Napenda kujua kwa namna gani mashushushu duniani wanaweza kutambuana

Napenda kujua kwa namna gani mashushushu duniani wanaweza kutambuana

Halafu ni wapi wanasomea hii kitu jamani? Navutiwa na kuwa shushushu
 
Wanapenda kujifanya magentlemen au charming hasa pale wanapotaka kukutumia, wanakuwa na ratiba ambazo wewe huzielewi, wanaongea shortcut sana, ukimuuliza swali anajibu short cut bila maelezo ya kujitosheleza, pia wana sifa ya kutembea na magazeti wakijifanya kusoma kwenye vituo vya usafiri au vya kupumzikia, wanapenda kujikausha sana kama hawajali au hawafahamiani na mtu yeyote yule.
[emoji4] [emoji4] [emoji4] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Halafu ni wapi wanasomea hii kitu jamani? Navutiwa na kuwa shushushu
kwa nchi yetu,watakutafuta wenyewe,unaweza ukawa shule wakakustudy na kuona unafaa,ukawa informer,baadae ukapata training na kuendelea,
kama tu unataka kuwa detective si unaanzia polisi then unaweza kuwekwa criminal investigation,

kwa nchi kama marekani wao unaweza kuapply,

How to Become a CIA Agent | CIA Agent Education
 
Mkuu watu kama hao achana nao tu maana akili yao ni mbovu. kwao wao lolote analofanya mzungu au rai wa kigeni ni zuri hata kama ni hovyo. hawajui kwamba mbinu na nyenzo za kazi hiyo ni sawa tu duiniani kote, tofauti ni vipaumbele, rasilimali (teknolojia na fedha), na mazingira.......
They are damn sick.
 
shushu mzuri ni yule anaeweza kujiblend katika watu na asiweze kutambulika iwe na mtu wa kawaida ama na shushu mwenzake.
Shushu anamtambua shushu mwenzake kama atakosea akajiexpose,
mfano kama shushu mmoja anahofia kuwa anafuatwa na mashushu wengine,atakachofanya ni kurun Surveillance Detection Run(SDR),
yaani anaweza kuwa anatembea,ghafla akageuka na kurudi alikotoka,kisha ghafla akadandia bodaboda akifika mtaa unaofuata atandandia daladala,kisha likisimama kituoni,atashuska dakika za mwisho,
ataingia kwa mfano bar na kukaa sehemu anayoweza kuona kila anaeingia,
sasa kama wewe ni shushu njaa,atakung'amua mapema tu kwamba i have grown a tail,yaani kuna mtu anamfuata,
ndo maana wenzetu sikuhizi wanatumia drone kufuatilia mtu,maana shushu makini huwezi kumfuata atakugundua tu
Aisee
 
The only way Mashushushu wanaweza kutambuana ni pale wanapoingia wote kwenye operesheni katika eneo moja au wanapowindana. Shushushu akiwa kwenye operesheni lazima akifika sehemu asome mazingira. KAtika kusoma mazingira anaweza kuona kwamba kuna mtu ana characteristic fulani ambazo zipo out of place katika watu waliopo pale anaweza akawa yupo too careful au amejiposition mkao fulani wa kuzuga..
 
Wanajuana sna tu tena kikawaida Mashushu usifikir ni kundi kubwa la watu hapana hiyo ninkazi inayohitaji usiri mkubwa na ndyo maaana ni watu wachache ambao kujuana ni rahisi kila mkoa wapo na wanajuana kawaida tu
 
Mie nikiona kavaa kaunda suti kaweka na pen kwenye shati kisha kanyoa ndevu zote na nywele kapiga unga nakimbia fasta hapo maana utakuwa unadukuliwa .
 
Back
Top Bottom