tu ni Bashite na vyeti vyake vya kufoji na uvamizi pale Clouds. Na upo ushahidi mwingine chungu nzima wa jinsi anavyopindisha sheria za nchi.
Kosa lake: Alifanya kazi ya Raisi bila kutumwa na Raisi. In administrative law is called excess of powers,usurping of powers,Ultra vires. Aliunda kamati kumchunguza mteule wa Raisi bila kutumwa na Raisi. This is absolutely ultra vires. Ilikuwa au ajihuzuru au atumbuliwe. There was no shortcut.
 
Kuna mfalme anapenda kusifiwaaaaaa huyo acha kabisa. Anapenda muda wote iwe vipindi vya sifa kwa mfalme. Akikosea aaachwe kisa fom alijichulia menyeweeeeh
 
Rais Magufuli Jana kaweka wazi kilichomtumbua Nape japo kwa Njia ya Mafumbo

Alimwambia Mwakyembe kuwa Mtangulizi wake ( Nape) alikuwa anasita kuvichukulia hatua Vyombo vya habari vinavyoonesha Migogoro kwa Muda mrefu na habari za kichochezi chochezi na akamtaka Mwakyembe 'akafanye kazi'.

Ile ya Clouds na Timbwili la Madawa ya kulevya ilikuwa ndo Sababu ya Mwisho Ila ilishaonekana Nape kamchoka Magu na Magu kamchoka Nape,
 
Kutumbuliwa kwa Nape kumeacha maswali mengi na mjadala mkubwa huku wengi wakijiuliza ni kosa gani kubwa alilolifanya hadi kupelekea kupokwa wizara aliyokuwa akiisimamia!
Najua kuna wenye ubuyu wa uhakika juu ya kutumbuliwa kwake, hivi kosa lake kubwa ni lipi maana hata hakuna taarifa iliyotolewa ikulu kama pengine alijiuzulu kama inavyosemekana au la!
Wanaofahamu kosa lake kwa jamii hadi kutolewa na mteule watueleze...
Ulikuwa ni mtego hakutumbuliwa, bali aliletwa mtu mwingine kwenye nafasi yake bila ya yeye kuambiwa chochote
 
Dili lake kunyakwa, aliposhindwa kulificha ndani yake Jumatatu. Huku wanampa timing tamuuu tangu kabla, akalewa kusifiwa Mtwara akaingia mkenge.

Kisa RC mpendwa aondolewe kazini.

Makonda oyeeeee
 
Kutumbuliwa kwa Nape kumeacha maswali mengi na mjadala mkubwa huku wengi wakijiuliza ni kosa gani kubwa alilolifanya hadi kupelekea kupokwa wizara aliyokuwa akiisimamia!
Najua kuna wenye ubuyu wa uhakika juu ya kutumbuliwa kwake, hivi kosa lake kubwa ni lipi maana hata hakuna taarifa iliyotolewa ikulu kama pengine alijiuzulu kama inavyosemekana au la!
Wanaofahamu kosa lake kwa jamii hadi kutolewa na mteule watueleze...
Kosa kubwa kama kiongozi ni Ku mis handle suala zima la Clouds.

Kivipi,

Hadi anachukua uamuzi wa kutembelea Clouds, alikuwa hajapokea official complain from Clouds au MOAT.

Pia alikurupuka kutoa tamko la kujiuzuru iwapo itabainika kuwa ni kweli Makonda alikwenda Studio za Clouds

Kwa hiyo alikuwa ana maslahi binafsi na Makonda kama subject not object.
 
Kosa kubwa la nape ni kusimamia haki na sheria kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi, katika kufanya hivyo akawa amemgusa mtoto mpendwa wa mkulu
 
Hakutenda kosa lolote lile ambalo lilistahili afutwe uwaziri. Alifanya kile alichostahili kufanya kama waziri. Cha kustaajabisha huyu uchwara anasema Mawaziri wasimamie haki lakini yeye ndiye kinara wa kupindisha sheria za nchi. Mfano mmoja tu ni Bashite na vyeti vyake vya kufoji na uvamizi pale Clouds. Na upo ushahidi mwingine chungu nzima wa jinsi anavyopindisha sheria za nchi.
Kwani rais kumchomoa waziri ni hadi waziri afanye kosa? Kuondolewa kwa Nape kumevunja sheria au katiba ipi? Acha ushabiki na mihemko...reasoning yako inapaswa kuwa rational...sio kuwa guided na emotions..
 
Kimsingi yule ni kijana wake.. hata yeye alikuwepo eneo la tukio. Najiuliza kwa nini kamera hazikumuonesha usoni mshika bastola
haitaji kumuonesha usoni ndio afahamike,,,yaani ata wakipangwa 300 kwenye mstari naweza kumtambua bila shida yoyote licha ya kwamba hakuoneshwa usoni.
 
Nilikuwa nashangaa sana kuona Nape anasema kuipinga serikali hadharani, nikajiuliza huyu ni Nape kweli au kuna jambo jingine nje ya boksi.

Maana nimeshuhudia matukio mengi mengi ya hovyo Nape akitetea kipindi cha Jakaya leo hii anajidai kabadilika km sio unafiki nini.

Tumeshuhudia akitetea makosa makubwa hadharani leo Magufuli ndio shujaa eti huu ni unafiki ni kampeni za chini chini ili serikali ya Magufuli ionekane inachukiwa zaidi na zaidi.

Kumbukeni Nape alikuwa team Membe hivyo hapendezwi kabisa kuona Rais watu akiongoza nchi hii kwa nia njema.

Issue ya Clouds ni kweli Makonda alichemka angempigia simu tu Ruge na kumuuliza mbona vijana wako hawarushi issue ya Gwajima?.

Nafikiri angefahamishwa na Ruge jinsi ilivyo na taratibu zipi zilikuwa zinasubiliwa.Nape alichochmka naye kwa hili yeye ni serikali.

Makonda pia ni serikali kwanini huyu waziri wa Diamond asimuhoji kwanza Makonda ili ajue kuna nini chini ya kapeti sasa yeye Nape alitaka kufurahisha media tena akizidi kwenda mbali akaunda kamati je hiyo kamati ilimuhoji Makonda?.

Je Nape alimuhoji makonda? Au Nape alimpigia simu Boss wake? Kama jibu ni no nikisema Nape alikuwa na interest zake tafauti na za issue hii.

Nape kafanya madudu mangapi kazuia bunge live kafungia magazine mangapi. leo Nape awe shujaa no no Big no. Nape siku zone anatetea serikali siku zote liwe jema au baya anatetea kipindi cha JK vipi leo Magufuli au ana hasira za Membe kukosa Urais.
 
achana na huyo mleta mada kwani kaonekana bado yupo nyuma na teknolojia, tujipange kudai uhuru toka kwa wasukuma wawili kama ilivyokuwa mwaka 1961
Tafadhali usilipe hili suala sura ya ukabila.

Kwanza kabisa Magufuli si Msukuma. Nyie msiowajua Wasukuma ndio mnamuita Msukuma.

Pili hata mimi Msukuma na sitaki ujinga huu unaoendelea.
 
Kuwa na watu wa propaganda katika chama cha siasa ni kitu cha kawaida sana,lakini pale unapokuwa na wapiga propaganda wenye akili ndogo ni hasara kubwa kwa chama husika.
 
Hili la nape ukiangalia kwa jicho la tatu. Ni style ya uongozi wa kupenda matukio kwenye press conference. Hata Dr Mwele dada yake fulani wa uswazi media yalimkuta na hatuwezi kuwalaumu haya wameyarithi toka juu.

Imefika wakati kila kiongozi anataka akitenda jambo kuwe na waandishi wa habari na itoke kwenye matv na redio breaking news.
 
Yale yote yalikuwa maigizo wewe muangalie Kitenge alivyo kuwa anaongea na yule wanao muita askari hadi wakaelewana hahahaha
 
mkuu unatiming nzuri yaani kila post lazima utokee, tena unakuwa wa kwanza kwanza. sasa kwa nini usifungue tuakaunti twingi twingi ili kuo geza wingi wa supports wa bwana mkubwa?

Kwani kuna tabu yoyote!?

Tabia yenu ya kufungua ID nyingi kuandika juu ya jambo ndio unataka nifanye mimi kabisaaa eeeeh, hivi hukuweza kufikiria lingine. Inaelekea ndio zako hizo.
 
4cb0503eef1403e9df5e4414678a337e.jpg
 
Back
Top Bottom